Ni mauzauza gani ulishawahi kukutana nayo barabarani?

Ni mauzauza gani ulishawahi kukutana nayo barabarani?

Dah umenikumbusha, hiyo ya kukatiziwa na nyoka nimekutana nayo mara zaidi ya tatu. Unajuwa mume wangu kazi zake Tanzania ni za kusafiri sana na hupenda kufatana nae. Siku hiyo tunatoka Tanga tunarudi Dar., kabla ya kufika hale bonge la nyoka limetoka kulia kwenda kushoto mbele ya gari, mume wangu kasimamisha gari, laktupita taratibu, kumaliza njia kufika kushoto kanyanyuwa kichwa, mume wangu akaondosha gari akasema, anatwambia ahsante. Ile scene nilitamani ingekuwa nimeipiga picha, ilikuwa nzuri sana.

Dah, nna visa vingi sana vya safari za Tanzania na nje ya Tanzania, ntakuwa nawapa kidogo kidogo. Vinapotokea unaona vya kawaida tu, lakini baadae ukivifikiri vinakuwa ni "adventure".

Mimi nashukuru Mungu, nimesafiri sana hii Tanzania na duniani kwa ujumla. Mwenyezi Mungu alimjaalia kazi za safiri mume wangu na mimi huwa nakuwa betri kila inapotokea fursa.
Leo amesafiri naona upo jf muda huu saa nane usiku
 
View attachment 2870193

Nakumbuka tulikuwa tunatoka kijijini Kibungo wilaya ya Kigamboni, tunaelekea Pemba Mnazi kuogelea.


Tulipokuwa tunaingia Pemba Mnazi, barabara imefunikwa na kivuli kikali cha miti mikubwa ya miembe.

Katikati ya kivuli ukatokea mwanga mkali sana kiasi cha kutufanya tusiweze kuona mbele.

Basi wale wamama niliokuwa nao wakaanza kukemea, mara mbele katikati ya barabara kakatokea kababu kamevaa nguo zote nyeupe, kana ndevu nyeupe, kamekaa chini barabarani.

Basi nilikuwa naendesha Mark ll Super Charger ya boss TAJIRI MKUU WA MATAJIRI, bwana ehh, kazee haka hapa, nikakwepe au nikagonge?
Ile nimekakwepa,, mara bonge la shimo hili hapa, ndio gari inaenda kuzama. Pongezi kwa wana maombi.

Tukarudisha gari nyuma, wananchi wanapiga miluzi kama yote, mna bahati sana nyie, huu ni muda wa majini kwenda kuswali, kweli MUNGU wenu ni mkubwa.
Hatari sana
 
Yes, barabarani kuna visa vingi.
Miaka kama 10 hivi nilikuwa nasafiri kwenye basi jina Born city toka Arusha kuelekea Singida.
Baada ya kupita Endasak, kuna Mwiraq alikuwa amesimama ukingo wa kulia mwa barabara, gari ilipokaribia alijirusha katikati ya barabara, jambo la kushangaza sikusikia kishindo cha kugongwa wala dereva hakushtuka wala kupunguza mwendo.
Duh, dereva naye alikuwa kajisindika
 
Visa vingi sana, kimoja wapo; Nilikuwa nasafiri na mume wangu, kufika mikumi tukaenda Snake Park, kuna Restaurant nzuri pale, baada ya kula tunatoka nje tukamkuta kijana mmoja akatwambia na yeye hajala, tumsaidie akale, mume wangu akampa pesa, tukaondoka. Tunafika mbele kidogo kuelekea ilima vya uaha kuna getilipo karibu na reli, tukasimamishwa, ile tumesimama askari wawili wakaja, mmoja akauliza mnaenda wapi, mume wangu akamwambia Iringa, yule askari akamwambia, "mzee tuwachie chochote, getini hapa mambo magumu" ile mume wangu kabla hajasema chochote yule askari mwenzake akamwambia, tayari wazee hao wameshatupa pesa ya kula, kumtazama ni yule kijana alikuwa pale Snake Park aliyepewa pesa na mume wanu na alikuwa kavaa kiraia sasa yupo kwenye magwanda. Yule askari akatwambia haya safari njema wazee.

Hilo tukio lilitushangaza sana na mume wangu, mpaka leo tunashindwa kupata jibu.

Mie huwa nayaita, majegajega ya mikumi.
Aisee, kumbe na wewe shule ulienda kusomea digrii ya ujinga
 
Write your reply...Yaani nihatari tupu barabarani , kunasiku nipo na chopa yangu rodini mida ya saa4 usiku nikawa nakutana na warembo kibao. Aiii! mara nakatiza kipori flani hivi mara nakutana na kademu nikajisemea chakujitesea nini nikatupia vocal kiaina dakika mbili mtoto katiki piga gori mbili chapu nikaendelea na safari Aise!! yani barabarani mauzauza nimengi mno ni Nungutu anatuepushia na madhara yake yanakuwa machache.
 
Yes, barabarani kuna visa vingi.
Miaka kama 10 hivi nilikuwa nasafiri kwenye basi jina Born city toka Arusha kuelekea Singida.
Baada ya kupita Endasak, kuna Mwiraq alikuwa amesimama ukingo wa kulia mwa barabara, gari ilipokaribia alijirusha katikati ya barabara, jambo la kushangaza sikusikia kishindo cha kugongwa wala dereva hakushtuka wala kupunguza mwendo.
Khaaa ulikaa siti ya ngapi ukamuona?
Unajua hata prado TX ikiwa kwa mwendo kwenye tuta uhisi kama umeligusa🤣🤣.
 
Back
Top Bottom