Juzi jumatano nilikua namnunulia mtu voucher kwenye max malipo ya elfu 10 nikakosea namba ikaenda kwa mtu mwingine. Leo asubuhi nilikua namtumia dogo hela nikakosea hapa nasubiri ndani ya hizi siku 3 irudishwe hiyo hela maana ilikua ni hela ya dogo nimepewa na mtu nimpe ikapitishwa kwangu.
Kinachoniuma zaidi ni sasa hivi nilikua nalipia tena king'amuzi nimekosea namba elfu 69 yangu imeenda na maji.
Inawezekana nina mawazo sana bila kujijua ndo maana nakosea sana au nimekua mzembe tu? Maana hali Hii si kawaida kabisa