DJ SEPETU
JF-Expert Member
- Apr 17, 2017
- 8,413
- 12,336
Mkuu upo safichangamoto za kimaisha ukichanganya na maisha binafsi inaweza kuwa chanzo cha mambo haya.
nakushauri nenda eneo la bustani ukiwa na chupa ya maji kama lita na nusu peke yako kaa ukimya ukitafakari moja baada ya lingine na kisha kupata majibu kisha ndo tafuta mtu wa kushare naye kwa yale ambayo majibu hukuwa nayo ya kutosha huku ukilinganisha na ya kwako.
yapo mengi lakini nafikiri haya yanaweza kuwa msaada kwako.
- katika kujadili kwako anza na mafanikio kisha matatizo na hapa matatizo utaona ni changamoto usianze na mtatizo kisha mafanikio hutaondoa stress.
- jitahidi usijihukumu na mshushe kila mtu aliyekukwaza na uliyembebaikiwezekana waweza kumpigia simu ya kumsalimia na hata asipopokea usijali ruhusu moyo usukume damu na sio machungu.
- tumia muda pia kujadili uchumi wako kwa kuangalia nini ulipanga mwaka jana kipi hakikwenda na kipi unafikiri unaweza kuendelea nacho na ni kwanini?
- panga upya mambo yako ya mwaka huu kwa kadri ya resource chache ulizonazo
- yatazame mahusiano yako yakoje, na angalia jinsi ya kuyaboresha ukianza kuangalia mapungufu yako kwa mpenzi wako na sio yake kwanza. anza kubadilika wewe kwanza kisha mwenzako
Ila hapa ni nyeegee