Ni vizuri zaidi kumshukuru na kumuomba mungu kila wakati, bila kuchoka wala kukata tamaa.
Sio tabia njema wala sio tabia nzuri kujenga mazingira au hali ya huruma na kuombaomba kwa wanyonge ambao hawawezi kukataa kuchangia kwasabb wamefundishwa utamaduni kutoa. Utamaduni na malezi haya sio fursa ya kuchangiwa ndugu zangu [emoji205]
Ni vizuri na muhimu sana kujifuza kujitegemea. Kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato cha kutosha na kuepuka fedheha na aibu ya kutegemea kuomba na kuchangiwa mara kwa mara.
Ni aibu na fedheha kubwa kwa wana familia, ndugu, jamaa, marafiki na taasisi uliopo na kwamba kuomba omba kwako kuna maanisha, hawakujali, hawana uwezo, hawakusaidii na hawana kabisaa msaada kwako. Unawaumiza, unawafedhehesha hawasemi lakini wanaumia sana, hujui tu [emoji205]
Ingekuwa akili inaweza kuchangiwa, ningekushauri uombe uchangiwe akili.
Mwalimu wakati anaenda UN kutafuta uhuru wa Tanganyika, gharama za safari yake zilichangiwa na wote waliokuwa na uwezo na dhamira njema. Hata wakati anazunguka nchi nzima kuwaelimisha watu, maisha yake yote yalifadhiliwa na watanzania wenye dhamira njema na nchi yao ya Tanganyika.
Ungeonekana ni mwendawazimu wa kiwango cha juu sana kama eti ungeanza kusema kuwa Mwalimu hakustahili kuchangiwa. Alikuwa na kazi ya mshahara, akaacha kazi ili awakomboe Watanzania, hana mshahara, unataka ale nini, aishi wapi, asafiri na nini, wakati ameamua kuacha yote kwaajili ya Watanganyika? Utakuwa ni kichaa kama unafikiri hakustahili kuchangiwa.
The same applies to Tundu Lisu. Ameacha yote, ameacha kazi za mshahara, ameamua kuwapambania Watanzania na nchi yake, anafanya hiyo kazi bila ya kuwa na mshahara. Halafu mwehu mmpja anasema eti hastahili kuchangiwa. Unamlisha wewe, anaishi kwako, anasafiri kwa gari lako?
Lakini pia kama wewe ni kapuku kabisa, hujalazimishwa kuchangia. Au kama wewe ni mtu mnafiki ambaye huoni umuhimu wa kazi anayofanya Lisu, kaa na pesa yako. Hakuna atakayekufuata nyumbani kwako kuwa eti unatakiwa kuchangia ununuzi wa gari ya kutumia Lisu. Hujachangia chochote, hujalazimishwa, lakini kwa ushetani wako, unaumia kuona wapo watu wanaochangia! Si bure, ni mgonjwa wewe.
Watu wote wanaofanya kazi kubwa za kujitolea kwaajili ya watu wengine, wanaopokea hiyo huduma, wenye uwezo, akili, na dhamira njema, huwa wanachanga ili kumwezesha huyo aliyejitolea kwaajili yao, aweze kumudu majukumu yake. Ndiyo maana huwa tunachanga kununua magari ya mapadre, maaskofu, hata mashekhe. Ikilazimu huwa tunachanga hata kuwanunulia mavazi ya ukihani. Tunachanga kwaajili ya chakula chao. Na hiyo siyo hisani, bali ni wajibu wetu kama wanufaika wa huduma yao.