Ni mbinu gani unatumia kubalance shobo kwa mpenzi wako?

Principle ya kuishi vyema na mpenzi haswa katika njia ya mawasiliano

1, piga simu asipopokea usipige tena mpaka yeye akutafute na akikutafute usimuulize why hujapikea simu yeye ñdio atatoa maaelezo .,kama asipo toa maelezo wewe cool mpe Hi then kama kuna mawili matatu fresh

2,Tuma SMS mbili au moja kama ni morning asipo jibu on time usiendelee kutuma huu ni usumbufu kama ni asubuhi mjulie Hali ameamkaje,kama ni mchana mejulie za mchana kashindaje then mtakie mchana mwema Kwa jioni unaweza mpigia simu na kuongea nae mawili matatu kuhusu yeye then kama nyie ni wapemz wa wale wa kuongea mda mrefu mtanendelea

3,Usiwe mtu wa kupiga simu kila saaa pasipo Sababu ya msingi, hapa wapo wale sijui nimekumiss mara sijui nn nimemiss kusikia sauti yako bla bla bla kibào hapo utachokwa na kuonekana haupo seriously kbsà


4 Be serious to increase you're value ,kama Kuna mengine mtamalizia
 
Mburaa...
 
Me nikituma text pasipo majibu siongezi text juu ya text ambayo haijajibiwa. Nikipiga call hujapokea na haujani flash back siongezi mawasiliano juu ya mawasiliano hajajibiwa.

Mwanaume hajaumbwa kutuma good morning text tuu. Mwanamke ukiona yuko mguu ndani mguu nje ujue wewe ni substitute au mko wawili anashindwa pakuegama.
 
Shobo ni nini hasa??
 
Kupenda kupitiliza hakujawahi kumuacha mtu salama, mpe muda mwenzi wako. Tuma sms ya kumtakia asubuh njema, mchana mwema na usiku mwema inatosha. Kama anajar basi katika reply za sms hizo ataonesha muendelezo wa ww kuchat nae. Na kama hakuna muendelezo basi kausha na ujue haitaji kujari kwako. Ila pamoja na yote hakikisha kila unapomuhitaji faragha unampata kwa wakati. Kama faragha naye pia shida basi kunywa Panadol Kisha chukulia unalazimisha mapenzi.
 
🤣Hata akiwa ukanda wa gaza atumie basi satellite phone anipigie wakati wanapambana nisikie milio ya risasi na mabomu hapo nitamuelewa
nimecheka sana hiyo ya ukanda wa gaza
 
Binafsi nimekuelewa.
 
🤣Hata akiwa ukanda wa gaza atumie basi satellite phone anipigie wakati wanapambana nisikie milio ya risasi na mabomu hapo nitamuelewa
nimecheka sana hiyo ya ukanda wa gaza
Weeee chekaa tu... Omba Mungu yasikukutee ndg......
 
Hii ya kumtumia msg asubuhi,mchana ndo siwezi
Mwanamke akiwa na utabiri wowote juu yako atakuchkulia poa
 
Yeah na hiki mimi ndio kimesababisha hata kumtumia ujumbe siwezi labda aanze yeye

Maaana akishajua unamtegemea sana hata penzi utalisikia kwenye bomba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…