Ni mbinu gani unatumia kubalance shobo kwa mpenzi wako?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]we kiboko...wacha nidese hapa
 
Yeah na hiki mimi ndio kimesababisha hata kumtumia ujumbe siwezi labda aanze yeye

Maaana akishajua unamtegemea sana hata penzi utalisikia kwenye bomba
yeah naweza kubaliana nawe kiukweli huwa naiona hata kwenye mahusiano yangu huwa namtafuta sana mwenza wangu ila yeye haoneshi na hii imepelekea kupigwa pesa maana anajua unampenda ila pia kiukweli kama utaweza punguza mawasiliano huu ni ushauri wa bure maana kuna mtu unakuwa nae kwenye mahusiano wewe kutwa ndio unamtafuta hadi unajishusha thamani kabisa ,unajiona Mungu hayupo nawe mbaya zaidi unampigia hapokei na hajibu text ila whatsup unamuona kila mara
 
kiukweli hii ni njia sahihi kabisa ya kudeal na mahusiano maana unaweza kuwa unaforce bini kulazimisha mwisho wake utapigwa pesa na utabaki kujilaumu mi nafikir wewe tizama wajibu wako kwa kumtafuta na sio mara kwa mara nikisema hiv nishajifunza ukimtafuta mara kwa mara kwa baadhi hasa ya watu anakuona wewe ni looser fulani so ukimtafuta na asipopokea tulia akutafute ukiona hajakutafuta the whole day na next day ujue tu kitumbua kimeingia mchanga
 
Kwel mapenzi ya siku hizi yamekaa kuviziana viziana tu
Hakuna anetaka kuonekana kazimika kwa mwenzie
 
hahahah kitumbua kimeingia mchanga.
 
Mimi siwezi kubalance, yaani kama simu ntapiga, sms ntatuma. Bila kujali sana yeye kanitafuta or not. Nampenda why nimpimie.
sasa kama unampigia yeye hana muda wa kukutafuta yaani kila siku wewe unamuwaza yeye anakutafuta pale anapojisikia ,unafikiri bado utaendelea kumtafuta mbaya zaidi unampigia simu hakutafuti ila whatsup unamuona online sasa unajiuliza hiv huyu ni kwamba simu zangu hazioni au[emoji24][emoji24]
 
Hautakiwi babu jikatae
 
Nikweli mkuu, hiyo ni mbaya kama unamuona online na hapokei mmh, mimi nasemea ile ukimtafuta anakujibu, or anashindwa sababu yupo busy na kazi kidogo ila akipata chance anakucheki back.
 
Nikiona najipendekeza huwa nafuta namba kwanza , huku nikiamini kama tupo pamoja atanichek ,akinichek Wala Simind tunaanza upya akizingua nafuta tena naendelea na ishu zingine
 
Kwel mapenzi ya siku hizi yamekaa kuviziana viziana tu
Hakuna anetaka kuonekana kazimika kwa mwenzie
shida iliyopo ni kuwa ukizimika mwenzako anakuona boya ,yani unamtafuta mtu mara kwa mara yeye hana time na wewe sasa hapo hayo mapenzi haya ushirikiano kabisa ,maana ukifanya wewe utaonekana mbaya ila kikubwa ni kujitambua japo hili ni gumu sana hasa ukishampenda mtu
 
Nikiona najipendekeza huwa nafuta namba kwanza , huku nikiamini kama tupo pamoja atanichek ,akinichek Wala Simind tunaanza upya akizingua nafuta tena naendelea na ishu zingine
hii ndio njia sahihi ili kuishi kwa usalama japo kama umeshaikariri namba ndio itakuwa changamoto kubwa sana ,kikubwa ni kuacha kukariri namba
 
Nikiona najipendekeza huwa nafuta namba kwanza , huku nikiamini kama tupo pamoja atanichek ,akinichek Wala Simind tunaanza upya akizingua nafuta tena naendelea na ishu zingine
mfano ukimwambia mbona online nakuona lakini hunitafuti anakwambia niliingia mara moja tu ,je utamuelewa
 
Huu jamani kubalance shobo ni muhimu mtu unamtext online sms zinafika hajibu znafikabtena hajibu jua huna chako hapo, we endelea na mambo yako ubize upo ila kaa kimya ubize ukimuisha atakutafuta asipokutafuta be kimyaa
 
daaah huo ni ukweli japo ni mchungu sana ,tujaribu kuwasaidia wale ambao wanaweza kuona dalili zote lakini bado anahisi kupendwa mfano anapiga simu hazipokelewi na bado unamkuta online ,unatuma sms hazijibu ,unatuma sms whataup hata kuziangalia hawezi ,na anakutafuta muda anaotaka yeye ila wewe unamtafuta kila mara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…