Ni mchallange vipi huyu mtoto maana akili yake imevuka mipaka ya elimu na hataki shule

Ni mchallange vipi huyu mtoto maana akili yake imevuka mipaka ya elimu na hataki shule

mr pipa

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2021
Posts
4,335
Reaction score
9,286
Ni mtoto wa miaka mi 5 kutotaka shule na ukimpeleka shule analia, na kusema siwezi kujifunza kitu hicho hicho kila siku

Nilileta uzi hapa Wadau wengi walinishauri na nikachukua ushauri wao nikaufanyia kazi
Nikambadilishia mazingira ya shule, akawa amesoma kama miezi 6, akaanza tabia ile ile kwamba hataki shule nikawa nimekaa na walimu wake kuhusu hili jambo

Wakanishauli nimuhamishe shule mpaka sasa kwenye darasa moja nimemuamisha shule tatu na bado mambo ni yale yale

Nikili kwamba huyu mtoto ana uwezo binafsi, tokea anazaliwa na yuko haraka kukariri vitu
Katika shule zote nilizompeleka, anashika nafasi ya pili au moja na walimu wanamkubali sana ni mtii

Kwa mfano ukiwa unachezea simu akawa jirani, then ukaiacha utakuta tayari ametoa patten, na kuanza kuichezea, kama ina bando atawasha data ataenda play store atapakua gem na kuanza kuzichezea

Na vingine vingi ambavyo hata sijawah kumfundisha, juzi nimepark gar nimemkuta amewasha na hapendi kucheza na watoto wenzake

Wakuu nipeni ushaur nn nifanye?
 
Kama fimbo kapigwa lakini nahisi haijawa suluhisho, ukimuelekeza ni rahisi kuelewa kuliko ukimkaripia

Ana uwezo wa kuchukua gazet au kitabu akakisoma kwa kutumia akili yake sio maelezo ya kwenye kitabu yaani kama anakisoma lakini kumbe anatunga maneno yake

Na anavyotulia kwenye hiko kitabu unaweza zania anakisoma, wakati uwezo wa kusoma hana
 
Me nikimpata huyo mbna shwari
Kwanza Nikwambie tu huyo ndo mtoto sasa... chakufanya nenda kawaonge walimu pesa ili wamruhusu awe anasoma siku 3 kwa wiki zile mbili mtafutie fani yeyote unayoona itamsaidia hata km ni uko veta we peleka ili kichwa kuanze kula vitu vikubwa na venye maana .... lasivyo akikosa vtu sahihi vya kujifunza bas hatajifunza hat visivo sahihi..
 
kwa umri alionao watamchukua huko veta?
 
watoto wa siku hizi
mwananngu kuna kitu alikua ananiambia
sikumuelewa nikamwambia unasemaaa? yaani kama nauliza aseme vizuri sikumuelewa
akasema "its beyond ur knowledge level..never mind"
akanyamaza
yaan tangu juzi namtafakari
 
Usipagawe na mtoto wa miaka mitano,Asome kwa lazma kwa sababu ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA.Angalau akifika darasa la saba anza kuwa naye karibu zaidi utapata faida kubwa ya matarajio yake.

Usiruhusu akutawale sana,hawezi kusema “siendi kwa sababu kila siku nafanya kitu hichohicho,hizo ni mbinu za yeye kukuongoza….be carefull.”
 
Mtoto wa umri gani huyu?.
😂😂😂😂
 
Yani walimu wameshindwa kushauri kitu cha kufanya zaidi ya kukwambia umuhamishe mtoto?
Walimu wanawajua watoto wetu zaidi ya tunavyowajua sisi. Shirikiana na walimu vizuri utapata ufumbuzi.
Mtoto wa miaka 5 si ndio yuko KG 2 au Std 1.
Hajui chochote huyu mtoto.
Ila ni Mtundu .

Ongea na Walimu vizur. Apende shule. Kama akifundishwa anaelewa haraka. Ili asikereke. Bas akielewa aambiwe aelekeze wenzake 😊😊😊.

Itamfanya awe na muda mwing wa kutumia hizo akili zake.
 
kama ni kweli ana higher iq vs the rest mbona suluhisho ni rahisi sana tu? wampandishe darasa kama yuko la 1 wampelekea la 2 wakiona bado halitoshi la 3 na kuendelea, lkn tanzania hard work and high iq are not rewarded kwa hiyo ni pagumu hapo.

jiulize kwa nini ((they)) wameua special schools zilizokuwepo? zamani kuna shule za watoto wenye vipaji maalumu na huko ndiko alikopaswa kwenda, zilikuwepo leo hii ((they)) wameua zote ...
 
Hii ni Tanzania sio Ulaya, Dogo inabidi asome Kwa lazima hiyo Elimu Yake ya msingi, akili akuzidi Hadi busara pia akuzidi!, haiwezekani kabisa.

Ingekuwa ni Ulaya huyo dogo angefanya vitu vizuri Tu baadae ila bongo hii hamna hiyo reward, so mfanye alazimike kwenda shule, shule TZ ndio Kila kitu, hakuna mfumo wowote ule rasmi utakaomkubali mwanao kama hakwenda shule....
 
Yani walimu wameshindwa kushauri kitu cha kufanya zaidi ya kukwambia umuhamishe mtoto?
Walimu wanawajua watoto wetu zaidi ya tunavyowajua sisi. Shirikiana na walimu vizuri utapata ufumbuzi.
labda hujakutana na watoto aina hiyo
 
Usipagawe na mtoto wa miaka mitano,Asome kwa lazma kwa sababu ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA.Angalau akifika darasa la saba anza kuwa naye karibu zaidi utapata faida kubwa ya matarajio yake.

Usiruhusu akutawale sana,hawezi kusema “siendi kwa sababu kila siku nafanya kitu hichohicho,hizo ni mbinu za yeye kukuongoza….be carefull.”
kwahiyo elimu ya kusomea historia ya tanzania na raisi wa kwanza ndio iko sahihi, umesema elimu ni ufunguo wa maisha? Kwamba wasio na elimu hawaishi, vipi aliebuni hiyo elimu alikuwa amesoma hadi darasa la ngapi? Au ndio mm mzazi ninaetaka aende shule ndie mpumbavu
 
Kuna uwezekano mwanao ana autism spectrum. Mi nashauri kama anaweza kusoma na kuandika, mfanyie home teaching halafu muengage kwenye mafunzo kwa vitendo. Kuna shule moja nimeiona Bagamoyo wanafundisha watoto skills mbali mbali kama za umeme, makenika, upishi, etc, huenda akawa interested huko. Pole mkuu, Mungu atakuvusha.​
 
Hii ni Tanzania sio Ulaya, Dogo inabidi asome Kwa lazima hiyo Elimu Yake ya msingi, akili akuzidi Hadi busara pia akuzidi!, haiwezekani kabisa.

Ingekuwa ni Ulaya huyo dogo angefanya vitu vizuri Tu baadae ila bongo hii hamna hiyo reward, so mfanye alazimike kwenda shule, shule TZ ndio Kila kitu, hakuna mfumo wowote ule rasmi utakaomkubali mwanao kama hakwenda shule....
kwakuwa baba hela ipo nimeunganisha michango yenu nimeamua nimpeleke next level namtafutia walimu atajifunza anachokitaka mambo ya kwenda kukaririshwa asije akawa jinga

Elimu yenyewe ya mchongo bado akomae nayo
 
Back
Top Bottom