Ni mchambuzi gani bora wa michezo Tanzania?

Soka la bongo

Ally Mayay Tembele

Jofrey Leah

Eddo Kumwembe

James Samweli

Gift Macha



ULAYA

Dr Leacky

Maestro

Eddo Kumwembe
hahahha umetisha , wachambuzi wanaona huu uzi ......watajipima
 
Wengi wanachanganya uchambuzi na ushabiki ndo maana at time mimi huwa napenda kumsikiliza kibonde akiwa anatangaza epl kwa kiswahili huwa natamani angelijikita kwenye uchambuziii tungeliongeaa mengine
 
Wachambuzi ambao kwa kiasi fulani wananivutia kuwasikiliza
1.Oscar Oscar
2.Geofrey Leah
3.Eddo Kumwembe
4.Ally Mayay
5.Gift Macha

Kuna wanaojiita wachambuzi kipindi cha U live Idd Salum na mwenzake Rashidi watumie muda huu kujifunza zaidi.Sijawahi kuona wachambuzi weupe kama hao.Yani huwa wanaongea kama wapo kijiweni hivi.Hawana facts wala sio wafuatiliaji wa kitu wanachojadili.Kwa upande wangu hawa mi wachambuzi wabovu ziadi kupata kutokea.

Kwa upande wa watangazaji wa mpira Paschal Kabombe unajitahidi sana lazima nikupongeze.Unajua sana kutangaza mpira kisasa mdogo wangu.Kwa sasa bongo you are the best.Wengi hawaendi na wakati wanatangaza koredioredio sana na kupenda kuwakopi akina Omary Jongo ambao kwa kipindi chao ni kweli walikuwa the best kwa mazingira yaliyokuwepo.Na hapa nimtolee Hassan Mvula.Anatangaza mpira wa tv anatujulisha watazamaji kimo au muonekano wa mchezaji.Anasema "Ni kijana mrefu mweusi huyu mtazamaji"!Kifupi hajui kufanya commentary.

Nurdin Suleman upo vizuri pia upande wa utangazaji wa mpira ukizingatia kuwa unaingia maeneo mengi na hujawahi niangusha.Nakupa big up!!
 
shida ya

dr leaky anakuwa anajikita sana katika kuelezea historia za virabu na wachezaji lakini pale katikati kwenye pitch technically si sanaa.

Mimi Dr Leakey namwelewa kwa sababu anaongea vitu ambavyo nakuwa sijavisoma au siwezi kuhangaika kuvitafuta vitu hivyo.

Hawa wengine wanaongea vitu ambavyo hata mimi naviongea. Ukisoma pre game previews za mitandao mikubwa then ukija kuwasikia Hawa unakuta wamepita nukta Kwa nukta.
 
Wote wanazama INTERNET wanatazama taarifa before kipindi,, then wanakuja kutudanganya sisi,,,mchambuzi bora ni BANDO LAKO LA INTERNET... mm huwa siwasikilizi hao,,,
 
Jeff Leah wa Azam yuko vizuri ana data za kutosha wengine wababaishaji tu.


Angekuwepo Dr. Leak yuko vizuri pia
 
Huyo ndiye mchambuzi bora basi kwa vigezo vya swali

Kwenye Basketball-NBA ni mweupe sana, kwenye mpira huwa namwelewa.

Anyway, sema tu ni vile watu hawazitafuti hizi taarifa, ila ukweli ni kwamba jamaa wanapita mahali ambapo hata wewe ukiamua kupita utawaelewa.

Mimi kumpa Leakey ni vile taarifa ambazo anazitoa, mfano historia, ground altitude, weather conditions za venue, travel distances kwa away teams, spectators influence (mfano Anfield washabiki wanakuwa ni full time kushangilia ambapo inaweza kuwapa home team competitive advantages), etc sina muda wa kuzitafuta na most of pundits na sports analysts hata wa Ulaya wanavisahau sana hivi vitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…