Umeuliza swali zuri sana mkuu 'pilipili-mbuzi'
Hao viongozi ndio hasa waliotakiwa kuzimia na kufa kabisa kwa sababu ndio wanufaika wakubwa.
Mtu kama yule aliyeokotwa Jalalani, na mwingine tena alisema kaokotwa wapi..., watu wa ajabu sana. Hawa ndio waliopaswa kufa kabisa!
Basi mkuu wangu, ujue kuna uigizaji mwingi sana, hata wa kufikia kufa kabisa. Ndiyo, mtu anaigiza, hadi anajikuta kapitiliza na kwenda kimoja.
Kadri ya kuwa na wajinga wengi nchini, ndiyo kadri ya waigizaji wa namna hiyo kuwa wengi.
Wewe kamwambie mtu mwenye uelewa mzuri, akaigize kuzimia kama hatakucheka kama sio kukuzaba vibao!
Huo mstari wako wa mwisho nilitaka kukuunga mkono kwenye maneno uliyoandika mwa sentensi hiyo. Mwanzo wa mstari huo, siyo kweli hata kidogo.
Mnyonge unampenda mtu aliyeshiba, sana sana anachokwambia ni maneno matupu!. Utashiba maneno?