Fortilo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 5,807
- 17,416
Kuna mambo yanaendelea nchini unajiiza hizi Habari kwanini zinatoka sasa bila maelezo?
Mawaziri viburi na majibu ya rejareja kwenye mambo mazito yanayohitaji utulivu wa akili.
Mambo haya yafuatayo yanamfanya Rais aonekane anatoa maelekezo kwa manufaa ya wachache wasio na uchungu na taifa hili hata kidogo.
Kitu ambacho ni uhakika pengine Rais lazima asisitiziwe na wasaidizi wake ni kwamba Tanzania ni nchi masikini na watu wake ni masikini mno.
Karibu asilimia 50% ya watanzania wote wanaishi chini ya USD 2 kwa siku.... hawa watu lazima maamuzi yeyote yawe yanawazingatia sana.
Habari zifuatazo zitamchafua sana Mh Rais kuelekea uchaguzi mkuu wa 2024/25.
1. Nyongeza ya karibu 40% ya Mishahara ya wabunge? Kulikuwa na haja gani kufanya jambo hilo sasa?
2. Kupanda bei za nishati ya mafuta na kuadimika bila maelezo yanayojitosheleza, awali ilisemekana ni kukosekana kwa $ sasa imegeuka imekuwa kupanda bei kwenye soko la dunia... bado shutuma hizi zinaelekezwa kwa teuzi za Mh Rais kwamba mume wa Spika anaesimamia EWURA wanakula njama na wafanyabiashara. (Rejea hotuba ya Mbunge Tabasam bungeni iliyozimwa na Spika?)
3. Kukatika umeme bila maelezo wala taarifa za kutosha nchi nzima.( Watu wanajiuliza Magufuli aliwezaje? Kalemani alifanyq kitu gani? Majibu hayatolewi.
4. Kuna mgao wa maji unaotarajiwa kuanzia wiki ijayo maeneo ya Dar, Arusha na Tabora....
5. Kuondoa Bima za Afya kwa watoto kwa kisingizio cha gharama, huku NHIF wakilipana posho na Mkopo binafsi na matumiz mabaya ya kias cha zaid ya 129B bila maelezo yakueleweka.(Report ya CAG)
6. Kuongezeka matamasha na warsha nchi nzima bila kutatua matatizo halis ya wananchi wa kipato cha chini.
7. Miradi ya kilimo isiyomnufaisha mkulima wa kijijini moja kwa moja.., kama BBT, Kumbuka kilimo ni maisha ya watu huko kijijini na sio agenda.
8. Kuongezeka maradufu kwa matumizi ya serikali bila kuongeza tija...hii ni pamoja na upanuzi wa Baraza la mawaziri pamoja na uwepo wa tume nyingi zinazozunguka bila matokeo ya utendaji wa tume hizo kuonekana kuleta mabadiliko kwa umma.
9. Kudumaa kwa demokrasia, kulinganisha na Mwaka mmoja wa utawala wako..., hisia zinatawala ukwel kuliko uhalisia, mfano... Katiba mpya nk.
10. Kaa la moto la DP world, na shutuma za Rushwa ambazo hazijajibiwa kwa ufasaha hadi leo.
11. Kuna hili la Cartels (madalali biashara) kuwepo kila kona ya mambo yanayohusu maslahi ya nchi moja kwamoja, ikiwemo mafuta, Gas nk.
Mtiririko wa haya mambo ni mrefu sana, lakini watendaji wako walikuwa na nafasi kutafuta ukwel na kuuweka hadharani au hata kwenye baadhi ya mikutano ya Chama kwa ajili ya ufafanuzi.
Namsikitikia Mh. Rais kwamba pengine wasaidizi wake aliowaamini hawamsaidii ipasavyo??