Ni mke wa mtu, ni mzuri, ANANITAKA nifanyeje?

Ni mke wa mtu, ni mzuri, ANANITAKA nifanyeje?

Mjomba, kumuacha inauma na hata mm ingeuma lakini je we mwenyewe toka moyoni mwako unadhani kumtosa au kumchukua kipi bora? Kipi kina hasara na kipi kina faida? Shinda kishawishi uncle, k2 ya kupita tu hiyo, jiheshimu nae atakuheshimu.
 
Simung`unyi maneno, wewe ni fuska, huna lo lote. Mchumba unaye,huyo wa nini? Tayari ni mke wa mtu na ana familia yake. Je mchumbako aakiliwa wewe utakuwa mvumilivu?

we mkulima acha kutoa mapovu. Unayajua mazinhira aliyo mleta mada? Si kila jambo kukurupuka mkuu kama ulivyokurupuka kujibu. Mpe mchakato wa kumuepuka huyu mwanamke na si kuanza kumshambulia.
 
ndg si kila king''aacho ni dhahabu, usijaribu,utakufa kabla ya wakati wako

unajuaje akama ana ukimwi au anataka kula fedha zako, angekuwa hajaolewa ningekushauri nn cha kufanya

kumbuka mke wa mtu sumu, wengine wlipofumaniwa, wamelawitiwa mbele ya watu na kuachwa na aibu ya milele

haya ww jifanye kidume mbegu, utaelewa ukishatendwa
 
nina umri wa miaka 30 single... tangu nimeachana na girlfriend wangu miaka mitatu iliyopita imekuwa ikiniwia vigumu kuconnect with a woman, so nimekuwa na marafiki wa kawaida, kati ya marafiki hao, ni huyu dada. Ni age mate, mwaka wa nane yuko kwenye ndoa na ana watoto wawili sasa, urafiki ulianza wa kawaida tu, mara nyingi amekuwa akiniomba ushauri kuhusu mambo mbalimbali na mimi bila hiyana nimekuwa nikimpatia ushauri huo.... miezi sita iliyo pita aliuguliwa na mtoto wake, mimi kama rafiki nilitoa msaada mwangu kulingana mazingira yaliyokuwepo kwa huruma tu rafiki yangu anauguliwa... baada ya mtoto kupona balaa ndipo lilipoanzia, kwanza alianza na shukrani za kilio kwa kudai nilichomfanyia hajawahi kufanyiwa na mtu yeyote... halafu akaanza kunipa historia ya maisha yake ya ndoa, kwanza alilazimishwa kuolewa, na huyo mume wake kila siku ni vipigo, na akadai kuwa huyo mume wake mtoto wake wa pili si wake kwa sababu eti alishaenda kwa daktari akamwambia kuwa hana uwezo wa kuzaa tena... na huyo dada anadai hajawahi kutoka nje ya ndoa.. kwa hiyo umekuwa ni ugomvi mtindo mmoja, si kwa mawifi hadi kwa mama mkwe wake....Nilichokifanya ni kumpa tu ushauri wa kukaa na mumewe wayazungumze wayamalize na ikiwezekana wakafanye DNA ili kuondoa utata...kilichonishangaza akaanza kunambia she is deeply in love with me.. na muda mrefu amesubiri labda nitasema kitu sisemi amejaribu kila njia kunionyesha ila mimi nikawa kipofu... nilipomwambia kuwa siko tayari si tu kwa kuwa yeye ni mke wa mtu pekee bali bado kuna ghost linani haunt siko ready kuwa kwenye mahusiano kwa sasa bado aliendelea kung'ang'ania.... ananijua vizuri kila uongo nilioutumia kumkwepa ilikuwa ni kazi bure...
Najisikia vibaya sio kwamba ni mlokole, ila pia si mfuasi wa shetani, ninge hit nikakimbia lakini kila likinijia wazo la kuwa huyu ni mke wa mtu nashindwa, kibaya zaidi anasema yuko tayari ku sacrifice everything hata ikibidi kuivunja hiyo ndoa kwa ajili yangu... hicho ndio kinaniogopesha zaidi, kwanza najifeel guilty kwa kuiweka mashakani ndoa ya mtu pili hata nikikubali ipo siku yatanikumba kama ya huyo jamaa...TAFADHALI NAOMBA USHAURI WENU.... kama utanitumia email nitashukuru zaidi ...... ngomz25@gmail.com..............THANX
 
Mke wa mtu? kimbia kabisa kama anakupenda basi akae mbali na wewe. ogopa sana mke wa mtu mkuu
 
Kama mtu huwezi kutoa maamuzi ambayo yapo ndani ya uwezo wako,basi wewe ni hatari!.
 
Hivi mtu ukiamua kumkwepa mtu kwa gharama yoyote ile utashindwa??haupo serious it seems na wewe unamtaka!
 
Mke wa mtu SUMU!!!!! Full Stop!


Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 
Back
Top Bottom