Ni mnyama au mdudu gani akiingia chumbani huwa unakosa amani?

Ni mnyama au mdudu gani akiingia chumbani huwa unakosa amani?

Nyoka mwezi wa tatu jua lilikuwa Kali nimerudi kwenye mihangaiko nataka kudeki naona uvivu nikaona nioge Kwanza nimetoka kuoga nasikia kitu kinagusa kavera nikajua mjusi kumbe nyoka tunatazamana nikapiga fimbo akarudi kwenye mfuko nikatoka nje nikaita jirani akaja na gongo kamuua sikulala nilimwaga mafuta ya taa mengi Kila mara namwaga mafuta
Pole
 
Naplan kwenda hospital kwasababu nahisi nina tatizo la akili. Wadudu wote wataambao nawaogopa kupita kiasi mfano mjusi hasa tule tudogo yaani nikimuona chumbani na akapotea nisimuone tena huwa siwezi kulala kwa namna yoyote ile humo ndani mpaka nihakikishe katoka nje. Naichukia hii hali ila huwa naogopa kuisema kwa watu kwasababu wengi hushangaa mwanaume mzima unagopa wadudu wadogo.
Jumapili kanisani nilikaa karibu na dirisha kulikuwa na kimjusi kile kidogo sikukiona na kikadondoka karibu yangu aisee niliruka watu wakabaki wanashangaa na nilipata fedheha sana maana si kitu cha kawaida mwanaume kuogopa hivyo vitu.
Nahisi nina tatizo mimi kwasababu nikiona hata chura mwili unasisimka vibaya sana na siwezi kupita hapo mpaka aondoke. Niliwahi kukaa kwa muda mrefu njiani nimeganda baada kuona chura wawili wako njiani nao ni kama walijua naogopa wakakaa hapohapo aisee ilikuwa ni fedheha nyingine maana nilisubiri mpaka mtu mwingine apite wale chura wakimbie ndo na mimi nipite
Naichukia sana hii hali na sometimes najipa ujasiri kwamba sitaogopa ila nikiona tu napata uoga uliokithiri sijui nimerogwa hata sielewi
phobia
 
Najuta kuandika hapa kuhusu kuogopa mjusi ( vile vidogo) hapa niko sebleni chumbani kuna kimjusi sijui hata nifanye nini. Wakuu hivi ukiua kile kimjusi kuna madhara yoyote? Please unaejua naomba msaada
 
Back
Top Bottom