Ni mnyama au mdudu gani akiingia chumbani huwa unakosa amani?

Ni mnyama au mdudu gani akiingia chumbani huwa unakosa amani?

Nyoka huwa sina shaka kutokana najua hawez tambaa kwenye malu mslu(Tiles) ila kuna kitu n'ge aisee aman kwishaa
Nyoka wanaingia mpk kwenye hizo tiles sema wanakua hawana kasi ya kutambaa maana wanateleza na kukosa balance
 
Nyoka wanaingia mpk kwenye hizo tiles sema wanakua hawana kasi ya kutambaa maana wanateleza na kukosa balance
Huko kukosa balance ndio nafuu yangu kuliko huyo N'ge niliyemtaja
 
Buibui aisee
Daah Umenikumbusha juzi kati niliua buibui mkubwa sana, sawa na kiganja cha mtoto wa miaka kumi.
Nilikuwa nimekaa kweny sofa mara akapita ukutani, aisee nilishtuka sana, sikulala hadi nilipomuua, maana nilijua nisipo muua leo kuna siku atanipandia wakati nimelala na situmiagi chandarua
 
Mimi hakuna mdudu ninayemuogopa ila wako baadhi ninaowachukia mfano maparata huwa siwapendi kwa kweli wengine ni mapanya,kunguni,mbu na konokono

Ila mijusi nawapenda sana kwa sababu ni harmless na wananisaidia kupunguza wadudu waharibifu!
Ki ujumla hakuna mnyama atakayeingia kwenye territory yangu muharibifu akapona
 
Naplan kwenda hospital kwasababu nahisi nina tatizo la akili. Wadudu wote wataambao nawaogopa kupita kiasi mfano mjusi hasa tule tudogo yaani nikimuona chumbani na akapotea nisimuone tena huwa siwezi kulala kwa namna yoyote ile humo ndani mpaka nihakikishe katoka nje. Naichukia hii hali ila huwa naogopa kuisema kwa watu kwasababu wengi hushangaa mwanaume mzima unagopa wadudu wadogo.
Jumapili kanisani nilikaa karibu na dirisha kulikuwa na kimjusi kile kidogo sikukiona na kikadondoka karibu yangu aisee niliruka watu wakabaki wanashangaa na nilipata fedheha sana maana si kitu cha kawaida mwanaume kuogopa hivyo vitu.
Nahisi nina tatizo mimi kwasababu nikiona hata chura mwili unasisimka vibaya sana na siwezi kupita hapo mpaka aondoke. Niliwahi kukaa kwa muda mrefu njiani nimeganda baada kuona chura wawili wako njiani nao ni kama walijua naogopa wakakaa hapohapo aisee ilikuwa ni fedheha nyingine maana nilisubiri mpaka mtu mwingine apite wale chura wakimbie ndo na mimi nipite
Naichukia sana hii hali na sometimes najipa ujasiri kwamba sitaogopa ila nikiona tu napata uoga uliokithiri sijui nimerogwa hata sielewi
Una entomophobia broo
 
Back
Top Bottom