Ni mradi upi ungerudisha mtaji wa uwekezaji kwa TPDC?

Mimi naweza kusema makampuni yote ya mafuta duniani yamejikita kwenye biashara ya utafutaji, uchimbaji, uzalishaji wa mafuta na gesi, usafishaji na utengenazi wa kemikali bila kusahau uuzaji.
Mfano mmoja tu nakupa
Kuna, kampuni inaitwa EXXONMOBIL hii kampuni inafanya hizo kazi zote
mfano mwingi ni British Petroleum (BP) inafanya hizo kazi zote.
Mifano ni mingi.

Kwa hiyo mimi sioni ubaya kwa TPDC kujitanua mkuu. Hilo swala lina faida nyingi sana. TPDC pale alipo anatakiwa kuwa na vyanzo imara vya mapato. Chanzo imara cha mapato ndio kama hizo biashara anazofungua ili akipata faida huko, anaweza kuitumia hiyo faida kwenye kuendeleza hizo shughuri za uendelezaji bila kutegemea mabeberu
 
TPDC inaendeswa Kama SACCOS ya Chama tawala,ikiacha Hilo itaendelea.
Kuna miradi Mimi naijuwa mitatu iwapo wangeifanya basi bajeti ya Tanzania 100 ingetokana na mapato ya mwaka ya TPDC.
 
1. Tatizo lipo wapi TPDC kushindwa kusambaza gesi kwenye bus za mwendo Kasi??
2. Nini Tatizo Mpaka leo TPDC Aina bomba la gesi kwenye mikoa ya Tanzania na pia Nchi jirani?? Kama TTCL inauza data Rwanda kwa Kuwa mkongo wa taifa umefika Rwanda why wao TPDC ata Chalinze awajafika??
3.TPDC wanakwama wapi ku JV na kufungua kiwanda ata Cha kuzalisha malighafi za chupa tu za plastic za maji???(Tanzania kwa mwaka wanatumia dola billions ngapi,ku order plastic pallets kwa viwanda vya maji??)Nchi zaidi ya tano(landlocked) malighafi za chupa za plastic zinapita bandari ya Dar es salaam🤣🤣🤣why TPDC isiwe ndo supplyer wa hii raw materials???
Niishie hapa kwa Sasa .ngoja nimalize supu kwanza
 
hapa tanzania mpaka yafanyike mapinduzi kwanza ndio utaona faida ya gesi asilia
 
Vipo viwanda vidogo ambavyo avizidi dola million 200. Vinaweza zalisha mitungi ya kutosha kutumia Kama Nchi then tuna expand.(Proposal nnayo) Penye Nia Pana njia......Tatizo TPDC imejaa ukiritimba na umangi meza....Nna jamaa zangu huu mwaka wa 3 .Wana pesa na Technology TPDC awajawajibu kitu chochote...wao wanataka kuinvest kwenye flare and stranded gases...ambazo almost ni waste kwao...awazitumii na Wala aziwaingizii faida ana kuja mtu anataka umuuzie uchafu unaozalisha unampiga Dana Dana😭😭.rushwa rushwa tu ndo wakupe deal..Kuna wachina hapo Dar Wana hela na Technology ya kufunga /kusamba gesi kwenye gari za petrol na Wana order/mikataba ya kuinstall kwenye gari zaidi ya 3000....TPDC mpaka kesho Wana just one has filling station Dar nzima😭😭😭Dereva awezi toa Taxi pale Airport kuja kujaza gesi Ubungo cause not economical..... So mchawi wa TPDC ni TPDC wenyewe..
 
Hii sio issue ya TPDC ni ishu ya selikali.

TPDS haiwezi kufungua kiwanda cha mbolea. Selikali inatakiwa ifungue, au itafute wawekezaje wafungue kiwanda cha mbolea nchini, then TPDC wauze gas kwa kiwanda.

Mfano mimi nafanya kiwanda cha saruji. Na tunatumia gas kuchoma ule udongo. TPDC wanatuuzia gas kwa unit.

Same applies katika products nyingine za gas. Selikali itafute wawekezaji wa viwanda mbalimbali ambao wata nunua ile gas.
 
Mkuu residentura,

Ahsante kwa kunikaribisha kwenye mjadala mujarabu kama huu!! Lakini kwa kuwa sikuwepo hapa jamvini kwa siku kadhaa kutokana na hili na lile, wacha ni-settle kwanza nitarudi!
 
Hii kitu nimekuwa nikiiwaza sana, lakini kufanyika haya inahitaji kiongozi mwenye nia nayo.
 
Ni sawa kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…