Ni msanii gani wa Kenya anakubalika sana Tanzania?

Poapoa mkuu. Hiyo lugha gongana aliimba Noorah.
Aaah, Baba Styles! Niliisikia zamani sana nikiwa shuleni ila naikumbuka sana, sijui ni lugha gani huwa anaitumia mwisho mwisho, inafanana sana na kinyarwanda.
 
Huu sio uzi wa ligi mzee baba! Mbona wakenya mna force ligi kila mahali?? Huu ni wetu sisi watanzania kuwaambia msanii au wasanii wenu tunaowakubali. Hii ndio platform itakayowawezesha kuwapima wasanii wenu. Hii ni kama free questionare ambayo haina gharama yotote!


Sasa nyie badala ya kukaa kando mkajua nani artist wenu anakubalika zaidi East Africa mnaanza kuleta ujuaji wenu!

Hebu jitahidini basi saa nyingine kujifanya wajinga ili mpate kitu!
 
Sasa unataka kusema tupige marufuku nyimbo zinazoimbwa kwa lugha za kikabila? Naelewa Tanzania yote mnazungumza kiswahili na nyimbo zote zinaimbwa kwa hii lugha. Je,hizo kabila za kichagga,kisukuma,na spinach zipo kweli ama ni majina tu?
Hizo nyimbo zinacheza katika vipindi maalumu vyenye lengo la kutambulisha makabila mbalimbali ya nchi, yaani redio station moja inacheza nyimbo na kutangaza mila za makabila yote kwa usawa, sio kila kabila kuwa na radio station yake.
 
Mtanzania Saida Karoli alikuwa anaimba nadhani ni kwa kihaya, na nyimbo zake zilisikizwa sana. Nandani kuna nyimbo moja ambayo Diamond ametumia line zake za kihaya. Ile ya chambua kama karanga. Waache unafik.
Ninyi wakenya acheni ubishi na ujuaji usiokua na sababu, Saida Karoli 90% ya nyimbo zake anaimba Kiswahili, ila anachanganya kidogo na kihaya, hiyo inakubalika, kama ambavyo wanamziki wengine wanavyochanganya Kiingereza.

Kwa Tanzania kwa sasa Ukabila sio tatizo, kwa hiyo hata ikitokea mtu akatumia lugha yake mwanzo hadi mwisho huwa haishitui sana, ila hatoruhusiwa kuimba nyimbo zote kwa lugha yake.

Tatizo ni ninyi wakenya ambao ukabila ni tatizo kubwa lakini mnaruhusu hata wagombea wanatumia lugha ya kabila lake katika mikutano ya kampeni za kura, ukifanya hivyo huku Tanzania automatically unafutwa katika orodha ya wagombea.
 
Hahaha! [emoji1] We jamaa ni mbishi kweli kweli.
 
Juma Nature na Nonini walifanya corabo kari sana enzi zile, Dar mpaka Moro ya kina Chege( je kuna uhisiano wa jina hilo na lile la Kikuyu?), Zali la Mentali proff Jay, Mikasi, Nakshi mrembo ya Ali kiba, mapoz nawe ya Mr.blue n pia ile za Siada karoli zilikuwa safi sana ukilinganisha na hizi za kina Diamond sijui nani nani Upuzi mtupu kila SAA ni mapenzi na ngono, hamna mawaidha ama la maana kujifunza hapo.
 
Points gani sasa, na chochote kile nitakachosema bado utabisha tu? [emoji23] Yataisha lini jombaa? Haya basi, jioni njema. 😎
Pingli nywee hivi ile kass TV yenu wanazungumzaga lugha gani?
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]we kweli mwehu waletwe wasanii wakimataifa sembuse artist wa kenya tena ambao bado local......

Unazungumzia pesa we kseli chizi[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Siri ya mafanikio ya mziki kwanza ni lazima kama taifa liwe na mtindo wake wa mziki yaani ID hiyo miziki mingine ya watu ni extra tu kuifanya nasikudandadanda na style za watu,,,,Nashukuru kwa hilo tumefanikiwa natunazidii fanikiwa

TAKE EXAMPLE
South Africa-kwaito
U.s.a-pop,rock, n.k
Indian-wanamziki wao
Nigeria-nao wamebuni ID yao
Tanzania-Bongo flavour

Kenya-?????????????????

Mtasubiri sana
 
Miziki yao ya kikabila tu
 
Miziki yao ya kikabila tu
Kama hujui haimaanishi haipo. Tangia enzi za E-Sir mtindo wa mziki wa kikenya, wa kizazi kipya, ulikuwa unaitwa Kapuka, na hadi sasa hivi watu kama Juakali, Nonini, Nameless bado wanatumia mtindo huo. Haufanani na bongo, ni wa kufoka sanasana kwasababu wakenya wanapenda sana hip hop na raga/reggae pia. Unajaribu kueneza chuki kwa sababu ya mziki tu jombaa?
 
Achana nao. Ni wabishi kupitiliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…