πππππππIla wasanii wa zamani kila mtu alikuwa na staili yake ya kipekee.
Kuna Crazy Gk,D knob,Kali P na yule mwingine jina nimemsahau aliimba nyimbo ya Nampenda bibi kikongwe hawa jamaa ilikuwa nikisikiliza nyimbo zao nilikuwa nacheka sana hadi nikawa addicted nazo bila ya kutarajia
Hii comment yangu nitakuwa sijaitendea haki bila kumuongezea marehemu Mr Ebo mmasai alikuwa na burudani sana nyimbo zake yaani alikuwa anaelimisha pamoja na kuchekesha/comedy.
Moja ya mistari yake ambayo nilikuwa nikiisikia navunja mbavu kwa kucheka ni hii hapa;
1. CHORUS
MOTIKA RECORDS
Acha kubishabisha kitu usichokijua eeh aah unalimbikiza ujinga eeh,uliza fafanua kama una swali uliza eeh aah,Mnatupakazia sana.
VERSE YA 1
Bado hujaona mbuzi anasukutua?Bado
Kunguru inanuka mdomo?Bado
Nyau imesukwa mabutu?Bado,eeh?bado
Nyoka imevaa hereni?Bado,eeh hata hii?Bado
Ajali ajali?Bado(hapa kwenye video yake ikaonesha ajali ya binadamu kwa binadamu kugonganaπ)
Na panya mwenye TB?Bado,hata hiyo?bado
Ng'ombe jike anarembua?Bado,wewe inakaa wapi?Bado
Self container ndani ni choo cha shimo?Bado,unatokea nchi gani?Bado
Na mkate imepakwa colgate?Bado,wewe ni kijana mudogo eeh?Bado
Na kaburi za kupangisha?Bado,nisamilie-bado.
Na kondoo mwenye mwanya?Bado,hata hiyo hujaona?Bado
CHORUS
VERSE YA 2
"Mnanisema vibaya kisa kusimamisha bus,na mahali ni porini ni bora nikawa wazi,bus ya kwanza kusimamisha kanipita kabisa,nikaona nikae rabarabani kabisa,gari ya pili ikaja ikafunga breki kali,dereva na abiria wote wakawa wakali.
Masai tungekugonga haya unakwenda wapi?
Masai:Aah mimi nilitaka kujua tu ni saa ngapi.
Wakaanza kunicheka wengine wamekarisika".
Na kuna mudogo wangu amevunjika muguu,tulikuwa tuko wote tunakwenda kwa sikukuu,tuko kwenye lori tunaimba tunaruka juu,eeh yule rafiki yangu si kapandisha mori,karuka juu zaidi kasahau yupo kwenye lori,alivyorudi chini kajikuta kwenye lami,ikawa bonge la soo na noma kilo kumi.
Bado hujaona samaki imepakwa wanja?Bado,nasema?Bado
Kinyonga ameshikwa na kwikwi?Bado
Mbwa anakohoa kapaliwa na kwikwi?Bado,alikuwa anabweka umbea-Bado
Kupewa makande kwenye ndege?Bado,hujasafiri na ndege eeh?Bado
Bus imefungwa injini ya pikipiki?Bado,Tanga na Arusha siku nne-Bado,wewe kila kitu ni bado?Bado,eeh?Bado
Hata kuzaliwa?Bado
CHORUS
VERSE YA 3
Hata mama ntilie muzungu bado hujaona?
Eeh Samahan babe sasa hivi tumemaliza chai,sasa hivi tumebakisha supu ya mkia na chapati,karibu sana(In European accent)
CHORUS
KIBWAGIZO
Na ndugu zangu wasambaa kwa nini majina yenu yote yanaanzia na She she she? Shehulosa,Shehasi,Shehemweri,Shelukosi,angalieni hata msije mkasema shetani ndugu yenu.
πππππππππππππππππππIlikuwa burudani sana yaani nilitaka kuandika mstari mmoja tu nikajikuta nimeandika nyimbo nzima kwa burudani iliyopo kwenye hii nyimbo.
Watoto waliozaliwa 2000 wamezikosa burudani hizi
πππππππIla wasanii wa zamani kila mtu alikuwa na staili yake ya kipekee.
Kuna Crazy Gk,D knob,Kali P na yule mwingine jina nimemsahau aliimba nyimbo ya Nampenda bibi kikongwe hawa jamaa ilikuwa nikisikiliza nyimbo zao nilikuwa nacheka sana hadi nikawa addicted nazo bila ya kutarajia