[emoji2]
Zuchu kawaacha mbali Sana wasanii wenzake kwenye upande wa uandishi mashairi...
Ukiachana na zile nyimbo za kupigia show (ambazo wewe unaziita za kipumbavu) kama siji, chapati na honey Zuchu amezidi kuonesha umahari kwenye kutunga mashairi yaliyotukuka...
Halafu inabidi ujue muziki Una angle nyingi sema wabongo wanataka mtu aimbe nyimbo zinazogusa Matatizo kama alizofanya Lady Jay Dee kwenye Ngoma kama Mawazo, siri, Ndindindi, yote mlosema na Joto hasira...
Lakini Kwenye angle ya mapenzi pia watu wanashauriwa na kuburidika... Mfano hiyo Ngoma ya nyumba ndogo kuna meseji nzuri tu Kwa wanawake jinsi Ndoa zao zinayumba Kwa kutokujali waume zao Hadi inapelekea kuzaliwa Kwa nyumba ndogo.... Rejea hii mistari
....Bwan'ako ana lalamika kila akija nyumbani
Eti hujui kupika
Kula kwako hatamani
Kwangu kalipenda tembele
Toto laini, laini
Shoga umenyimwa upole
Tajiri wa kisirani
Na samahani, samahani mwanzoni
Siku jitambulisha mimi nani
Ni miye njoo mke mwenzio A.K.A nyumba ndogo......
Hapo kawasihi Sana wanawake waache Kiburi na kisirani.... Sema nyie hua hamsikilizi content