Ni msanii gani wa muziki Bongo ambaye tangu uanze kumsikia hujawahi muelewa kabisa?

Ni msanii gani wa muziki Bongo ambaye tangu uanze kumsikia hujawahi muelewa kabisa?

Bora hata zawadi lakini zuchu huwa anaimba upumbavu tu hasa hiyo nyimbo ya nyumba ndogo na siji
[emoji2]
Zuchu kawaacha mbali Sana wasanii wenzake kwenye upande wa uandishi mashairi...

Ukiachana na zile nyimbo za kupigia show (ambazo wewe unaziita za kipumbavu) kama siji, chapati na honey Zuchu amezidi kuonesha umahari kwenye kutunga mashairi yaliyotukuka...

Halafu inabidi ujue muziki Una angle nyingi sema wabongo wanataka mtu aimbe nyimbo zinazogusa Matatizo kama alizofanya Lady Jay Dee kwenye Ngoma kama Mawazo, siri, Ndindindi, yote mlosema na Joto hasira...

Lakini Kwenye angle ya mapenzi pia watu wanashauriwa na kuburidika... Mfano hiyo Ngoma ya nyumba ndogo kuna meseji nzuri tu Kwa wanawake jinsi Ndoa zao zinayumba Kwa kutokujali waume zao Hadi inapelekea kuzaliwa Kwa nyumba ndogo.... Rejea hii mistari

....Bwan'ako ana lalamika kila akija nyumbani
Eti hujui kupika
Kula kwako hatamani
Kwangu kalipenda tembele
Toto laini, laini
Shoga umenyimwa upole
Tajiri wa kisirani
Na samahani, samahani mwanzoni
Siku jitambulisha mimi nani
Ni miye njoo mke mwenzio A.K.A nyumba ndogo......

Hapo kawasihi Sana wanawake waache Kiburi na kisirani.... Sema nyie hua hamsikilizi content
 
Mimi labda ninatatizo ila kiukweli AY sijawahi kumuelewa kabisa. Tangu nimeanza kumsikiliza wayback hajawahi kutoa ngoma nikaielewa kabisa. Labda ile Yuleee, nampenda sana jinsi alivyooo.... nayo kwa mbaali sana. Hata nikikutana nayo kwenye playlist ntaiskip tu.
AY pindi niko secondary niliikariri sana mistari yake na ya mwana FA. Nakbuka tulikuwa na utaratibu wa kushindana kuchana mistari, sisi wengine tulikuwa tunapenda ila vipaji hatuna ila kuna wenzetu wawili walikuwa na vipaji ile hatari na sasa ni wasanii wanaojulikana sana hapa nchini.

Nafikir kutokumkubali ni sababu hukufuatilia mziki wake, upande wangu wanaoimba sasa hiv wengi siwaelewi sababu siwafuatilii.
 
Hii ni 10 bora ya watu ambao hawakupaswa kujihusisha na muziki kwa sababu ya kukosa vipaji;
1. Jux
2. Shilole
3. Wakazi
4. Queen Darlin
5. Madee
6. AY
7. Babalevo
8. Ali Kiba
9. Tundaman
10. Best Naso.
Mtoe Ali Kiba na Jux hapo haraka
 
Shilole
Luludiva
Snura
Ibra wa harmonize
Shilole alipiga show huko Brussels, Ubelgiji na kuacha historia isiyoweza kufutika. Wazungu walishindwa kujizuia na kujikuta wanacheza miondoko ya Shishi baby. Baada ya hiyo show watu wenye roho mbaya na wivu walimfungia kujihusisha na muziki kwa mwaka mmoja.
shi2.jpg
 
Diamond huwa simuelewi na ninaamini nyote mnaompenda mmerogwa na kurogeka haswaa!
Huwezi kuniaminisha tofauti na hivyo
 
AY pindi niko secondary niliikariri sana mistari yake na ya mwana FA. Nakbuka tulikuwa na utaratibu wa kushindana kuchana mistari, sisi wengine tulikuwa tunapenda ila vipaji hatuna ila kuna wenzetu wawili walikuwa na vipaji ile hatari na sasa ni wasanii wanaojulikana sana hapa nchini.

Nafikir kutokumkubali ni sababu hukufuatilia mziki wake, upande wangu wanaoimba sasa hiv wengi siwaelewi sababu siwafuatilii.
Wasaanii karibu wote wanao imba saizi siwaelewi. Namaanisha karibu wote...
 
Dully syks nyimbo zake hazieleweki kabisa.yaani anaimba maneno mengine hata yeye hayajui.mfano Kuna wimbo siufahamu anaimba Njagara Njagara ooh ooh.
 
TID mnyama nakataa. Enzi zake tumeenjoy sana mziki wake.
Zeze
Girlfriend
Mtanzania pekee
Rahisa
Siamini... etc. Kati ya wasanii walokuwa hawakosei wakipiga ni TID.
Hapo kwenye siamini, bonge la ngoma la muda wote
 
Back
Top Bottom