Ni msiba! Mahakama imetekwa rasmi na Dola

Na Askofu Kalikawe Bagonza:

UJINGA WANGU SASA UMEKOMAA

Niliamini UHAINI ni kosa kubwa. Neno lenyewe tu, linaogopesha kulisoma, kuliandika na kulitamka. Ni kitendo cha kutaka au kupindua serikali yoyote (halali au haramu).

Sasa kuna mtu mmoja katuhumiwa kutaka kutufanyia hayo. Huyu atakuwa ni mtu mbaya sana. Kwa nini atuhumiwe yeye kwa kosa hili baya? Nikawaza;

1. Kesi yake ingesikilizwa wazi (uwanja wa Taifa maana Kisutu hapatoshi).

2. Pale uwanjani wangeweka vipaza sauti na televisheni zote zirushe mubashara ili watu wote waone.

3. Makarandinga ya polisi yangesomba wote wasio na nauli kwenda kusikiliza kesi.

4. Asasi za kiraia na kianaharakati wangetoa maji ya kunywa bure kwa waliofika kusikiliza.

5. Posho za watumishi wa mahakama zingeongezwa ili kuwatia moyo wakati wa usikilizaji.

6. Siku ya hukumu ingekuwa siku ya mapumziko ili nchi itulie na kusikiliza hukumu hiyo.

Kwa nini nafikiri hivi?

a) Ingetoa fundisho la wazi kwa watu wote wanaopenda kuchezea amani ya nchi yetu.

b) Elimu ya uraia na utii wa sheria bila shuruti ingetolewa kwa vitendo kupitia kesi hii.

c) Hatua hii ingehamasisha watu wengi zaidi kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu bila kuhofia Polisi kuvuruga uchaguzi huo.

d) Wale wenye “mdomomdomo” kama mimi, wanaopenda kutumia neno HAKI kuliko amani, wangekuwa wamefungwa goli la kisigino na timu AMANI isiyopenda kutamka neno haki.

e) Hatua hii, ingeua kabisa kampeini za za NO REFORMS, NO ELECTION kwa sababu utawala wa sheria ungeonekana wazi.

f) Chama kingepata fursa nzuri ya kuonyesha ushahidi jinsi mabeberu wanapandikiza wahaini katika siasa zetu.

SASA, nimegundua ujinga wangu umekomaa. Kumbe kesi hii ni muhimu na nyeti. Haiwezi kuwa wazi. Ni kwa ajili ya wanasheria na wateule wachache wenye vifurushi kwenye simu.

Nilidhani nchi hii ni yetu wote kumbe ya wana sheria tu na polisi. Hata serikali iliyotaka “kupinduliwa” ni yetu au ya wana sheria na polisi?

Kama ni yetu wananchi, kwa nini hairuhusiwi watu kwenda mahakamani kusikiliza?

Aisee ujinga wangu una gharama. Akili zimeisha kichwani. Nimebakiza za kunipeleka msalani.

Wajinga wengine kama mimi wameenda wakaishia kuvunjwa viuno, mikono, na migongo.

Hili giza la kuona haki ikitendeka haliwezi kutuacha salama.

Nawaombea uponyaji walioumizwa.
Nawaombea waliowaumiza ili wao wasiumizwe maishani maana inauma.

Vitendo hivi vimelaaniwa vya kutosha. Nafasi za kulaani zimejaa. Nitalaani kesho.
 
Moja ya sifa kuu ya Majaji Wakuu Watatu (Wazawa) wa Kwanza wa Mahakama ya Tanzania yaani Jaji Francis Nyalali, Jaji Bararbas Samata na Jaji Augustino Ramadhani ni kwamba, pamoja na kuiheshimu sana Serikali ila walisisitiza sana Serikali kuheshimu Uhuru wa Mahakama.

Majaji hawa walitengeneza Mhimili ambao sio tu Serikali waliuheshimu bali kutowaza hata kuuingilia...

Katika kipindi cha Majaji Wakuu hawa Majaji na Mahakimu walitoa hukumu dhidi ya Serikali na matakwa ya Serikali na vyombo vyake kwa kuzingatia misingi ya haki iliyopo Kikatiba.

Katika Kipindi cha Majaji Wakuu hawa, Sheria ya kuwaweka watu kizuizini ilitamkwa na Mahakama kuwa kinyume na Katiba hadi kupelekea Serikali kusitisha taratibu za kuwaweka watu vizuizini chini ya Sheria ile.

Katika kipindi cha Majaji Wakuu hawa, Mahakama ilisema Mgombea binafsi ni haki ya Kikatiba

Katika kipindi cha Majaji Wakuu hawa, haki za binadamu zilikuwa zinawekewa misingi ya kimahakama hadi kufanya Serikali iepuke kuzivunja sio tu kwa kificho bali hata waziwazi.

Kipindi cha Majaji Wakuu hawa, ilikuwa ikitokea umemuona Jaji Mkuu kwenye shughuli za Serikali ilikuwa labda iwe uapisho wa Rais au kuzinduliwa kwa Bunge. Majaji na Mahakimu waliheshimika kweli.

Tangu alipoingia Jaji Othman Chande na sasa Jaji Prof. Ibrahim Juma, tumeanza kuona Mhimili wa Mahakama ukiwa sehemu ya Serikali, ukimezwa na kutekwa kabisa na dola ya Serikali.

Maamuzi madogo yaliyotolewa na Mahakama ya Kisutu leo hii ya kumnyima Tundu Lissu haki yake ya kikatiba ya kuja Mahakamani kuonana na Mawakili wake na Kusikilizwa kwa namna anavyotaka yeye kama Mtuhumiwa ni kielelezo tosha kuwa Mhimili wa Mahakama umejifia baada ya kutekwa rasmi na dola

Kitendo cha Jeshi la Magereza kumuhamisha Tundu Lissu gereza bila amri na maelekezo ya Mahakama tu kilipaswa kutolewa kalipio kubwa sana na Mahakama. Hii ni kwa sababu endapo Tundu Lissu akifa au lolote likimpata Wachunguzi watakachochunguza cha kwanza watakachoanza nacho ni kama kulikuwa na Maelekezo ya Mahakama kumuhamisha Gereza.

Kitendo cha kutomleta Mahakamani Tundu Lissu na kumkatalia kuonana na Mawakili wake, kilipaswa pia kukaripiwa sana na Mahakama kwa sababu kwa mujibu wa Katiba yetu ambayo ndo Sheria mama na Kuu, Mtuhumiwa anapaswa kusikilizwa, kupata haki za kuwakilishwa ikiwemo kuonana na Wakili wake pamoja na kutotendewa kama ameshatiwa hatiani.

Kama Wakili Mkongwe, nimesikitika sana kwa hali hii ilipofikia Mahakama. Na hapa sijazungumzia vitendo vya Kwaya ya Mahakama kubeba picha ya Rais na kuimba nyimbo za kumsifia Rais. Sijazungumzia vitendo vya Wabunge 19 wa Chadema waliovuliwa ubunge na Chama Chao kuendelea kuwa Bungeni huku wakila kodi za Wananchi pamoja na Mahakama kusema hawastahili kuwa Wabunge.

Kwa hali hii tuliyofikia ya Mahakama kumezwa na dola sioni tumaini lolote lile kwa Wananchi wa Tanzania zaidi ya Mapinduzi ya Kijeshi.

Profesa Juma na Jaji Chande. Mtalaaniwa Milele kwa kuifikisha hapa Mahakama.
Kama chadema ilivyotekwa na Mariah sarungi..
 
Ulikuwa hujui. Mahakama inapogeuka chaka la chawa jua hakuna haki hata kidogo.
 
Siku nyingine mtajifunza kuwa ni kosa kubwa sana kumpa uongozi mkubwa mwanamke, wanawake hawajawahi kubadilika tabia zao za asili
Umeshamsahau Magufuli? Hao vibaraka walikimbia nchi huyo unayemsema vibaya ndiyo kawarudisha. Au kwa kuwa ninyi ni nyumbu mlitegemea Rais akiwa mwanamke ni wa kumchezea, hana mamlaka kamili? Huyo ni Mkuu wa nchi, Amiri jeshi mkuu madaraka yake ni yale yale, vyombo vya dola ni vile vile, ameapa kuilinda nchi hii, mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Halafu Rais haingilii kazi za kila siku ya vyombo vya usalama. Rais wetu yuko imara hamtafanikiwa kufanya upuuzi wenu huo mlioupanga.
 
Kuna siku isiyo na jina wananchi watawaua sana polisi, wanajeshi na viongozi wengi wa serikali.
 
2 TIMOTHEO 2:19​

"Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu"
Sisiem hawawezi kukuelewa, laana imeshapenya ndani yao kiasi kwamba hawawezi kupokea maonyo tena kama farao
 
2 TIMOTHEO 2:19​

"Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu"
mama D acha kulihusisha neno la Mungu na haya matendo yanayofanywa na hawa watawala wenu wenye roho za kishetani.
 
Ulikuwa hujui. Mahakama inapogeuka chaka la chawa jua hakuna haki hata kidogo.
Walianza kuuharibu Usalama wa Taifa, Wakaja Jeshi la Wananchi sasa Mahakama.

Nguzo zote ambazo ndizo kimbilio la Wananchi wanyonge wameziharibu. Kwa hali hii huu ni msiba mkubwa sana kwa Wananchi wa Tanzania.

Pona yetu Watanzania kwa sasa ni kujitokeza Mwanajeshi mwenye akili na moyo kama wa Traore wa Burkina Faso ili atukomboe.
 
Moja ya sifa kuu ya Majaji Wakuu Watatu (Wazawa) wa Kwanza wa Mahakama ya Tanzania yaani Jaji Francis Nyalali, Jaji Bararbas Samata na Jaji Augustino Ramadhani ni kwamba, pamoja na kuiheshimu sana Serikali ila walisisitiza sana Serikali kuheshimu Uhuru wa Mahakama.

Majaji hawa walitengeneza Mhimili ambao sio tu Serikali waliuheshimu bali kutowaza hata kuuingilia...

Katika kipindi cha Majaji Wakuu hawa Majaji na Mahakimu walitoa hukumu dhidi ya Serikali na matakwa ya Serikali na vyombo vyake kwa kuzingatia misingi ya haki iliyopo Kikatiba.

Katika Kipindi cha Majaji Wakuu hawa, Sheria ya kuwaweka watu kizuizini ilitamkwa na Mahakama kuwa kinyume na Katiba hadi kupelekea Serikali kusitisha taratibu za kuwaweka watu vizuizini chini ya Sheria ile.

Katika kipindi cha Majaji Wakuu hawa, Mahakama ilisema Mgombea binafsi ni haki ya Kikatiba

Katika kipindi cha Majaji Wakuu hawa, haki za binadamu zilikuwa zinawekewa misingi ya kimahakama hadi kufanya Serikali iepuke kuzivunja sio tu kwa kificho bali hata waziwazi.

Kipindi cha Majaji Wakuu hawa, ilikuwa ikitokea umemuona Jaji Mkuu kwenye shughuli za Serikali ilikuwa labda iwe uapisho wa Rais au kuzinduliwa kwa Bunge. Majaji na Mahakimu waliheshimika kweli.

Tangu alipoingia Jaji Othman Chande na sasa Jaji Prof. Ibrahim Juma, tumeanza kuona Mhimili wa Mahakama ukiwa sehemu ya Serikali, ukimezwa na kutekwa kabisa na dola ya Serikali.

Maamuzi madogo yaliyotolewa na Mahakama ya Kisutu leo hii ya kumnyima Tundu Lissu haki yake ya kikatiba ya kuja Mahakamani kuonana na Mawakili wake na Kusikilizwa kwa namna anavyotaka yeye kama Mtuhumiwa ni kielelezo tosha kuwa Mhimili wa Mahakama umejifia baada ya kutekwa rasmi na dola ya Serikali.

Kitendo cha Jeshi la Magereza kumuhamisha Tundu Lissu gereza bila amri na maelekezo ya Mahakama tu kilipaswa kutolewa kalipio kubwa sana na Mahakama. Hii ni kwa sababu endapo Tundu Lissu akifa au lolote likimpata Wachunguzi watakachochunguza cha kwanza watakachoanza nacho ni kama kulikuwa na Maelekezo ya Mahakama kumuhamisha Gereza.

Kitendo cha kutomleta Mahakamani Tundu Lissu na kumkatalia kuonana na Mawakili wake, kilipaswa pia kukaripiwa sana na Mahakama kwa sababu kwa mujibu wa Katiba yetu ambayo ndo Sheria mama na Kuu, Mtuhumiwa anapaswa kusikilizwa, kupata haki za kuwakilishwa ikiwemo kuonana na Wakili wake pamoja na kutotendewa kama ameshatiwa hatiani.

Kama Wakili Mkongwe, nimesikitika sana kwa hali hii ilipofikia Mahakama. Na hapa sijazungumzia vitendo vya Kwaya ya Mahakama kubeba picha ya Rais na kuimba nyimbo za kumsifia Rais. Sijazungumzia vitendo vya Wabunge 19 wa Chadema waliovuliwa ubunge na Chama Chao kuendelea kuwa Bungeni huku wakila kodi za Wananchi pamoja na Mahakama kusema hawastahili kuwa Wabunge.

Kwa hali hii tuliyofikia ya Mahakama kumezwa na dola sioni tumaini lolote lile kwa Wananchi wa Tanzania zaidi ya Mapinduzi ya Kijeshi.

Profesa Juma na Jaji Chande. Mtalaaniwa Milele kwa kuifikisha hapa Mahakama.
MIMI NATAMANI JESHI LICHUKUE NCHI
 
Back
Top Bottom