"Ni msiba mzito. Ametutoka, ametuachia pengo kubwa. R.I.P"

"Ni msiba mzito. Ametutoka, ametuachia pengo kubwa. R.I.P"

"Ni msiba mzito, ametutoka jamani, ametuachia pengo kubwa! Ooh, tumempoteza. Ni vigumu kueleza machungu tuliyo nayo mioyoni. Tutaendelea kumkumbuka daima. Pumzika kwa amani(R.I.P.)"

Kila dakika, kuna watu wanafariki huku na kule duniani. Maneno kama hayo husemwa na wafiwa. Ni vizuri kuelewa kuwa maneno yetu: "Pumzika kwa amani(RIP), au Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi" hayawezi kubadilisha hatima ya mtu aliyekufa katika dhambi. Kama mtu amekufa akiwa jambazi, mwizi, mzinzi, mnafiki au muongo bila kutubu, basi hakuna maombi wala matamko ya heri yatakayomwokoa.

Roho ya mtu aliyefia dhambini hailali—bali inalia, inaomboleza na kuteseka.

Bwana Yesu mwenyewe alitufundisha hivyo kupitia kisa cha tajiri na Lazaro (Luka 16:19–31). Tajiri aliishi kwa anasa na dhambi, kisha akafa katika hali hiyo. Alizikwa kwa heshima, lakini Biblia inasema, “alipoinua macho yake kule kuzimu akiwa katika mateso, alimwona Lazaro mbali akiwa kifuani mwa Ibrahimu.” Tajiri hakuwa na usingizi wala amani —bali maumivu mazito.

Hili ni onyo kwa wote: kifo hakibadilishi tabia ya mtu wala hali yake ya kiroho. Mtu anapokufa, anavuna kile alichopanda akiwa hai. Maombi yetu hayawezi kumtoa mtu kutoka kuzimu hadi peponi. Never!
Gal 6:7-9

"Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele."
May God give us rest when we die
 
Ninasali Kila siku asubuhi na kabla ya kulala, ninafunga kwa maombi, biblia yote ipo kichwani ila situmii vifungu vya biblia nawaelewesha watu kile nimelewa kwa sababu sio wote wanasoma biblia ila ukiwaelewesha wanaelewa
Kongole
 
Back
Top Bottom