Ni msomi yupi mwenye sifa hizi na bado yuko mtaani hana ajira?

Ni msomi yupi mwenye sifa hizi na bado yuko mtaani hana ajira?

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,042
Reaction score
17,320
Darasa la saba ulipata wastani wa "A" na ukakosa fursa ya kwenda kidato cha kwanza? Kidato cha nne ulipata Division ONE na hukuchaguliwa kwenda Alevel au vyuo (kama ulichagua vyuo)? Alevel ulipata Division ONE ukakosa fursa ya kwenda Chuo Kikuu? Chuo Kikuu ukapata GPA ya "First Class" au "Upper Second" alafu ukakosa ajira?

Wengi wanaolialia wamesoma wakakosa ajira ni wale vilaza na wanaolazimisha ufauru afifu kuwa wamefauru! Katika Dunia hii ya utandawazi ili utoboe unahitaji viwango vya juu vya kudhihirisha kuwa uko vizuri! Sio unajikusanya na Division two au GPA ya lower au Gentleman alafu unalialia sina ajira! Hizo enzi zimepita mkuu! Ukiona umetupwa nje na mfumo wa ajira jiongeze kivingine!

Nashangaaga kuona mtaani vijana eti wanahusstle kwa kuendesha bodaboda, kupika mandazi, vitumbua, samaki, miogo alafu wanategenea kutoboa kuwa na maisha safi ya kumiliki nyumba nzuri, gari zuri, majina na heshima nzuri ya ukwasi! Thubutu! Utapata ela ya kula lakini umasikini umeishatia timu!

Povu ruksa!
 
Unaweza ukawa na hiyo first class lakini usifanikiwe kupata ajira.

Kwa Ulimwengu wa sasa wenye wahitimu wengi wa Vyuo Vikuu, muhimu uwe na connection pamoja na bahati tu
Kuna watu mpaka Sasa Bado hawajajua uhalisia kama mtoa mada, unatangaza nafasi ajira ya watu 50 wanaomba 1500 hapo hizo first na upper second ni zaidi ya 400 na hiyo ndio trend kwa sasa kwa tangazo la ajira
 
Kuajiriwa ni kujifungia mkuu ,kitaa kuna pesa nyingi sana zinarandaranda tu, kuziongeza ziwe nyingi ni juhudi zako tu na sio mpaka maamuzi ya wengine.
Mimi mwenyewe sikuwahi kuajiriwa kwasababu sikutaka japo sifa nilikuwa nazo! Shida ninayoiona ni vijana kulialia ajira ili hali ni ma failures!
 
Kuna watu mpaka Sasa Bado hawajajua uhalisia kama mtoa mada, unatangaza nafasi ajira ya watu 50 wanaomba 1500 hapo hizo first na upper second ni zaidi ya 400 na hiyo ndio trend kwa sasa kwa tangazo la ajira
Jamaa hajui tu kwamba Kuna watu Wana miaka almost 8 tangu ahitimu akiwa na hiyo first class yake ila Hana ajira

Kuna wengine Wana pass tu lakini wameajiriwa 🙌
 
Kuna watu mpaka Sasa Bado hawajajua uhalisia kama mtoa mada, unatangaza nafasi ajira ya watu 50 wanaomba 1500 hapo hizo first na upper second ni zaidi ya 400 na hiyo ndio trend kwa sasa kwa tangazo la ajira
First Class GPA 4.2 up to 5.0 aje!
 
kuna mwamba alitoka chuo na gentleman, anakula usd 12k+ take home saudia huko, alipata kazi kisa tu ni muslim, kwenye interview aliokuwa nao wakiristo wa4 wa chini kabisa alikuwa na upper second, mwamba pekee ndo alikuwa na gentlemen na akanyaka ajira. usikariri mambo mkuu hii dunia ni duara sio tambarare, thngs does turn 180 degrees sometimes
 
Ma failures ndo yamejaa mtaani alafu domo lefu wanataka ajira! Akuajiri nani? Unadhani tuko zile enzi za mwalimu miaka 47? Tena hata hizo GPA ziangalie kama ni masomo yanayoendana na soko! Sio una GPA kali ya Socialogy alafu unakuja kututambia! Huu ni ulimwengu wa sayansi na technologia! Kama uwezi kumudu masomo ya sayansi wewe ishia tu kidato cha nne alafu nenda chuo cha kusomea ufundi upate cheti njoo kitaa pambana! Utapoteza muda kuendelea na masomo hayo ya Art au endelea lakini uwe na ubavu wa ushindani! Hatutaki jamii inayolialia kila kukicha utadhani jamii au serikali ndo iliyowazaa!
 
Back
Top Bottom