Ni Muda Muafaka Kwa Serikali Kuipa Kipaumbele Barabara Ya Mpiji Magoe

Ni Muda Muafaka Kwa Serikali Kuipa Kipaumbele Barabara Ya Mpiji Magoe

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Baada ya agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Albert Chalamila, kutaka mabasi yote ya mkoa kuanzia na kumalizia safari zao katika Magufuli Bus Terminal, nadhani sasa ni muda muafaka kwa serikali kuangalia pia upande wa miundombinu ili agizo hilo liende sambamba na kurahisisha usafiri kwa wananchi. Si bus terminal pekee inayopaswa kupewa kipaumbele, bali pia barabara zinazounganisha terminal hiyo na maeneo mbalimbali ya jiji na mikoa jirani.

Moja ya barabara inayostahili kupewa kipaumbele ni barabara ya Mpiji Magoe, kutoka Mbezi Magufuli Bus Terminal hadi Bunju B, yenye urefu wa takribani kilomita 25. Ikitengenezwa kwa kiwango cha lami, barabara hii inaweza kuwa na mchango mkubwa sana katika kupunguza muda wa safari na msongamano kwenye baadhi ya barabara za Dar es Salaam.

Kwa sasa, magari na mabasi yanayokwenda upande wa Kaskazini, hususani Tanga, Moshi na Arusha, yanapotoka Magufuli Terminal hulazimika kufanya mzunguko mrefu kupitia Goba, njia nne, Madale hadi Tegeta ndipo yakutane na Bagamoyo Road. Hii inaongeza muda wa safari, matumizi ya mafuta na wakati mwingine kuchangia msongamano kwenye njia hizo.

Lakini kama barabara ya Mpiji Magoe ikijengwa kwa kiwango cha lami, magari hayo yataweza kutoka Magufuli Terminal, kupita moja kwa moja kuelekea Bunju B na kuendelea na safari zake za kuelekea Kaskazini bila kulazimika kufanya huo mzunguko mrefu. Kwa kifupi, hii ni njia ambayo inaweza kuokoa muda na kurahisisha sana usafiri.

Na si wasafiri wa Tanga, Moshi na Arusha pekee watakaonufaika. Wakazi wa Mpiji, Magoe, Bunju na maeneo mengine yanayozunguka barabara hiyo pia watapata manufaa makubwa kupitia usafiri rahisi, kuongezeka kwa shughuli za biashara, kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na hata kuongeza thamani ya maeneo hayo.

Kwa hiyo, kama serikali inalenga kuifanya Magufuli Bus Terminal kuwa kituo kikuu cha mabasi ya mkoa wa Dar es Salaam, basi ujenzi wa barabara ya Mpiji Magoe kwa kiwango cha lami unapaswa kupewa kipaumbele. Ni miundombinu ambayo haitanufaisha wasafiri pekee, bali inaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuboresha usafiri na maendeleo ya maeneo yote yanayounganishwa na barabara hiyo.
 
Na ina umbali mfupi zaidi kushinda ile ya Goba.

Screenshot_20260820_132145_Maps.jpg
 
Naunga mkono hoja ile barabara wameweka changarawe sijui matope na pale kanisani kuna karavate haliishi wanalijenga muda.
Nashangaa imechukua mda mrefu sana, na wananchi wa kule wanapata shida hasa kipindi cha mvua
 
Kweli kuna vumbi sana aseeh barabara mbovu sana
 
Kweli kuna vumbi sana aseeh barabara mbovu sana
Watu wa kule wanapata tabu sana, ukienda pale mbezi kituo cha daladala, jioni utawakuta wamepanga mstari wanasubiria usafiri....yani wanatia huruma sana
 
Back
Top Bottom