Ni muda muafaka sasa TRA mtoke hadharani mtuambie hayo mabango yenye picha ya Rais nchi nzima nani anayalipia na yanaingiza kiasi gani

Mr mutuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2023
Posts
2,869
Reaction score
14,501
Nilikua nadhani ni kwenye majiji makubwa tu ila tuwe wakweli picha ya rais Samia ipo kwenye mabango karibu nchi nzima tena sehemu karibu zote potential kibiashara

Kuna mahali nilikua na kakibanda tena ndanindani sio hata main road, njia Haina hata lami walikuja TRA wakanipigia hesabu laki 3 kwa mwaka tukashindwana ikabidi nilitoe lile bango, sasa TRA mje mtueleze hayo mabango nchi nzima nani analipia kama ni chama, serikali, au watu binafsi na yanaingiza pesa kiasi Gani?
 
Kodi za wanachi zinafanya kazi.
 
Ni suala la muda tu ipo siku CCM itaondoka madarakani. Kuna kizazi kile cha kupokea vitenge vyenye sura ya mama kikiishia tukabaki vijana na elimu ikifika vzuri mpaka vijijini, CCM ataondoka tu tena kwa aibu kubwa
 
Watanzania tushakua kama makondoo, mtu nauliza swali basic tu mtu anajibu uchochezi, tumerudi enzi za utumwa sasa huku tukitawaliwa na weusi wenzetu
 
Mama katundikwa kwenye mabango nchi nzima kama kapotea na anatafutwa na Wanakizimkazi wenzake!🀣🀣🀣
 
nadhani yeyote yule yuko huru kuweka mabango popote nchini ikiwa anaona inafaa, na ikiwa atapata idhini ya mamlaka husika kwenye eneo husika....

hakuna bango maalumu popote nchi , lisilolipiwa wala eti halina idhini ya mamlaka husika, labda yale ya waganga wa jadi ya kurudisha mpenz aliepotea πŸ’
 
Majibu yatakuwa rahisi tu. Wanaolipia ni Wajomba Zake waliopewa bandari zote nchi hii kwa miaka 100, na kupiga marufuku uendelezaji wa bandari sehemu yoyote nchi hii bila ya ruhusa kutoka kwao
 
Kwani nyie ni wageni wa hayo mabango,mbona aliyepita naye
Alijaza mabango nchi nzima
Lakini hamkuhoji πŸ˜„

Ova
Hata kwa mwendazake mambo ambayo tulikua hatuelewi tulihoji pia, ni Haki yetu kupata majibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…