Ni muda muafaka sasa TRA mtoke hadharani mtuambie hayo mabango yenye picha ya Rais nchi nzima nani anayalipia na yanaingiza kiasi gani

Ni muda muafaka sasa TRA mtoke hadharani mtuambie hayo mabango yenye picha ya Rais nchi nzima nani anayalipia na yanaingiza kiasi gani

Mr mutuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2023
Posts
2,869
Reaction score
14,501
Nilikua nadhani ni kwenye majiji makubwa tu ila tuwe wakweli picha ya rais Samia ipo kwenye mabango karibu nchi nzima tena sehemu karibu zote potential kibiashara

Kuna mahali nilikua na kakibanda tena ndanindani sio hata main road, njia Haina hata lami walikuja TRA wakanipigia hesabu laki 3 kwa mwaka tukashindwana ikabidi nilitoe lile bango, sasa TRA mje mtueleze hayo mabango nchi nzima nani analipia kama ni chama, serikali, au watu binafsi na yanaingiza pesa kiasi Gani?
 
Nilikua nadhani ni kwenye majiji makubwa tu ila tuwe wakweli picha ya rais Samia ipo kwenye mabango karibu nchi nzima tena sehemu karibu zote potential kibiashara

Kuna mahali nilikua na kakibanda tena ndanindani sio hata main road, njia Haina hata lami walikuja TRA wakanipigia hesabu laki 3 kwa mwaka tukashindwana ikabidi nilitoe lile bango, sasa TRA mje mtueleze hayo mabango nchi nzima nani analipia kama ni chama,serikali, au watu binafsi na yanaingiza pesa kiasi Gani?
Kodi za wanachi zinafanya kazi.
 
Uchochezi Kwa maana gani? Kwamba kuuliza hayo mabango nani anayalipia na yanarudisha vipi pesa? Maana tunafahamu mtu akiweka bango la biashara ili kufikia wateja wengi na hivyo ndivyo pesa hurudi

Haya yale mabango yanauza nini pale na pesa zinatoka wapi?
Watanzania tushakua kama makondoo, mtu nauliza swali basic tu mtu anajibu uchochezi, tumerudi enzi za utumwa sasa huku tukitawaliwa na weusi wenzetu
 
Mama katundikwa kwenye mabango nchi nzima kama kapotea na anatafutwa na Wanakizimkazi wenzake!🤣🤣🤣
 
Nilikua nadhani ni kwenye majiji makubwa tu ila tuwe wakweli picha ya rais Samia ipo kwenye mabango karibu nchi nzima tena sehemu karibu zote potential kibiashara

Kuna mahali nilikua na kakibanda tena ndanindani sio hata main road, njia Haina hata lami walikuja TRA wakanipigia hesabu laki 3 kwa mwaka tukashindwana ikabidi nilitoe lile bango, sasa TRA mje mtueleze hayo mabango nchi nzima nani analipia kama ni chama, serikali, au watu binafsi na yanaingiza pesa kiasi Gani?
nadhani yeyote yule yuko huru kuweka mabango popote nchini ikiwa anaona inafaa, na ikiwa atapata idhini ya mamlaka husika kwenye eneo husika....

hakuna bango maalumu popote nchi , lisilolipiwa wala eti halina idhini ya mamlaka husika, labda yale ya waganga wa jadi ya kurudisha mpenz aliepotea 🐒
 
Majibu yatakuwa rahisi tu. Wanaolipia ni Wajomba Zake waliopewa bandari zote nchi hii kwa miaka 100, na kupiga marufuku uendelezaji wa bandari sehemu yoyote nchi hii bila ya ruhusa kutoka kwao
 
Back
Top Bottom