Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Watu huangamia kwa kukosa maarifa, lakini watu huangamia kwa upumbavu wao au kiburi chao.
Sisi kama Taifa na dunia kiujumla tunalo la kujifunza kutoka Uchina na nchi za Asia, kulekule ambapo ugonjwa wa Korona ulianzia! Wao waliweka sheria ya lazima kuvaa mask ukitoka nje na hiyo sheria ilikuwa very strict. Na kwa kweli hii ilielekea kuona rate ya maambukizi ikipungua siku baada ya siku mpaka wakawa katika hali inayoridhisa.
Wazungu walicheza makidamakida kwenye ishu ya barakoa, mwanzoni wakawa na mchezo wa "vaa usivae", wakaleta habari zao za "uhuru wa mtu binafsi" lakini sasa korona ilivyokuja kuwatandika kisawasawa ndo wanakumbuka kufanya uvaaji wa barakoa kuwa kitu cha lazima!, Tunaona eti madakatari wao wanashauri watu wavae barakoa doubledouble. Walikumbuka shuka asubuhi.
Sasa sisi kama Taifa hatuna luxury ya kuacha anayetaka avae na asiyetaka asivae.
Hatuna option kwa sababu:
1. Uhai wa mtu mmoja siyo mali yake peke yake ni mali ya Taifa, ndiyo maana kutaka kujiua ni kosa la jinai
2. Pili kuvaa barakoa hakumnusuru mvaaji asiambukizwe bali kunawanusuru wengine pia ambao huenda wangeambukizwa na mvaa barakoa kama ana huo ugonjwa.
3. Gharama za kupoteza mwabanchi mmoja na kwa Taifa zima ni kubwa, maana unakuta mtu ndo mlisha familia, mlipa kodi kwa serikali, daktari, mwalimu, injinia, Lecturer, mhasibu etc. Ni ujinga kutoona madhara kwa nchi kutokana na vifo vya mtu mmoja mmoja
Sasa huu siyo muda muafaka wa serikali kuendelea na approach zake za kusuasua, au za "hayanihusu kila mtu apambane na hali yake", Ni lazma serikali itimize wajibu wake wa kikatiba wa kulinda uhai wa wananchi.
Chombo kuitwa serikali maana yake ni chombo cha nguvu kwa ajili ya common good. Nchi haiwi na wanajeshi, polisi, mgambo na usalama kwa ajili ya kuweka gwaride zuri tu kwa ajili ya mtawala, baki hivi ni vyombo vya kulinda uhuru, mali na uhai wa wananchi pindi vikiwa called ob duty. Kwa hiyo kupitia vyombo hivi kwa kushirikiana na wananchi suala la kufanya uvaaji wa barakoa kuwa ni jambo la lazima linawezekana na ndiyo njia sahihi kwa sasa ili kuzuia usambaaji wa kirusi kama moto wa kiangazi.
Raisi Magufuli akumbuke tu kuwa pale alipoapishwa, alipewa ngao na mkuki, ile ngao siyo urembo, ile ni ishara kuwa ni lazima atumie uwezo wake wote kuhakikisha analilinda taifa dhidi ya hatari yoyote inayotishia maisha ya watu wake.
Hii approach ya Rais Magufuli kupigana vita ya Korona kwa shingo upande ni staili ya upiganaji legelege na ni aibu kwa kiongozi aliyeapa kulinda katiba inayotamka kuhusu haki ya kuishi kuwa legelege kwenye kulinda uhai wa watu wake.
Viongozi wa Magufuli hawaishi kwa mfano kwenye vita hii, na kwa tabia zao za kutovaa barakoa, kutoweka social distance, kuzungumiza uwepo wa korona kwa kudonyoadonyoa, kutopiga kampeni ya kuelimisha umma juu ya hatari hii kama jinsi tulivyowahi kuona kampeni mbalimbali za kitaifa zikifanywa ni aibu kubwa.
Just Imagine kuna kipindi serikali ilikuwa ikinenga awareness kubwa juu ya ugonjwa wa Tezi Dume, Mabusha etc lakini serikali hiyohiyo haitaki kuendesha kampeni kubwa kwenye vyombo vya habari vya kuelimisha umma juu ya hatari ya gonjwa hili linavyoua.
Yaani laiti muda ambao TBC wanautumia kumsifu Magufuli ungekuwa unatumika kujenga public awareness ya ugo jwa huu hakika tungeupiga vita vizuri zaidi.
Sasa Serikali iachane na denial, na iache uyageuza maisha ya watanzania sinema.