Ni muda muafaka uvaaji wa barakoa uwe jambo la lazima kwenye umma

Una scientific proof kuwa barakoa zinazuia virusi? Nafikiri hujajifunza toka mataifa ya wenzetu.

Nimeandika sana hili, lakini niandike tena angalau kwa ufupi sana:
1. Ukiacha barakoa zile za maabara na mahospitali zilizoundwa maalum kuzuia virusi hakuna utafiti unaonesha hizi tunazotumia mtaani ambazo hazikuundwa kuzuia virusi kama SARS COV2 zinazuia virusi. Hizo za kuzuia virusi ni ghali na kama mnataka watu wavae gaweni bure.

2. Corona ina mortality rate ndogo sana ukiangalia statistics zilizopo. Kuna magonjwa yanaua zaidi ya Covid na hatukuwahi kuwa na mandate. Mara zote tumefundishwa na kushauriwa kupambana na malaria. Hatujawahi kulazimishwa kununua neti. Inapobidi neti hutolewa bure na bado hulazimishwi kuifunga.

Iweje leo Corona yenye mortality rate ndogo tuanze kuwatisha watu na mask mandate? Utaratibu mzuri ni kuwaelimisha watu namna gani barakoa inazuia na kuwapa bure. Sio kuwatisha na kuwalazimisha.

Mwisho niseme tu nawashauri mnaopenda na kuona barakoa ni mkombozi msigeuke Gestapo wa Hitler. Kama barakoa inazuia virusi hamna tatizo, vaa na utakuwa salama. Asiyevaa achana nae, ni mtu mzima ana akili timamu huyo.

Ukiona unadhani hana elimu jaribu kumuelimisha. Kiufupi anayevaa barakoa amheshimu asiyevaa. Vivyo hivyo asiyevaa barakoa amheshimu anayevaa. Mmoja asijaribu kuingilia uhuru wa mwingine wala kugeuka askari wa Hitler kuwa terrorize wasiokubaliana na upande wake.

Mask mandate is new dictatorship. It should be avoided and fought at all levels. We are grownup humans not sheeps or pigs!
 
Una reference yoyote ya kisayansi kuonyesha barakoa zinazuia ukiacha zile za maabara zilizotengenezwa maalum kuziia virusi?

Wengi naona huwa tunachukulia zile picha tunazosambaziana kwenye mitandao ya kijamii kama proof. Zile ni picha hata mimi naweza tengeneza. Utafiti wa kisayansi upo unao sapoti notion hii?

Maana ukiangalia diameter ya virus na diameter ya matundu ya barakoa zetu, unajiuliza akitua pale juu nikivuta hewa si namvuta anaingia? Barakoa zinazuiaje?
 
Upo utafiti unaoonyesha barakoa hata hizi za vitambaa zinasaidia kwa kiasi kikubwaa kuzuia kusambaa kwa virusi vya korona
 

Attachments

Kuongezea; barakoa zenyewe ziwe za kushona, sio hizi zinazotumiwa na madaktari wakati wa upasuaji.

Vv
 
"The objective of this study was to investigate whether cotton mask worn by respiratory infection person could suppress respiratory droplet levels compared to medical mask"

Hili sidhani kama kuna anayepinga. Naulizia tafiti za barakoa kuzuia virusi na sio comparison ya aina ya barakoa ambao Hili andiko limetafiti
 
UVCCM na MATAGA hawawezi kukuelewa, wao huwa wanasikilizia siku hiyo jiwe amesema nini. Leo akisema barakoa hazifai wanashangilia na kusema kuwa huyo ndiye mwanasayanso makini, kesho akisema barakoa zinakinga korona watampongeza kuwa anajali wanyonge
 
Wewe si umevaa balakoa nani atakuambukiza!.kila mtu aamini chake.korona ipo ila kwenye tatizo ambalo halina ufumbuzi kila mtu ana mbadala wake anaoona unamfaa.
 
Umeamua kubisha for the sake ya kubisha au unachallenge objective ya study husika.

Sasa kwani hujui Covid inakuwa transmitted pia kupitia respiratory droplets (vikohozi, mate etc?)

Huoni kwenye methodology hapo walitumia pia suspected cases za watu wenye Covid kama case study?

Huoni kuwa conclusion inasema kuwa kwenye kuzuia respiratory transimisable deseases barakoa zote ziwe za vitambaa(pamba) na hizo nyingine bora zaidi zote zimekuwa effective kwenye kuzuia droplets zinazotransmit hizo desease

Au mzee ulidhani kuwa waliinclude wenye Covid kwenye study yao kama urembo tu?

Ukiwa mbishi basi umeamua kuwa mbishi but study iko clear na zipo nyingi tu za kuonyesha kuwa mask works kwenye covid
 
Wewe si umevaa balakoa nani atakuambukiza!.kila mtu aamini chake.korona ipo ila kwenye tatizo ambalo halina ufumbuzi kila mtu ana mbadala wake anaoona unamfaa.
Mimi unaweza usiniambukize kwa kuwa nimevaa, ila anaweza akaambukizwa mbishi mwingine wa kuvaa barakoa kama wewe au akaambukizwa mtoto asiyevaa barakoa atakayeenda kuambukiza wazee wake nyumbani, au akaambukizwa mtu mwingine tu asiye na uelewa mzuri wa kujikinga na Covid.

Mimi siyo selfish, siyo lazima nijilinde peke yangu, namjali hata mtu mwingine nisiyemfahamu
 
Hakuna haja ya kunishambulia, present facts na sio kumshambulia mtu. Kama kukushambulia personally sio kwamba uwezo sina ila ni upumbavu kufanya hivyo wakati mjadala ni kwenye facts.

Point yangu ni straight forward na sidhani kama ni ngumu kueleweka. Tunavaa barakoa ili kujikinga na Virusi vya Corona. Ili ikubalike scientifically lazima ufanyike utafitj dedicatedly ambao utakuwa conclusive kwamba barakoa zinazuia virusi vya covid na ni kwa kiasi gani.

Utafiti ulioleta ni wenye lengo la kuonesha kuwa medical mask zina effectiveness ambayo haitofautiani sana na Cotton mask. Lengo lao liko wazi upfront kwenye abstract na kuendelea.

Huu utafiti ulilenga kuondoa mashaka juu ya kutimia cotton mask badala ya medical mask. Haukulenga kuonyesha kama barakoa zinazuia virusi ama la.

Ndio nimekuomba uniletee utafiti unaoonesha barakoa ni kinga dhidi ya virusi vya Corona. Umeishia kunishambulia tu, kitu ambacho hakisaidii kitu.

Twende kisayansi japo ni jukwaa la siasa. Tuliza munkari, hakuna anayetafuta ushindi hapa. Tunatafuta ile iliyo kweli.

Wakati nasubiri utafiti nilioomba, kuna point zingine za msingi umeziruka kwenye bandiko langu la kwanza. Hebu zichungulie!
 
Ni bora kusisitiza watu kunawa kwa maji tiririka na sabuni kuliko hayo mavitambaa. Mdudu anaenea kupitia mikono siyo hewa. Somo hili tangu mwaka jana limesomeshwa lakini mnazidi kuatamia mbinu za kibeberu. Tumia NIMRICAF, COVIDO na NYUNGU
 
Findings za hiyo study inasema effectiveness ya aina zote za barakoa inashabihiana, sasa swali la msingi ni kuwa hiyo effectiveness ni effectiveness katika nini?, na significance ya hiyo effectiveness ni nini ?

majibu ya maswali yote hayo yamo katika hiyo study. yako open kabisa

Pia swali jingine ni kwenye methodoojia kwa yao kwa nini watumie pia Covid suspected cases, walitaka kuachieve nini?
 
Mkuu umenena hoja kubwa sana. Wataalamu wa kizungu wanasema tuvae barakoa ingawa wao wenyewe wanasema haijathibitika kuwa zinazuia maambukizi. Ikiwa mtu anawaunga mkono avae, hakuna anayemkataza.

Wataalamu wetu wanasema tujifukize, tupige tangawizi, vitunguu, limao, mdalasini, nk. Tunaowaamini tuachwe tufanye hayo bila kulazimishwa kufanya hayo watakayo wazungu.

Mie hapa na-type huku namalizia juice yangu ya;

Tangawizi + Limao + Asali

Halafu niko confident wala sina shaka na huo ugonjwa wao.
 
πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎKabisa Mkuu asiyevaa barakoa ni MUUAJI.
You are absolutely correct. Put on a mask wherever you go. You will be saving your life as well as of others. "Asiyevaa barakoa ni MUUAJI".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…