Hamza Nsiha
JF-Expert Member
- Jul 25, 2022
- 221
- 197
NI MUDA MUAFAKA WA KUINUA VILIVYO VYETU.
Utangulizi.
Mpaka sasa, kumekuwa na imani hafifu kwa watanzania hasa linapokuja suala la kukubali vitu mbalimbali vinavyotengenezwa au kuzalishwa na raia kutoka nchini. Imani hii hafifu imekwenda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kudharau na kukandamiza baadhi ya huduma au bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa nchini, hivyo kupelekea kuwepo na ushindani uliokithiri kati ya bidhaa za ndani dhidi ya bidhaa za nje. Huku ikionekana dhahiri bidhaa zilizotengenezwa nchini kukosa soko zaidi ukilinganisha na bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
Baadhi ya maeneo ambayo yanaonekana kupokea upinzani mkubwa kutoka kwa wazawa.
Ni ukweli usiopingika kuwa kuna baadhi ya maeneo mengi ambayo yamepoteza imani kwa Watanzania licha ya kujitahidi katika kutoa huduma au bidhaa bora kwa watanzia. Baadhi ya maeneo hayo ni kama ifuatavyo;
Je, ukweli ni upi juu ya suala hili?
Ukweli ni kuwa kuna sababu kadha wa kadha zinazopelekea mambo haya kuonekana kwa wananchi, baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo;
Je, ni kipi kifanyike ili kuondoa tatizo hili kwa Watanzania?
Ni dhahiri kuwa wahenga waliposema “ukiona vya elea ujue vimeundwa” hakika walikuwa sahihi, ni wakati wetu sasa wa kuinua vilivyo vyetu hususani katika kipindi hiki ambacho bidhaa nyingi zimeonekana kupanda bei kutokana na migogoro iliyopo baina mataifa makubwa tegemezi.Vifuatavyo ni baadhi ya vitu vinavyotakiwa kutiliwa mkazo ili kuinua thamani ya bidhaa zetu nchini;

- Viwanda vya bidhaa za majumbani, kuna viwanda vingi nchini Tanzania vilivyojikita katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zitumikazo majumbani kama vile sabuni, samani. Hizi ni baadhi ya bidhaa ambazo zinazalishwa kwa wingi nchini Tanzania, lakini mapokeo ya baadhi ya watanzania yamekuwa ni tofauti huku wengi wakiamini bidhaa hizo si bora ukilinganisha na zile zinazoagizwa nje ya nchi.
- Viwanda vya bidhaa kama nguo, viatu pamoja na vitu vya urembo kama nywele bandia. Pia linapokuja suala la bidhaa hizi, bado inaonekana kuwa kuna upinzani mkubwa wa wananchi kukubali bidhaa hizi huku wengi wakiamini zaidi bidhaa zinazotoka nje. Mfano, nguo au viatu vya mtumba.
- Huduma mbalimbali za kijamii kama vile elimu, afya n.k. Pamoja na serikali kuonesha jitihada zake katika kuboresha huduma za kijamii bado kuna baadhi ya wananchi ambao hawana imani thabiti juu ya huduma hizo. Mfano, wananchi wengi huamini zaidi huduma za afya au elimu zinazotolewa nje ya nchi hata kama ni nchi ambayo iko nyuma kiuchumi ukilinganisha na Tanzania.
- Sekta ya michezo, sambamba na yote bado wananchi wengi hawana imani juu ya ubora wa michezo yetu ya ndani. Mfano dhahiri huonekana hata kwa mashabiki ambavyo hujenga imani kubwa kwa wachezaji wanaotoka nje ya nchi hata kama viwango vyao kuwa sawa na wachezaji wa ndani ya nchi.
Je, ukweli ni upi juu ya suala hili?
Ukweli ni kuwa kuna sababu kadha wa kadha zinazopelekea mambo haya kuonekana kwa wananchi, baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo;
- Uchakachuaji wa bidhaa unaofanywa na baadhi ya wazalishaji. Kuna baadhi ya wamiliki wa viwanda wamekuwa wakizalisha bidhaa ambazo ni dhahiri kuwa zimechakachuliwa, hii kupelekea kutodumu kwa muda mrefu. Jambo hili limefanya wananchi wengi kuondoa imani hata kwa baadhi ya wazalishaji wa nchini ambao bidhaa zao ni halisi na zenye ubora wa hali ya juu.
- Gharama za upatikanaji wa bidhaa zinazozalishwa nchini. Ukweli ni kwamba, baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini huonekana ni aghali mno ukilinganisha na bidhaa zinazotoka nje ya nchi jambo hili limefanya wananchi wengi kususia bidhaa za ndani na kupendelea zaidi bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
- Nguvu ya ushawishi kutoka kwa watu mashuhuri. Pia kumekuwepo na kasumba ya kufuata mkumbo kwa baadhi ya watu mashuhuri katika kufanya jambo fulani. Mfano dhahiri huonekana kwa baadhi ya watu ambao hupendelea kutumia vilevi kutoka nje ya nchi kwa sababu vimeonekana vikitumika na wasanii wakubwa, mf. Pombe aina ya Hennessy, Jack Daniels, Russian Vodka, jambo ambalo limedidimiza vilevi/vinywaji vinavyozalishwa nchini.
Je, ni kipi kifanyike ili kuondoa tatizo hili kwa Watanzania?
Ni dhahiri kuwa wahenga waliposema “ukiona vya elea ujue vimeundwa” hakika walikuwa sahihi, ni wakati wetu sasa wa kuinua vilivyo vyetu hususani katika kipindi hiki ambacho bidhaa nyingi zimeonekana kupanda bei kutokana na migogoro iliyopo baina mataifa makubwa tegemezi.Vifuatavyo ni baadhi ya vitu vinavyotakiwa kutiliwa mkazo ili kuinua thamani ya bidhaa zetu nchini;
- Utiliaji mkazo katika ukaguzi wa bidhaa kabla hazijamfikia mtumiaji. Licha ya kuwepo kwa kaguzi mbalimbali bado kuna baadhi ya wazalishaji ambao wamekuwa wakitumia njia za panya katika kupitisha bidhaa zao sokoni. Hivyo ni wakati thabiti wa serikali kupitia taasisi yake husika kuongeza mkazo juu ya suala hili kwa kuziba mianya yote batilifu ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa au huduma bora kwa wananchi.
- Uwiano wa bei baina ya bidhaa zinazozalishwa nchini na zile zinazotoka nje. Suala la bidhaa kuwa na bei kubwa hutokana na sababu mbalimbali kama vile tozo za kodi kutoka katika mamlaka husika, ubora pamoja na upatikanaji wake. Ni muda muafaka wa serikali kutoa msaada kwa wazalishaji wazawa ili kuongeza ushindani kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
- Kuinua viwanda vidogovidogo vilivyopo nchini. Pia ili kuonesha nia ya kuthamini bidhaa zetu ni wakati muafaka wa serikali pamoja na mashirika binafsi kuweka mikakati thabiti itakayolenga kuinua viwanda vidogovidogo vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ili kuendana na soko la ushindani juu ya bidhaa zingine.
- Kuongeza juhudi katika kuwahusisha watu mashuhuri au wenye ushawishi wa hali ya juu katika matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini. Mfano matangazo ya bidhaa kama vile vinywaji, mavazi, sabuni n.k. hii itasaidia katika kuvuta imani za watu juu ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini.
- Uboreshaji wa matamasha mbalimbali yanayohusu maonesho mbalimbali ya bidhaa kutoka kwa wajasiriamali. Hii ni pamoja na kuweka mashindano mbalimbali kwa wabunifu/watengenezaji wa bidhaa mbalimbali ili kutia chachu katika uboreshaji wa huduma au bidhaa zao.
- Sambamba na yote, ni wakati wetu pia kudumisha uzalendo kwa kukubali na kupenda huduma au bidhaa zinazozalishwa nchini. Yote yanaweza kufanyika lakini likabakia suala la uzalendo kwani hili ndio jambo kuu katika kuona thamani ya vilivyo vyetu. Kwa sababu kupitia uzalendo ni dhahiri kuwa tunaweza kushirikiana kwa pamoja katika kuimarisha misingi itakayotuwezesha kuwepo kwa uzalishwaji wa bidhaa au utolewaji wa huduma bora nchini. Mfano kuripoti baadhi ya taarifa zinazohusu bidhaa feki au huduma zitolewazo kwa kiwango cha chini.
Upvote
28