SoC02 Ni muda muafaka wa kuinua vilivyo vyetu

SoC02 Ni muda muafaka wa kuinua vilivyo vyetu

Stories of Change - 2022 Competition

Hamza Nsiha

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2022
Posts
221
Reaction score
197
NI MUDA MUAFAKA WA KUINUA VILIVYO VYETU.

Utangulizi.

Mpaka sasa, kumekuwa na imani hafifu kwa watanzania hasa linapokuja suala la kukubali vitu mbalimbali vinavyotengenezwa au kuzalishwa na raia kutoka nchini. Imani hii hafifu imekwenda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kudharau na kukandamiza baadhi ya huduma au bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa nchini, hivyo kupelekea kuwepo na ushindani uliokithiri kati ya bidhaa za ndani dhidi ya bidhaa za nje. Huku ikionekana dhahiri bidhaa zilizotengenezwa nchini kukosa soko zaidi ukilinganisha na bidhaa zinazotoka nje ya nchi.

Baadhi ya maeneo ambayo yanaonekana kupokea upinzani mkubwa kutoka kwa wazawa.
Ni ukweli usiopingika kuwa kuna baadhi ya maeneo mengi ambayo yamepoteza imani kwa Watanzania licha ya kujitahidi katika kutoa huduma au bidhaa bora kwa watanzia. Baadhi ya maeneo hayo ni kama ifuatavyo;
  • Viwanda vya bidhaa za majumbani, kuna viwanda vingi nchini Tanzania vilivyojikita katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zitumikazo majumbani kama vile sabuni, samani. Hizi ni baadhi ya bidhaa ambazo zinazalishwa kwa wingi nchini Tanzania, lakini mapokeo ya baadhi ya watanzania yamekuwa ni tofauti huku wengi wakiamini bidhaa hizo si bora ukilinganisha na zile zinazoagizwa nje ya nchi.
  • Viwanda vya bidhaa kama nguo, viatu pamoja na vitu vya urembo kama nywele bandia. Pia linapokuja suala la bidhaa hizi, bado inaonekana kuwa kuna upinzani mkubwa wa wananchi kukubali bidhaa hizi huku wengi wakiamini zaidi bidhaa zinazotoka nje. Mfano, nguo au viatu vya mtumba.
  • Huduma mbalimbali za kijamii kama vile elimu, afya n.k. Pamoja na serikali kuonesha jitihada zake katika kuboresha huduma za kijamii bado kuna baadhi ya wananchi ambao hawana imani thabiti juu ya huduma hizo. Mfano, wananchi wengi huamini zaidi huduma za afya au elimu zinazotolewa nje ya nchi hata kama ni nchi ambayo iko nyuma kiuchumi ukilinganisha na Tanzania.
  • Sekta ya michezo, sambamba na yote bado wananchi wengi hawana imani juu ya ubora wa michezo yetu ya ndani. Mfano dhahiri huonekana hata kwa mashabiki ambavyo hujenga imani kubwa kwa wachezaji wanaotoka nje ya nchi hata kama viwango vyao kuwa sawa na wachezaji wa ndani ya nchi.

Je, ukweli ni upi juu ya suala hili?
Ukweli ni kuwa kuna sababu kadha wa kadha zinazopelekea mambo haya kuonekana kwa wananchi, baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo;
  • Uchakachuaji wa bidhaa unaofanywa na baadhi ya wazalishaji. Kuna baadhi ya wamiliki wa viwanda wamekuwa wakizalisha bidhaa ambazo ni dhahiri kuwa zimechakachuliwa, hii kupelekea kutodumu kwa muda mrefu. Jambo hili limefanya wananchi wengi kuondoa imani hata kwa baadhi ya wazalishaji wa nchini ambao bidhaa zao ni halisi na zenye ubora wa hali ya juu.
  • Gharama za upatikanaji wa bidhaa zinazozalishwa nchini. Ukweli ni kwamba, baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini huonekana ni aghali mno ukilinganisha na bidhaa zinazotoka nje ya nchi jambo hili limefanya wananchi wengi kususia bidhaa za ndani na kupendelea zaidi bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
  • Nguvu ya ushawishi kutoka kwa watu mashuhuri. Pia kumekuwepo na kasumba ya kufuata mkumbo kwa baadhi ya watu mashuhuri katika kufanya jambo fulani. Mfano dhahiri huonekana kwa baadhi ya watu ambao hupendelea kutumia vilevi kutoka nje ya nchi kwa sababu vimeonekana vikitumika na wasanii wakubwa, mf. Pombe aina ya Hennessy, Jack Daniels, Russian Vodka, jambo ambalo limedidimiza vilevi/vinywaji vinavyozalishwa nchini.

Je, ni kipi kifanyike ili kuondoa tatizo hili kwa Watanzania?
Ni dhahiri kuwa wahenga waliposema “ukiona vya elea ujue vimeundwa” hakika walikuwa sahihi, ni wakati wetu sasa wa kuinua vilivyo vyetu hususani katika kipindi hiki ambacho bidhaa nyingi zimeonekana kupanda bei kutokana na migogoro iliyopo baina mataifa makubwa tegemezi.Vifuatavyo ni baadhi ya vitu vinavyotakiwa kutiliwa mkazo ili kuinua thamani ya bidhaa zetu nchini;
  • Utiliaji mkazo katika ukaguzi wa bidhaa kabla hazijamfikia mtumiaji. Licha ya kuwepo kwa kaguzi mbalimbali bado kuna baadhi ya wazalishaji ambao wamekuwa wakitumia njia za panya katika kupitisha bidhaa zao sokoni. Hivyo ni wakati thabiti wa serikali kupitia taasisi yake husika kuongeza mkazo juu ya suala hili kwa kuziba mianya yote batilifu ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa au huduma bora kwa wananchi.
  • Uwiano wa bei baina ya bidhaa zinazozalishwa nchini na zile zinazotoka nje. Suala la bidhaa kuwa na bei kubwa hutokana na sababu mbalimbali kama vile tozo za kodi kutoka katika mamlaka husika, ubora pamoja na upatikanaji wake. Ni muda muafaka wa serikali kutoa msaada kwa wazalishaji wazawa ili kuongeza ushindani kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
  • Kuinua viwanda vidogovidogo vilivyopo nchini. Pia ili kuonesha nia ya kuthamini bidhaa zetu ni wakati muafaka wa serikali pamoja na mashirika binafsi kuweka mikakati thabiti itakayolenga kuinua viwanda vidogovidogo vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ili kuendana na soko la ushindani juu ya bidhaa zingine.
  • Kuongeza juhudi katika kuwahusisha watu mashuhuri au wenye ushawishi wa hali ya juu katika matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini. Mfano matangazo ya bidhaa kama vile vinywaji, mavazi, sabuni n.k. hii itasaidia katika kuvuta imani za watu juu ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini.
  • Uboreshaji wa matamasha mbalimbali yanayohusu maonesho mbalimbali ya bidhaa kutoka kwa wajasiriamali. Hii ni pamoja na kuweka mashindano mbalimbali kwa wabunifu/watengenezaji wa bidhaa mbalimbali ili kutia chachu katika uboreshaji wa huduma au bidhaa zao.
  • Sambamba na yote, ni wakati wetu pia kudumisha uzalendo kwa kukubali na kupenda huduma au bidhaa zinazozalishwa nchini. Yote yanaweza kufanyika lakini likabakia suala la uzalendo kwani hili ndio jambo kuu katika kuona thamani ya vilivyo vyetu. Kwa sababu kupitia uzalendo ni dhahiri kuwa tunaweza kushirikiana kwa pamoja katika kuimarisha misingi itakayotuwezesha kuwepo kwa uzalishwaji wa bidhaa au utolewaji wa huduma bora nchini. Mfano kuripoti baadhi ya taarifa zinazohusu bidhaa feki au huduma zitolewazo kwa kiwango cha chini.
Kwa ujumla, ni ukweli usiopingika kuwa tunao uwezo na nguvu ya kushindana katika masoko mbalimbali duniani endapo tu tutakapo kubali kuwa huduma na bidhaa zetu ni bora kama zilivyo zingine. Hivyo ni wakati wetu sahihi wa kukubali na kuthamini vilivyo vyetu kwani hata hayati Dr. John Pombe Magufuli aliwahi kusema kuwa “ni lazima tuipende nchi yetu, kwani hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania”.
 
Upvote 28
Ni kweli kabisa yaani tunasahau kuwa hao wenzetu walianza kama sisi ili wao wakaviboresha vya kwao hadi vimefika hapo vilipo. Point sanaaa hii Kiongozi natamani hata ingekuw sheria kabisa watu kuapply uzalendo
Kweli mkuu angalia mfano wajerumani na viwanda vyao bora vya magari, Korea Kusini na kiwanda chao kikubwa cha Samsung, Kiukweli ni wakati wetu na sisi kuinua vya kwetu.
 
IDEAS ZA KUTOKA KIMAISHA KWA MTAJI MDOGO

1.Nunua pikipiki ya Dhamana ukaanza biashara ya Boda boda.
2.Fungua saluni
3.Mradi wa tofali za kuchoma
3.Fuga kuku
4.Somea ujuzi wowote
5.Mradi wa kushona nguo
6.kijiwe cha kuchomelea
7.kijiwe cha milango na madirisha ya aluminum
8.Mgahawa Mdogo
9.Kijjwe cha kahawa
10.Mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga, mtama, karanga, nk
11.Mashine ya kukata nyasi, kupalilia
12.Kuuza mbuzi, kuku,
13.Biashara ya mazao.
14.kukodi bus, daladala na kuzisimamia upate cha juu
15.Kutengeneza sabuni, sanitizer, handwash,
16.Kutengeneza unga wa lishe
17.Kilimo cha umwagailiaji water pump, mbegu, madawa
18.Jiko la supu
19.kutengeneza mkaa mbadala
20.Kuuza chips
21.Kukaanga kuku
22.Kutengeneza vitafunio
23.Kuzalisha ethanol
24.kufuga poko mbuzi katoliki
25.Kufungua kilabu cha pombe za kienyeji
26.Kufungua vijiwe vya Kukusanya ubuyu maporini yakitimia magunia unaleta mjini
27.Kuuza juice
28.Kuuza juice ya miwa
29.Kijiwe cha kukaanga samaki jioni
30.Shughuli za upambaji kumbi
31.Kusambaza bidhaa majumbani
32.Kusambaza bidhaa basic needs kwenye maduka ya vijijini yaani unanua mjini unasambaza kwa oda viduka vya vijijini.
33.Kuzunguka minadani kuuza nguo za mitumba, vyombo, nk
34.Kufungua tuition center
35.Kufungua grocery
36.Kuwa wakala wa bidhaa za viwandani
37.kijiwe cha kukusanya taka za plastic, chuma,oil chafu na tairi chakavu.
38.Kufungua genge la kuuza basic home need
39.Kufungua ofisi ya kupiga nguo pasi.
40.Ofisi ya kutengeneza viatu na mabegi
41.Kutengeneza vyombo vya kupikia mfano, majiko, ndoo, sufuria, mifuniko, vikaangio, nk
42.Saluni ya kutengeneza kucha za wanawake
43......Jengea vyumba vitatu wazazi wako nyumba ya Bati upate baraka
44..Nunua shamba
45.Nunua ng'ombe wadogo watano kwa laki na nusu anza ufugaji.
Au nunua mbuzi anza kufuga
46.Fungua kijiwe cha kuonyesha mpira
47.duka la nguo za kupoint classic za mitumba piga pasi tundika kwenye enga
48..Ofisi za baiskeli za kukodi hapo unapata baiskeli nane
49..Duka la spea za pikipiki na baiskeli
50.Duka la dawa na vipodozi
51..ofisi ya kuchaji simu kwa sola vijijini
52..ofisi ya uwakala wa kutuma na kutoa pesa
53.. Bustani za kuzalisha miche ya miti na matunda
54... Ufugaji nyuki na kuuza asali
55.. Kuzalisha unga wa muhogo
56..Direct sale yaani door to door delivery hapa unakuwa na torori na speaker unapita KILA nyumba unauza bidhaa na kuchukua oda ya nini wanataka Ili kesho uwaletee.
57.Utengenezaji pellets chakula cha mifugo,samaki.
58..unga wa lishe
59..mikeka
60.bidhaa za mianzi.
61.wine,
62.usafi wa majumbani
63.kuuza uji wa ulezi,mchele
64.utengenezaji mbolea za mboji na za maji.
65.utengenezaji wa vigae vya cement na vya udongo.
66.kupanda miti kwa ajili ya nguzo na mirunda
67.utengenezaji wa ndala
68.utengenezaji viatu
69.Upondaji kokoto
70.ufundi simu na radio
71
 
Good idea mkuu! But Kura yako muhimu Kiongozi Vote^
 
hii ilikuwa na bado itakuwa ndoto ya wengi tangu nchi mbali mbali barani Afrika zionje uhuru!

ila leo nimesoma "Nasaha Za Mihangwa" (kurasa ya 7, Raia Mwema) nikaelewa jinsi gani Waafrika tumegawanyika.

Kuna wale wazalendo na kuna wale mzungu akisema hili basi nalo liwe, at any cost!

Huenda nipo nje ya mada ila hii posti imenikumbusha sana nasaha hiyo!
 
Uko sahihi mkuu! Lakini atleast sasa hivi tuanze kuona umuhimu wake nadhani tumejifunza ata kupitia migogoro ya Mataifa makubwa hivi sasa kuna baadhi ya vitu havishikiki kwa bei lakini kama tungekuwa tumeinua vitu vyetu kwa kiasi kikubwa ingetusaidia sana!
 
Mimi pia ni mkereketwa wa hili jambo mfano sabuni za JAMAA ambazo hutengenezwa Kenya zmekuwa maarufu utadhani zinatoka Tanzania ipo haja kubwa ya wazalishaji wetu kuboresha ubora wa bidhaa zao.
 
Umenena vema kaka angu, mfano wa viwanda vikubwa ni MO~DEWJI COMPANY LTD, BAKHRESA n.k hivi viwe mifano bora kwa wengine hakina kwangu naona vinajitahidi. Nimependa tittle yako ya Ni muda muafaka wa kuinua vilivyo vyetu.
 
Hii ni kweli kabisa baadhi ya wazalishaji wetu ni wachakachuaji mfno japo naomba nisitaje jina la kiwanda kipo Dar es Salaam kinajihusisha na utengenezaji wa nywele bandia. Kwakwel niliwahi kununua nywele zao nilikoma sidhani kama nitarudia bora niendelee na Brazilian hair tu mpk watakapotushawishi.
 
Hakika kuna wanaozalisha bidhaa halali na wachakachuaji tatizo linaanzia hapa ndio maana nimesuggest mamlaka husika zitazame hili kwa ukubwa
 
Umenena vema kaka angu, mfano wa viwanda vikubwa ni MO~DEWJI COMPANY LTD, BAKHRESA n.k hivi viwe mifano bora kwa wengine hakina kwangu naona vinajitahidi. Nimependa tittle yako ya Ni muda muafaka wa kuinua vilivyo vyetu.
Asante kwa mchango wako ndugu yangu Vote ^
 
Mimi pia ni mkereketwa wa hili jambo mfano sabuni za JAMAA ambazo hutengenezwa Kenya zmekuwa maarufu utadhani zinatoka Tanzania ipo haja kubwa ya wazalishaji wetu kuboresha ubora wa bidhaa zao.
Ni kweli kabisa hizi bidhaa zimekuwa maarufu kulingana na ubora wake ukilinganisha na sabuni zetu za POA, sabuni za MAGADI hivyo tuone kama changamoto kwetu ili tuzidishe bidii
 
Wazalishaji wa nyumbani waongeze ubora kwenye bidhaa zao kama Bakhresa na Azam Tv anakimbiza kina DSTV hadi zinauzwa alfu ishirini plus free delivery and free installation
 
Wazalishaji wa nyumbani waongeze ubora kwenye bidhaa zao kama Bakhresa na Azam Tv anakimbiza kina DSTV hadi zinauzwa alfu ishirini plus free delivery and free installation
Yaaaap ni kweli kabisa Azam Tv kuwa kituo bora cha matangazo kinastahili kwa sababu ya ubora wa huduma zake mfno. Huwa nikifikiria vipindi vyake, quality za High Definition, bei zake kwakwel ni mfano bora sana!
 
Chapisho zuri, lakini pia ungeongezea hata kwa taasisii za rushwa maana kuna watu katika mamlakaa wanakula rushwa kupitisha bidhaa mbovu.
 
Back
Top Bottom