mbwangali
JF-Expert Member
- Jan 8, 2021
- 2,266
- 4,057
Shukrani mkuu kwa kunipa mwanga najaribu sana kuielewa hii ndoto maana ndio ndoto naiota sana kuliko zingine na huwa nakumbuka kila kitu. ila naamini ipo siku nitaelewa vizuriSijaweza kusema naweza kutafsiri ndoto za watu wengine ila naweza kukusaidia ukaweza kujua maana ya ndoto yako. Njia rahisi ya kuweza kutambua maana ya ndoto ni kutizama vitu vitatu kwanza ni (a)kitendo unachofanya ndotoni (b)unaangalia ulikuwa na hisia gani wakati unaota hiyo ndoto na hata baada ya kuamka(c)na Symbol.
Symbol ya daraja kwenye ndoto inaweza kuashiria transition kutoka sehemu moja kwenda nyengine katika maisha au uwezo wa kushinda changamoto kwenye maisha.
Sasa kwa kuangalia kitendo hapo tunaona unajaribu kuvuka daraja kwenda upande mwengine ila inashindikana unaishia kati, sasa jaribu kuhusisha hicho kitendo (cha kushindwa kuvuka daraja kwenda upande wa pili kila unapojaribu unafeli) na maisha yako yako halisi, wapi kwenye maisha yako unahisi unashindwa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine?