Ndoto ni namna mojawapo ya MUNGU kuwasiliana na wanadamu.Kupitia ndoto,MUNGU anatupa maonyo kuhusu yaliyopita na kutupa ushauri wa namna ya kubadilika for our own good.Kupitia ndoto,anatutabiria yajayo,yawe mazuri au mabaya.
Ukiona umeacha kuzikumbuka ndoto zako,basi jua kwamba umefungwa kiroho ili usiweze kuwasiliana na MUNGU.
Kama kuna maovu unayafanya,jaribu kufanya toba na jitahidi kujuta na kuachana kabisa na hayo maovu.Ukifanya haya,njoo utupe mrejesho nini kimetokea.
Nimewahi kupitia hali kama yako,ila nilijichunguza na nikajirekebisha kasoro zangu na hali ikarudi kama mwanzo.Japokuwa hizi ndoto tunazoziota huwa hazinaga maana ya moja kwa moja vile ulivyoiota,hivyo unahitaji mtaalam wa kukutafsiria,usije ukaota msiba ukadhani ni msiba kweli!