Ni muda sasa umefika makanisani kuwe na bar ndogo za kunywa pombe, waumini wanywe pombe kusuuza nafsi,

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Exception ni wakristo wachache sana kama wasabato wanaoamini bado Mungu huchukizwa na Pombe.

Hata ma askofu wakati wa misa hunywa mvinyo takatifu mbele ya macho yetu, sioni ubaya wowote kuwe na min bar makanisani kwajili ya waumini



Makanisani kuwe na bar ndogo ila kuwe na sheria mtu apige chupa mbili ama tatu ili awe katika kundi la mywaji (kulewa kidogo) na si mlevi.

Alafu kitu kizuri zaidi ni kwamba makanisa huwa yana misamaha ya kodi na tozo, si hivyo tu lakini pia wanaweza kuuza bila faida, hii itafanya bei iwe rahisi kuliko hata kwenye kambi za jeshi.


Agano la kale lilishapitwa na wakati kwa dini zinazoamini Mungu hachukizwi na Pombe, si pombe tu hata sheria za wanyama wa kula zilishapitwa na wakati watu wanagonga kitimoto, Hata sheria za agano la kale kuhusu mavazi zilishapitwa na wakati sikuhizi makanisani kawaida kukuta mwanamke kavaa suruali ama gauni linamchoresha hips, mapaja na makalio.


Mithali 31:6 -7

Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.

Ukiona maada hii imekuchukiza kwa kuona labda nadhihaki imani yako, jiulize mwenyewe "ni kwanini namuona mtoa post kanidhihaki wakati kashauri pombe iliyoruhusiwa na kanisa iwepo kanisani ?" ikiwezekana jipigie makofi kwa kupata akili ya kutambua kwamba Pombe ni chukizo kwa Mungu,
 
Na hii ni Pombe sio Chai wale wazee wa Chai leo mnywe Pombe kwenye mabanda ya uwani ya kanisa
 
Naunga mkono hoja, pamoja na nyama choma kitimoto na huku mziki laini, Bwana asifiwe🀣🀣🀣
 
Labda wakatoliki ndio wataweza
 
shusha mstari huo, ujue utapingwa kwa mstari pia
Mithali 31:6 -7

Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.

Huyu ni mnywaji wala si mlevi wa kutandika nusu kreti, ana chupa zake mbili tu, shida ashazisahau hapa

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…