lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Sasa si mpaka tujue kua ana bahati hiyo?š¤£Makocha hivo sometimes wana bahati utashangaa kaifikisha mbali
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa si mpaka tujue kua ana bahati hiyo?š¤£Makocha hivo sometimes wana bahati utashangaa kaifikisha mbali
Aaaahaa,na ndilo linalowatesa wanasimba hilo
Hahahaaaa we jamaaWazee wa direct football.
Kila siku huwa najiuliza wakinachilund wamesajiliwa kwa minajili ipi? Mana hata kwenye ligi hawapewi nafas walau zile dk za jion.Wachezaji wengi wamechoka timu haina plan B, kuna vijana pale wanakaa bench ni vizuri wapewe nafasi waonyeshe uwezo wao.
Nazani umeona.Hahahaaaa we jamaa
Tatizo ni bench lote la ufundi yaani wachezaji hawana fitness kabisaa wako slow na legelege kama bamia kocha hana uwezo wa kuwa simba ni big club kuliko uwezo wa kochaTatizo ni wachezaji
Mliwapeleka uturuki kwa mafungu unategemea nini ??Tatizo ni bench lote la ufundi yaani wachezaji hawana fitness kabisaa wako slow na legelege kama bamia kocha hana uwezo wa kuwa simba ni big club kuliko uwezo wa kocha
Bro AYA ya pili msitari wa 13, ile ni pre-season na sio per season.Ukiona kocha anatumia wachezaji wale wale kila mechi basi jua kabisa huyo kocha hana mbinu mpya. Kwa kocha mzuri mwenye mbinu hawezi kutumia wachezaji wale wale kwani kila timu pinzani ina mfumo tofauti. Lakini kwa Robertino yeye mechi zote hata za krafiki na vitimu vidogo vidogo wachezaji wanatumika wale wale maana yake huyo kocha hana mbinu mpya. Na mbaya zaidi hata kufanya "sub" anaogopa wakati ni yeye mwenyewe alikuwa analalamika wakati ligi inaisha kuwa ana kikosi finyu. Kaletewa kikosi kipana hawezi tena kukitumia. Kaletewa benchi la ufundi alilotaka yerye pamoja na mchezaji wake Onana lakini Simba ndio imekuwa hovyo kuliko hata Simba iliyopita ya wakina Okra na Nyoni.
Sijajua kocha wa viungo Adel Zrane alifanya kosa gani kubwa kiasi halisameheki ili arudishwe Simba na kama sikosei yupo hapo tu Rwanda na APR. Timu sasa hivi haina kasi kabisa, wachezaji wazito kukimbia na kufanya maamuzi ya haraka, wachezaji wanakaba kwa macho tu, wacheazji hawana pumzi, timu haina stamina. Sijui viongozi na bodi ya Simba kama wapo makini maana jambo zito kama hili lipo wazi na wameshindwa kuliona basi kuna shida mahali. Na hii timu ilpelekwa nje kwa "per season "na hapa katikati ilipata muda mrefu takribani mwezi mzima wa kufanya mazoezi kwa sababbu hakukuwa na mashindano yoyote.
Jambo ninalojiuliza mpaka sasa hivi Saidoo kampa nini Robertino? Kila mechi ni lazima acheze dakika 90 wakati mara nyingi anapoteza mipira hovyo, analazimisha kupiga chenga wakati uwezo wa kufanya hivyo umepungua kutokana na umri, ana lazimisha kupiga mashuti hata sehemu isiyohitajika kufanya hivyo. Hivi kweli Saidoo ni wa kucheza dakika 90 wakati Miquissone yupo benchi? Ni kweli uwezo wa Miiquissone bado haujafika 100% lakini mimi bado naona ni bora zaidi kuliko Saidoo kwa sababu Miquissone bado anaweza kupunguza wachezaji wawili watatu huku akiitembeza timu kwenda mbele kwa kasi na hata zile "one two"" bado anapiga na zilionekana kule Zambia. Sasa hivi watu wanamlalamikia Chama kuwa hachezi vizuri lakini wanashindwa kuona Chama anacheza na nani pale mbele.
Kwa sasa naona imedhihirika wazi kuwa Robertino ni aina ya makocha ambao wape "average players" wakutengenezee timu. Makocha wa namana hiyo ukiwapa mastaa watupu wanachanganyikiwa kabisa maana hawajui namna ya kuwatumia. Nalisema hili kwa sbabau msimu uliopita Simba ilikuwa na "average players " wengi sana lakini walau ilikuwa inaonekana inacheza vizuri sana kuliko hii Simba ya msimu huu iliyojaa mastaa wapya kibao.
Nini kifanyike?
Simba iachane na Robertino na kocha wa viungo haraka sana. Iwarudishe Mgunda na Adel Zrane. Mgunda achukue timu kwa kipindi hiki cha mpito wakati Simba inatafuta kocha wa kulingana na hadhi yake. Mwisho usahuri wa bure tu golini wamrudishe Ali Salimu kwa sababu kuna makosa ya kiufundi anayafanya Ayoub pamoja na uzoefu wake ambayo Ally Salimu hawezi kuyafanya kabisa. Na ni bahati nzuri tu Morison hayupo kwenye ligi yetu kwa sasa maana angekuwa anamtungu huyo Mwarabu kila mechi. Ila siku na Azam kama ataendelea kufanya hayo makosa basi Dube hata mwacha salama.
Ni mtizamo tu.
Ahsante; nimesharekebisha ubarikiwe sana.Bro AYA ya pili msitari wa 13, ile ni pre-season na sio per season.
Samahani lkn
PoaAhsante; nimesharekebisha ubarikiwe sana.
Hahaaaaaaaaaaaa hahahaha š¤£š¤£š¤£š¤£Hapo alipofikia inatosha, tumeishi maisha ya tabu sana hizi siku za huyu kocha, ni muda sasa Simba irudi kwenye biriani na sambusa, papatu papatu sasa imetosha, wachezaji wetu wanavyo cheza hawana spidi, unaweza kusema ndo wameanza ligi, wazito kweli hata kufanya maamuzi, sasa imetosha, Ahsante Robertinho!