Ni muda wa Simba SC kumchukua kocha Florent Ibenge

AS Vita hakuwahi kuvuka kwenda hatua ya robo fainali CAFCL.

Al Hilal Ormduman pamoja na bajeti kubwa hawajawahi kuvuka kwenda robo fainali msimu wake wa pili huu.

Akiifundisha DRC alikuwa akiishia hatua ya makundi kwenye AFCON licha ya kuwa na vipaji lukuki, wamekuja makocha wengine wamefika kwenye knockouts za qualification ya World Cup. Wamefika Semi final AFCON ndani ya miaka miwili tu wakati yeye kaifundisha DRC kwa miaka mitano.
Kwani makocha ambao wamewahi kuifikisha Simba robo fainali wamewahi kuzivusha timu zingine kufika robo au nusu fainali Ili tujue ubora wao ?
 
Najua amechukua ubingwa wa CAFCC akiwa na RS Berkane na fainali yenyewe alifika baada ya Mazembe kuonewa sana na Referee hapo Morocco.

Akiwa AS Vita alifika fainali ya CAFCC akafungwa na Raja Casablanca.

Hiyo CV ina tofauti gani na ya Benchika ?

Akiwa As Vita alifika fainali kwa kubebwa na kizazi bora sana cha kina Bongonda, Ngoma, Tuisila Kisinda, Jean Mark Makusu, Bangala, Luzolo, Juma Shaban, Moloko na Cesar Manzoki lakini CAFCL akashindwa kupenya robo fainali kwenye kundi ambalo lilikuwa na debutants wawili kwenye michuano.

The guy is somehow overrated.
Wewe sio mtu wa mpira ni mtu wa majungu
 
Kwani makocha ambao wamewahi kuifikisha Simba robo fainali wamewahi kuzivusha timu zingine kufika robo au nusu fainali Ili tujue ubora wao ?
Kipindi hicho Simba alikuwa bado anajitafuta hivyo alikuwa anaajiri makocha kulingana na profile yake.

Sasa hivi siyo timu inayojitafuta tena ni timu inayotaka kombe tuelewe huu utofauti.
 
Duuh, inamana kiufundi we unadhani kwa kinachoendelea simba, tatizo ni ubora wa kocha kuwa chini au ni kikosi kutokuwa imara?
Timu za Ibenge hazichezi kiufundi wowote na hana rest defence timu zake zinafungwa sana kwenye transition.
 
Kama ni kweli kocha Benchika anaondoka mwisho wa msimu, hakuna haja tena ya simba kutafuta kocha kutoka mbali au kocha mwenye rangi nyeupe.

Ibenge ni mmoja kati ya makocha wenye CV kubwa barani Africa, kinachomuongezea faida ni ubora wake katika kuwajua wachezaji na kulijua vyema soka la africa kwa hiyo kama simba sc mmepokea barua ya benchika kutaka kuondoka kubarini na kwa haraka
anzeni mazungumzo na Ibenge na kama mtafanikiwa muombeni aje na baadhi ya wachezaji wazuri.

Mkiukataa ushauri huu na kuwaleta kina cirkovic itakula kwenu tena.
Kigezo ni rangi nyeupe au kigezo ni uwezo?

Simba ina aging players , kama kocha watabadilisha mpaka mwisho wa dunia
 
AS Vita hakuwahi kuvuka kwenda hatua ya robo fainali CAFCL.

Al Hilal Ormduman pamoja na bajeti kubwa hawajawahi kuvuka kwenda robo fainali msimu wake wa pili huu.

Akiifundisha DRC alikuwa akiishia hatua ya makundi kwenye AFCON licha ya kuwa na vipaji lukuki, wamekuja makocha wengine wamefika kwenye knockouts za qualification ya World Cup. Wamefika Semi final AFCON ndani ya miaka miwili tu wakati yeye kaifundisha DRC kwa miaka mitano.
Uko sahihi CV pekee ni kuwapa DRC leopards..CHAN
As Vita Final Cafccl
 
Kama ni kweli kocha Benchika anaondoka mwisho wa msimu, hakuna haja tena ya simba kutafuta kocha kutoka mbali au kocha mwenye rangi nyeupe.

Ibenge ni mmoja kati ya makocha wenye CV kubwa barani Africa, kinachomuongezea faida ni ubora wake katika kuwajua wachezaji na kulijua vyema soka la africa kwa hiyo kama simba sc mmepokea barua ya benchika kutaka kuondoka kubarini na kwa haraka
anzeni mazungumzo na Ibenge na kama mtafanikiwa muombeni aje na baadhi ya wachezaji wazuri.

Mkiukataa ushauri huu na kuwaleta kina cirkovic itakula kwenu tena.
Tatizo usajili ndugu, huyo Ibenge kwa viungo wazito kama wamefungwa vyuma miguuni hatoboi. Washambuliaji wenyewe wako wapi. Timu isajili wachezaji wa maana. Hii Simba hata Gamondi hatoboi
 
Kipindi hicho Simba alikuwa bado anajitafuta hivyo alikuwa anaajiri makocha kulingana na profile yake.

Sasa hivi siyo timu inayojitafuta tena ni timu inayotaka kombe tuelewe huu utofauti.
Nakuomba ujibu swali ?

Kishingo baada ya kuifikisha Simba robo fainali alienda timu kadhaa akazifukisha Hadi nusu fainali au umejifanya kusahau ?

Makocha wote ni Bora.
 
Back
Top Bottom