Ni muda wa Yanga kuibeba Simba kimataifa

Ni muda wa Yanga kuibeba Simba kimataifa

Mkuu, labda umesahau kwamba kuanzia mwezi wa nane Simba anacheza michuano ya Super Cup kwa kupewa tiketi ya kudumu bila kujali imeshuka daraja au imeshika nafasi ya kumi na mbili. Maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa na ujumbe wa CAF ulikuwapo nchini wiki iliyopita kukagua miundombinu, Simba ipo mbioni kuingiziwa mpunga wa maandalizi na hakuna timu nyingine yoyote ya Afrika Mashariki itakayoshiriki zaidi ya Simba.

Michuano hii ni kwa ajili ya timu kubwa tu, na siku chache kabla ya mechi ya Horoya, Try Again alikuwa ana vikao viwili mfululizo, kimoja cha CAF na kingine cha FIFA.

Sasa wewe endelea kupigia hesabu nafasi nne wakati kuna nafasi moja tu ambayo nayo imeshapewa mwenye nguvu
Hii ni hatua kubwa sana kwa Simba na afrika mashariki kiujumla.
 
View attachment 2524707

By De Opera ,

Ni takribani miaka minne, tumeona klabu ya soka ya Simba ikifanya vizuri mashindano ya kimataifa kiasi cha kwamba hadi imesababisha uwepo wa vilabu vinne kushiriki mashindano ya CAF yaani Klabu bingwa barani afrika na Kombe la shirikisho barani Afrika ambapo timu mbili zilishiriki/zimeshiriki kombe la shirikisho na timu mbili kushiriki ligi ya mabingwa.

Tumeshuhudia kiwango cha Simba kinachoishi leo si kile kiwango cha Simba ambacho naweza nikasema kilikuwa ni cha gharama ya kawaida tofauti na sasa ambapo timu inawachezaji wa bei ghali wakati matokeo yakipatikana si ya kuridhisha ama hayaridhishi kabisa.

Simba imekuwa ikisuasua kitendo ambacho kimefanya wapoteze michezo miwili kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika kwenye kundi 'C'.

Sasa tunaona mwenendo ulivo na kuna matumaini madogo sana Simba kuweza kusonga hatua ya robo fainali msimu huu, kwani wanahitaji ushindi wa mechi tatu huku waendelee kumuombea Horoya apate matokeo mabaya katika mechi zake. Ni ngumu kwa aina ya kikosi na mfumo unaotumika kwa sasa.

Sisemi kwamba Simba ndio haiwezi kabisa, la hasha! ni jinsi tu ambavyo naona aina ya wachezaji na mfumo unaotumika simba.

Sasa, kutokana na mwenendo huu kama Simba wasipobadilika naweza kusema msimu huu kwenye CAF ni kwakheri, labda Simba ichukuwe ubingwa wa NBC, kombe shirikisho la Azam, ama Yanga wafanye vizuri zaidi kama tunavyoona sasa Yanga inakikosi kizuri inao uwezo huo. Hii itamfanya Simba ajihakikishie kushiriki klabu bingwa msimu ujao ambapo kule kuna nafasi ukishindwa raundi ya pili basi utaenda kupambania nafasi ya kombe la shirikisho, tofauti na kuanza na kombe la shirikisho ambapo ukifungwa mechi hata raundi ya pili, ni nyumbani kumenoga.

So, bila kuweka jicho la husuda, Simba imekuwa ikiibeba Yanga kimataifa nikimaanisha Ligi ya mabingwa na sasa ni zamu ya Yanga kuibeba Simba kimataifa.
Kwa Taarifa yako Simba ndo ataanza kuingia robo fainali ya champions kabla ya yanga kuingia robo fainali ya loosers. Simba anaanza kwa kumkaanga Vipers nje ndani kisha point tunazichukua kiulaini kwa Horoya, hapo tyr atakua na point 9 utake usitake game ya mwisho na Raja wanaenda kupanda ngamia na kunywa Al kasusu mjaaaaraaabuuu[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Back
Top Bottom