Memtata
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 587
- 1,863
“Dereve taratibu bana usije ukatuua, mi sina mtoto hata mmoja” Msemo kama huu husikika sana katika jamii yetu watu wakimaanisha ni kama mkosi kufariki kabla hujaacha mtoto. Imefikia watu kuona ni bora ufe na kumuacha mwanamke wako mjamzito kuliko kufa hujaacha chochote.
Katika jamii yetu kuna baadhi ya watu huona kama itatokea mpo watu wawili na anatakiwa afe mmoja basi ni bora afe yule ambaye tayari ana mtoto kuliko yule ambaye hajaacha mtoto hii ni tofauti kabisa na wenzetu wenye uelewa zaidi au walio katika nchi zilizoendelea. Wenzetu huona ni bora ufe hujaacha mtoto au mjazimto aliyebeba mtoto wako kuliko kufa na kuacha watoto au mjamzito sababu mwenye jukumu la kutunza familia yako ni wewe zaidi ya utakaowaacha bila kujali mahusiano nao.
Kufa ni mipango ya Mungu (kwa wenye kuamini) lakini tuwe makini jamani tusikomae kupata watoto/kuanzisha familia kwa kuhofia kufa bila kuacha familia. Kama tunataka kuanzisha familia basi tujipange tujue tutaimudu vipi (chakula, afya/matibabu, mavazi, malazi, elimu n.k) yale mambo ya kusema kila mtoto atakuja na riziki yake yamepitwa na wakati tuzae watoto ambao tuna uwezo nao tuwapambanie waishi maisha bora.
Usizae mtoto kwa matarajio ya kuhudumiwa na ndugu au jamaa yako au matarajio yako ukifa wapo watakaomtunza vizuri. Wapo wanaotunzwa vizuri bila wazazi wao lakini hii tuichukulie kama probability. Jukumu la kuitunza familia yako lipe kipaumbele kabla ya kufikiria kuacha mtoto kabla ya kufa.