Ni muhimu kuacha mtoto kabla ya kufa?

Ni muhimu kuacha mtoto kabla ya kufa?

Memtata

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
587
Reaction score
1,863
“Dereve taratibu bana usije ukatuua, mi sina mtoto hata mmoja” Msemo kama huu husikika sana katika jamii yetu watu wakimaanisha ni kama mkosi kufariki kabla hujaacha mtoto. Imefikia watu kuona ni bora ufe na kumuacha mwanamke wako mjamzito kuliko kufa hujaacha chochote.

Katika jamii yetu kuna baadhi ya watu huona kama itatokea mpo watu wawili na anatakiwa afe mmoja basi ni bora afe yule ambaye tayari ana mtoto kuliko yule ambaye hajaacha mtoto hii ni tofauti kabisa na wenzetu wenye uelewa zaidi au walio katika nchi zilizoendelea. Wenzetu huona ni bora ufe hujaacha mtoto au mjazimto aliyebeba mtoto wako kuliko kufa na kuacha watoto au mjamzito sababu mwenye jukumu la kutunza familia yako ni wewe zaidi ya utakaowaacha bila kujali mahusiano nao.

Kufa ni mipango ya Mungu (kwa wenye kuamini) lakini tuwe makini jamani tusikomae kupata watoto/kuanzisha familia kwa kuhofia kufa bila kuacha familia. Kama tunataka kuanzisha familia basi tujipange tujue tutaimudu vipi (chakula, afya/matibabu, mavazi, malazi, elimu n.k) yale mambo ya kusema kila mtoto atakuja na riziki yake yamepitwa na wakati tuzae watoto ambao tuna uwezo nao tuwapambanie waishi maisha bora.

Usizae mtoto kwa matarajio ya kuhudumiwa na ndugu au jamaa yako au matarajio yako ukifa wapo watakaomtunza vizuri. Wapo wanaotunzwa vizuri bila wazazi wao lakini hii tuichukulie kama probability. Jukumu la kuitunza familia yako lipe kipaumbele kabla ya kufikiria kuacha mtoto kabla ya kufa.

aoa300.jpg

 
Kuacha mtoto ndo jukumu namba moja la kiumbe hai chochote kile chenye uhai, ndivyo sayansi ya evolution inavyotufunza. Mafanikio (success) ya kiumbe hupimwa, sio kwa pesa na magari na utajiri, bali kwa uwezo wa kuzaa na kuacha vizazi vilivyo fit.
 
Tatizo ni kwamba watu wanawaza namna ya kupata mtoto bila ya kufikiria maisha baada ya kuwa na mtoto......kwa mtu makini anayewaza mambo kwa kutafakari....kuanzisha familia ni jambo zito sana linalohitaji mawazo na fikra yakinifu.....
 
Post namba 6,8 na 9 wameongea fact .ukileta mambo sijui ya evolution kwa mujibu wa post 7 unataka kumaanisha kwamba hatuna utashi wa kufanya maamuzi which is something totally wrong.huu ulimbukeni uko huku Afrika tu wenzetu wanajua kupangilia maswala ya familia huku tunazaana utadhani buibui.

Hitimisho
Swala la kuwa au kutokuwa na mtoto ni utashi wa mtu binafsi mwenyewe kwakuwa ana free will.
 
Zaeni, acheni principle za ajabu ajabu.. Mtajuta.. Kanumba imemsaidia nini mali bila kuacha mtoto wa kurithi hata kipaji chake?
Lakini sii alikula mbususu ya mrembo yule...inatosha hiyo
 
Umeandika vizuri ila mpangilio wa mawazo ni hovyo kiasi cha kuleta utata au kutoeleweka
 
Kaka naona akili yako imekaa katka unachokisikia na sio unachofikilia or wanachofikilia watu. Yanaonesha unahusudu sana wazungu kulingana na andiko lako.

Lakini fikilia ikiwa yanayoongelewa yangekuwa yanafanyika ni vijana wangapi ambao n above 24 hawana watoto kwamba wao hawajui kunakufa watafute watoto wa kuwaacha kama chapa/alama zao...? Usifatishe sana maneno ya watu ukazan ndo maisha yanavyoenda.
 
Back
Top Bottom