ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
Ilikuwaje mpaka ukakubali kwamba watu tuna mitazamo tofauti, na kwamba hata iweje hatuwezi kufanana mawazo?
Hapa naongelea kujifunza kuheshimu mitazamo ya watu wengine, hasa ile yenye upande chanya na isiyoleta madhara kwa jamii
Kwa mfano, kuna mtu anaamini Mungu yupo, na mwingine anaamini hayupo
Huo ni mtazamo wake binafsi
Kuamini kwake hakupunguzii kitu wewe unayeamini, wala hakumuongezei kitu asiyeamini
Vivyo hivyo kwa mtu anayesema yeye ni team kataa ndoa
Huo pia ni mtazamo wake binafsi
Aoe au asiolewe, hilo haliathiri maisha yako moja kwa moja
Hii naweza kuiita mitazamo chanya, kwa sababu haina madhara kwa watu wengine
Lakini pia kuna mitazamo hasi ambayo watu wengi waliostaarabika wanaweza kuipinga kwa sababu inaweza kuharibu jamii Kuna baadhi ya mawazo ambayo, hata kama watu wamekubaliana wenyewe, bado yanaweza kuleta madhara kwa jamii ikiwa hayatakemewa
Mitazamo ya aina hiyo ndiyo mara nyingi huzua mjadala mkubwa kwa sababu athari zake zinaonekana zaidi kwenye maadili na malezi ya jamii
Leo nazungumzia zaidi ile mitazamo ambayo, hata mtu akiwa nayo, haimdhuru mwingine
Kwa hiyo hakuna haja ya kuchukiana au kulalamika sana kwa sababu tu mtu ameamua kuamini au kuishi tofauti na wewe
Mimi zamani, sijui ilikuwa ni utoto au uelewa mdogo nilikuwa naamini kwamba kila ninachoamini mimi basi na wengine wanapaswa kuamini hivyo hivyo😅
Kama sipendi kitu fulani nilitaka hata mtu niliye karibu naye asikipende
Lakini baadaye niligundua kwamba hilo haliwezekani
Kwenye maisha tunakutana na watu waliokulia mazingira tofauti, tamaduni tofauti, na malezi tofauti
Kwa hiyo ni kawaida kabisa watu kuwa na mitazamo tofauti
Baada ya muda nikajifunza kwamba sina uwezo wa kubadilisha kila mtu ili awe kama mimi
Badala yake, ni bora kutafuta watu ambao tunaendana kitabia na kimawazo kuliko kutumia nguvu nyingi kuwalazimisha watu wabadilike wawe kama mimi
Maana mwisho wake unaweza kujikuta unaishi kwa hasira, chuki, na maumivu kwa sababu watu hawajawa vile ulivyotaka wawe.
Nilijifunza toka udogoni ila iliniingia kikweli kweli in my 20's baada ya maisha na kazi kunifanya nichangamane na watu wa aina mbalimbali. Sasa hivi sibugudhiwi kabisa na mawazo na mitazamo ya watu, hata kama sikubaliani nayo.Je, wewe ilikuchukua muda gani kujifunza kuheshimu mawazo na mitazamo ya watu wengine, bila kuwaona hawana akili, bali kwa kutambua tu kwamba binadamu hatufanani?
ShesRise_1 🖐
Hongera dear 😍View attachment 3593224
Nilijifunza toka udogoni ila iliniingia kikweli kweli in my 20's baada ya maisha na kazi kunifanya nichangamane na watu wa aina mbalimbali. Sasa hivi sibugudhiwi kabisa na mawazo na mitazamo ya watu, hata kama sikubaliani nayo.
Hii ni tofauti dear mitazamo ya CCM ni ya kuliangamiza taifa watu wote wastarabu hawakubaliana nao na wanapinga kwa nguvu zote sela za CCM kwa sababu zinaumizaMimi Abigail Bado
Itanichukiaua muda sana kuamini wanasisiemu ni watu wenye akili timamu na kuheshimu mitazamo Yao.
Kama wasivyoheshimu yangu,na mie siheshimu Yao.
kuheshimu mawazo na mitazamo ya watu wengine, bila kuwaona hawana akili, bali kwa kutambua tu kwamba binadamu hatufanani?
Hapana bhna mtu akisema hataki ndoa wewe unapata madhara gani?Sio rahisi hivyo kabisa. Unachokiona hakina madhara kuna wengi wanaona kinacho.
Lazima tugombane, ni sehemu ya maisha.
Hivi unajua utanifanya nikupende,haya ndio mambo yanguIlikuwaje mpaka ukakubali kwamba watu tuna mitazamo tofauti, na kwamba hata iweje hatuwezi kufanana mawazo?
Hapa naongelea kujifunza kuheshimu mitazamo ya watu wengine, hasa ile yenye upande chanya na isiyoleta madhara kwa jamii
Kwa mfano, kuna mtu anaamini Mungu yupo, na mwingine anaamini hayupo
Huo ni mtazamo wake binafsi
Kuamini kwake hakupunguzii kitu wewe unayeamini, wala hakumuongezei kitu asiyeamini
Vivyo hivyo kwa mtu anayesema yeye ni team kataa ndoa
Huo pia ni mtazamo wake binafsi
Aoe au asiolewe, hilo haliathiri maisha yako moja kwa moja
Hii naweza kuiita mitazamo chanya, kwa sababu haina madhara kwa watu wengine
Lakini pia kuna mitazamo hasi ambayo watu wengi waliostaarabika wanaweza kuipinga kwa sababu inaweza kuharibu jamii Kuna baadhi ya mawazo ambayo, hata kama watu wamekubaliana wenyewe, bado yanaweza kuleta madhara kwa jamii ikiwa hayatakemewa
Mitazamo ya aina hiyo ndiyo mara nyingi huzua mjadala mkubwa kwa sababu athari zake zinaonekana zaidi kwenye maadili na malezi ya jamii
Leo nazungumzia zaidi ile mitazamo ambayo, hata mtu akiwa nayo, haimdhuru mwingine
Kwa hiyo hakuna haja ya kuchukiana au kulalamika sana kwa sababu tu mtu ameamua kuamini au kuishi tofauti na wewe
Mimi zamani, sijui ilikuwa ni utoto au uelewa mdogo nilikuwa naamini kwamba kila ninachoamini mimi basi na wengine wanapaswa kuamini hivyo hivyo😅
Kama sipendi kitu fulani nilitaka hata mtu niliye karibu naye asikipende
Lakini baadaye niligundua kwamba hilo haliwezekani
Kwenye maisha tunakutana na watu waliokulia mazingira tofauti, tamaduni tofauti, na malezi tofauti
Kwa hiyo ni kawaida kabisa watu kuwa na mitazamo tofauti
Baada ya muda nikajifunza kwamba sina uwezo wa kubadilisha kila mtu ili awe kama mimi
Badala yake, ni bora kutafuta watu ambao tunaendana kitabia na kimawazo kuliko kutumia nguvu nyingi kuwalazimisha watu wabadilike wawe kama mimi
Maana mwisho wake unaweza kujikuta unaishi kwa hasira, chuki, na maumivu kwa sababu watu hawajawa vile ulivyotaka wawe
Je, wewe ilikuchukua muda gani kujifunza kuheshimu mawazo na mitazamo ya watu wengine, bila kuwaona hawana akili, bali kwa kutambua tu kwamba binadamu hatufanani?
ShesRise_1 🖐
Mlipishana mitazamo na vipaumbele aliwaza ndoa zaidi na wewe uliwaza ustawi before ndoaKuna binti nilimpenda kisawasawa wakati huo nilikua sina mbele wala nyuma napiga kibarua kiwanda fulani ...tulielewana sana baadae napata fursa maisha yanabadilika ...nikamtafutia kazi sehemu kafanya siku mbili kaacha ......then analazimisha mipango ya mahusiano na ndoa ilihali mipango yangu kwake anaivuruga...mahusiano yalifika tamati nikakubali hata kama miminaliona njia nuri ya kumsaidia kwake haikuwa nzuri tuliachana
Kutoyaheshimu na kisha kuyapuuza bila kuonyesha chuki safiii👏Hata huku JF kuna watu wana mitazamo na mawazo ya kipuuzi ,Hilo tulitambue. 😂😂😂😂
Na sio kwamb tunayaheshimu. Ila tunayapuuza.
Kwahiyo mpka sasa hunipendi🤔Hivi unajua utanifanya nikupende,haya ndio mambo yangu
Nakupenda 🤣🤣Kwahiyo mpka sasa hunipendi🤔
Asante kwa ufafanuzi kakaBinadamu duniani wamegawanyika makundi makubwa mawili, Conservatives na Liberals.
Liberals kwa kiasi kikubwa wanatambua na kuheshimu uhuru wa watu wengine katika mitazamo na machaguo yao binafsi, Conservatives wao wanaamini binadamu wote wanatakiwa kuwa na mawazo ya aina moja na wako hawana uvumilivu kabisa na mawazo tofauti.
Safiii 👍Nakupenda 🤣🤣
Yaani ulikua ujinga mkubwa kujipa umuhimu 🤣🤣Mimi zamani, sijui ilikuwa ni utoto au uelewa mdogo nilikuwa naamini kwamba kila ninachoamini mimi basi na wengine wanapaswa kuamini hivyo hivyo😅
Hapa ulijikuta wewe ni nabii au mtume hahah