Ni muhimu kwa viongozi wetu wa kisiasa kuchagua maneno sahihi ya kujibu hoja za wananchi

Ni muhimu kwa viongozi wetu wa kisiasa kuchagua maneno sahihi ya kujibu hoja za wananchi

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
501
Reaction score
1,214
Nakumbuka awamu ya tatu wakati serikali ikitaka kununua ndege ya Rais aina ya Gulfstream G550 kwa thamani ya bilioni 46

Watanzania walio wengi, walionyesha kupinga hatua hiyo, kwa kuzingatia hali ya uchumi ya nchi yetu kwa wakati huo

Lakini, aliyekuwa waziri wa fedha wa wakati huo, mzee Basil Pesambili Mramba, alikuja na kauli ya kusema, hata kama watanzania watakula majani, lakini ndege ni lazima inunuliwe , na kweli ndege ikanunuliwa

Lakini baada ya hapo, maisha ya kisiasa ya mzee Mramba, wote tuliona kilichofuata

Ni muhimu sana kwa viongozi wa kisiasa, kuwa makini sana kwenye aina ya maneno tunayotumia kujibu hoja zinazogusa maisha ya watanzania, hasa watanzania wa kipato cha chini

Kama hili la mheshimiwa waziri wetu wa fedha, kujibu wananchi wasiopendezwa na tozo hizi za mihamala ya simu kuhamia nchi jirani, si sawa kabisa

Kwa nafasi yake kama waziri, alipaswa kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa tozo hiyo

Uongozi ni dhamana
 
Kauli ya ukosefu wa utu kabisa toka mwigulu
 
Back
Top Bottom