Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,042
- 17,320
Ukiongelea taaluma ya Computer LAZIMA ujue kuandika lugha ya Computer (coding). Hiki chuo cha UDSM nina wasiwasi kila kitu wanafundisha nadharia tu (theory) hata katika taalum ambazo tunategenea wahitimu wawe wameiva kivitendo. Taaluma za uhandisi (engineering) wanaweza kujificha katika kivuli cha taasisi wanazofanyakazi kiasi kwamba wanaweza kuwa wanabebwa kwavile wanakuta taasisi au kampuni tayari imesimama inafanyakazi na wao tiamajitiamaji wanaibia na kukalili na mwisho wa siku wanajimwambafai. Sasa katika tasinia ya computer huwezi kudanganya. Sasa naomba (KWA USHAHIDI), muhitimu yupi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kahitimu anajua kuandika lugha ya computer (coding) na aje hapa na ushahidi wa kazi alizozifanya na jinsi ambavyo jamii tunajua na anaishi kwa taaluma hiyo. Mimi wengi ninaowajua kwenye coding wamejifunzia nje ya Tanzania. Nasema hivyo, tusijekuwa tunapeleka vijana wetu tukidhani watasaidika kumbe wanaenda kulishwa theories na mwisho wa siku wanaishia mtaani kama taaluma nyingine za Art! Kama kuna wataaluma wa UDSM ebu njoo mtuambie pia!