Ni mwaka wa 6 sasa sijapata ajira ya ualimu TAMISEMI

Sio kwamba sijichanganyi, ningekuwa sijichanganyi ningeishije sasa hapa naongelea ajira , sio kwamba nipo jobless ila nataka ajira ya serikali
Ajira Serikalini si umesikia Waziri wa TAMISEMI amesema wataajiriwa wenye maksi za juu,wanaangalia ufaulu kwanza,kwa hiyo jiangalie GPA yako
 
Ajira zinaweza kutoka na ukaajiriwa lakini usipate kile unachokifikiria kukipata. Mfano rahis sana ni huu. Kwa sasa uko maskani Dar, ajira zinatoka ukawa umepangiwa shule moja huko ndani ndani mkoa wa ruvuma, maeneo ya Nyasa, ni mbali na kijijini balaaa. Unafika huko unakutana na life iliyopinda balaa, hakuna life state ya kuweza kukufanya ukaenjoy, mshahara wote ukajikuta unaishia kutatua changamoto katika mazingira yako mabovu ya kuishi huko.

Anza kufikiri tofauti kidogo.
 
m
Hawa vijana wa ualimu ni kama wajinga fulani hivi.
Siku moja serikali iliposema patakuwa na usaili kwa kada ya ualimu walilalamika kana kwamba serikali imedhamiria kuajiri kada zingine ili wawe walimu.
Mjinga mwenyewe mpuuzi kama walimu ni wajinga basi utoe hoja course ya ualimu ifutwe ili watoto wenu muwafundishe wenyewe nyumbani

mjinga sana wewe
 
Nacheka kama mazuri. Watu wapo wa 2013 maticha na hawana mishe kitaa! Jiongezeni madogo mtazeeka hamna ajira.
 
Pole sana,ungekuwa unajitolea labda ungepata kipaombele ila jaribu zitakazotoka next July.

Mungeanzisha platform na movement yenu Ili mjisajili harafu idadi yenu ikijulikana mkamuone Waziri wa Tamisemi,Elimu, Utumishi na Waziri Mkuu mfanye kikao bila shaka wataanza kuwapa kazi kadiri ya nafasi Hadi mumalizike.

Kwa Hali ilivyo Sasa hawana data base
 
Mkuu miaka 7 kitaa na bado una hamu na ajira? Tena za uwalimu? Aisee
Huyo elimu haijamsaidia kitu mimi naona...tuseme ndo hana kabisa hata kipaji au nguvu ya kufanya kazi zingine au hayo maarifa aliyopata huko chuoni hawezi kabisa kuyatumia kufanya mitikasi mingine ya kimaisha anakaa kusubiria ajira za mpaka watu wajisikie kutoa mkeka tena ambao tayari una watu wa connections!
 
Kuna jamaa zangu wa 2015 mpaka leo bilabila da ajira hizi E MUNGU ingilia kati
 
bahati mbaya ajira sio hisani..
 
Mwalimu samahani lakini ni graduates sio graduators
 
Sababu za kukosa ajira:
1. Inafahamika mlibebwa matokeo ya O-level.
2. Inafahamika matokeo ya A level mlibebwa.
3. Ina fahamika matokeo ya Chuo mna low class kwenye digrii na wengine mpaka wana graduate hawajui kuandika barua ya ajira, ni kama mnakwepwa ili kije kizazi kingine ambacho kweli hawajabebbwa.
Kumbuka ninyi ndio wale mlifaulu wote lasaba, form two mkapita wote form four na siix the same na mitihani yenu majibu ni ya kuchagua.

USHAURI KWA SERIKALI: Iendelee kuwatumia kwenye sensa na kusimamia uchaguzi na nyie mjiajiri kwenye UMACHINGA, kuna masoko mengi ya kisasa yanajengwa, nendeni humo msitake white collar job.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…