Pole Sana inaonekana umelishwa propaganda mpaka uwezo wa kufikiri umepungua.... Haya tukubali tuliwavamia Uganda halafu??? Tukaikalia Kama unavodai tumeikalia Zanzibar!!???
Je tulivoipiga Uganda Muungano...
Labda tu nikuongezee Tanzania ilikuwa kitovu cha Pan Africanism.. Tumesaidia Nchi nyingi zilizoomba msaada kupambana na wakoloni. Nchi Kama Zimbabwe, Angola, Msumbiji, Sahara Magharibi, Palestina, Afrika Kusini na Nchi nyingine nyingi..
Bahati mbaya Sana Zanzibar mliomba tuungane na sio msaada ktk mapambano.. wenzenu wenye akili waliomba msaada ktk medani lakini nyinyi hamkutaka kuingia kwenye medani ya Vita mkaomba kufunikwa na koti la Tanganyika. Nchi yenye takriban kilomita mraba laki Moja wakati nyie Ni 2500 tu.
Pole sana