Ni nani aliyeharibu Mchakato wa Katiba Mpya? Tuanzie hapo

Ni nani aliyeharibu Mchakato wa Katiba Mpya? Tuanzie hapo

Mnakuja msumbua mama bure. Mchakato wa Katiba ilikuaje ukasitishwa? Ni nani alifanya uharibifu ule wa pesa?

Je Rais aliyepo Madarakani alihusikaje katika mchakato wa Katiba?

Mnataka mchakato uendelee kuanzia wapi?

Kama kuna aliyeharibu mchakato achukuliwe hatua gani?

Vipi Raisi aliyeko madarakani akisema hakuna pesa za kulipa wabunge wa bunge la katiba. Kutakuwa na option gani?
Kha! Kwahio nani aliyeharibu? Mbona umeuliza swali very genuine halafu umeishia kuongea ugoro?
Hakuna aliyeharibu, ila kuna watu wawili walioliokoa Taifa hili kuangamia baada ya wasaliti kujipanga vizuri kutuvuruga. Wa kwanza ni huyo mtoto wa Msoga, Mkoa wa Pwani. It was a clasic:

Kulikuwa na mambo mengi Sana yaliyopekea mchakato wa Katiba mpya kukwama, yote Yale yaliangukia kwenye makundi 4 yafuatayo;
1.MAMLAKA NA MUUNDO WA BUNGE LA KATIBA.
Kimsingi kambi 2 kuu hazikukubaliana juu ya Mamlaka na Majukumu ya BUNGE la KATIBA kisheria. UKAWA waliamini RASIMU ya Warioba ndio Katiba na kwamba BUNGE halina mamlaka ya kubadili, kuongeza au kufuta kipengele chochote zaidi ya kuboresha. Upande wa Pili CCM waliamini BUNGE la KATIBA ndio linaandika Katiba na Lina mamlaka kamili na kwamba Rasimu ya Warioba Ni Muswada tu ambao wao Wana haki ya kuuweka itavowapendeza.
Kwenye suala la MUUNDO watu wa ukawa hawakujua athari ya MUUNDO. Kwamba BUNGE lililopo Ni sehemu ya BUNGE la KATIBA. Wakati ule BUNGE lilikuwa na zaidi ya 70% Toka CCM.. Tafsiri yake Ni kwamba KATIBA itakayotungwa lazima iridhiwe na CCM maana ndio wengi. Na hii NDIO DEMOKRASIA

2. MCHAKATO WA KIDEMOKRASIA
Mwisho wa siku mchakato wote Ni Democratic, kwa maana kwamba vipengele vyote vitapigiwa Kura ili kwamba matakwa ya wengi yazigatiwe huku wachache wakiachwa wazungumze wamwage nyongo tu ( Naamini haimaanishi wasikilizwe kwa sababu uchache wao unaponza hoja zao zitupwe likija suala la kupiga kura).

3. UMILIKI WA MCHAKATO.
Kuna watu walipigania kuwepo Katiba mpya,na ilipokuja... walijua imekuja kwa ajili yao na kwamba hoja zao lazima zisikilizwe bila kujua it's Democratic process na kwamba mwenye majority ndio ataamua CONTENT ya KATIBA.. UKAWA walifadhaika baada ya kuona watu wengine ambao Wala hawakuwa wanataka Katiba ndio wanakuwa na sauti na maamuzi nini na nini kiwemo au kisiwemo kwa kutumia wingi wao.

4. UKAWA WALISUSA. Walijiona wanawakilisha matakwa ya WANANCHI waliamini mchakato wanaumiliki, ni Mali yao.. lakini hakuna ambacho waliweza kukipitisha ambacho CCM hawajakiridhia, kinyume chake CCM walipitisha agenda zao wapendavyo . Msingi wa kususa Ni kuonyesha Katiba ilikosa political legitimacy. Japo CCM waliendelea na kukamilisha kazi ya BUNGE, lakini hawakuipeleka hatua ya pili, KUPIGIWA KURA NA WANANCHI. Nafikiri walifanya makusudi, hawakuogopa, hawakuona aibu. WALISITISHA MCHAKATO MAKUSUDI, kulinda maslahi yao.
Ukweli Ni kwamba japo content waliamua wenyewe lakini yalikuwepo mambo kadhaa ambayo waliridhia kwa aibu na kwa shingo upande, hususan TUME HURU na mengiyo. Kwa hiyo walisitisha mchakato na kuturudisha pale tulipokuwa kwa kisingizio Cha wenzetu wamesusa. Naamini wangeamua kwenda kwenye REFERENDUM wangeshinda kwa sababu bado Wana MAJORITY kwa wapiga kura wengi huko uraiani, kinyume na tunavojdanganya humu JF na kule Twitter.. Maamuzi Yale yaliwasaidia Sana ndio maana leo wana Halmashauri zote na Wabunge wote (98%)

WAY FORWARD..
Leo tunadai upya mchakato sijui Katiba, labda tujiulize maswali machache
1. Nani atatunga KATIBA, ni BUNGE au Ni ile RASIMU ya Tume ya Warioba ndio katiba na BUNGE linaipigia kura tu!?
2. Je BUNGE Lina MUUNDO gani balance ikoje!? Kama kipindi kile CCM walikuwa 70%... leo hii CCM Wana MAJORITY ya 98% ya Wabunge was majimbo UKAWA wataendelea kusubiri huruma ya CCM Tena.!? Au mbinu gani itatumika!?
3. Japo UKAWA wanajinasibu kubeba agenda za wananchi na kujiona wanaumiliki mchakato lakini urari uliopo ni wazi demokrasia inawapendelea CCM kuanzia BUNGE la KATIBA mpaka KURA ya MAONI. Chama Cha Mapinduzi Wana Rasilimali na Wingi wa kutosha kumiliki na kudhibiti mchakato..
Je Kuna mbinu gani mbadala ku offset huu urari na ushawishi wa CCM ambayo pia Wana DOLA..!??
Je viongozi wa vuguvugu la kudai Katiba hawaoni changamoto hii au wanaleta UJONGOO kwamba hawajui Kama wamepotea mpaka wagonge ukuta ndio waanze kupapasa njia upya!?

Kifupi hakuna asiyejua majibu ya maswali haya...
Tunasubiri kuona mkakati wao au ndio ndio lengo lao Ni hizo hela na political platform tuwaone wanavobwabwaja!?

My Take.
The art of negotiation inataka balance of power or votes. Ngazi ya BUNGE inahitajika ⅔ ya Majority, tusubiri hiyo au tupokee tutakachopewa na CCM wenye majority.
Kinyume chake tuache kulishana matango pori, muda wa kutengeneza Katiba NZURI bado japo TUNAWEZA kutengeneza KATIBA MPYA. Hata jirani zetu Kenya wakati wanaingia kutengeneza Katiba mpya hakuna kundi lililokuwa na zaidi ya 66% majority sio ORANGE wala BANANA MOVEMENT
 
Wapinzani
Mnakuja msumbua mama bure. Mchakato wa Katiba ilikuaje ukasitishwa? Ni nani alifanya uharibifu ule wa pesa?

Je Rais aliyepo Madarakani alihusikaje katika mchakato wa Katiba?

Mnataka mchakato uendelee kuanzia wapi?

Kama kuna aliyeharibu mchakato achukuliwe hatua gani?

Vipi Raisi aliyeko madarakani akisema hakuna pesa za kulipa wabunge wa bunge la katiba. Kutakuwa na option gani?
 
Nakuuliza maswali ya kilogic basi Sawa mie katiba ya zamani siifahamu na watz wengine wengi hawaijui, tufanye wanaijua wanaccm wenye madaraka na lissu pekee. Haya swali la kilogic kuna ubaya gani kuipatia nchi katiba bora hata kama raia 99% haiwafahamu ile mbovu ya zamani? Au swali jingine la kilogic wewe kama mzazi kipi ni bora kuipelekea familia yako samaki au Joka hata kama familia ilikuwa haijaomba samaki?
Kweli wewe Ni shida, hivi unafikiri hiyo KATIBA ni ya nani na ni nani anaitunga na Nani anaipigia kura na kuipitisha au kuikataa!!??
Mambo yote haya yanataka majority na uelewa sio logic.
Logic ilitumiwa na TUME tu ambao hawakuwahi kupiga kura kwenye kuandaa rasimu Bali walikuwa Wana exhaust hoja badala ya kura.
Kama wapiga kura hawaelewi basi watapiga kura kwa mkumbu wa vyama vyao, nguvu ya majority. Tukifika huko hakuna Tena fursa ya kupata KATIBA Bora.
 
Mnakuja msumbua mama bure. Mchakato wa Katiba ilikuaje ukasitishwa? Ni nani alifanya uharibifu ule wa pesa?

Je Rais aliyepo Madarakani alihusikaje katika mchakato wa Katiba?

Mnataka mchakato uendelee kuanzia wapi?

Kama kuna aliyeharibu mchakato achukuliwe hatua gani?

Vipi Raisi aliyeko madarakani akisema hakuna pesa za kulipa wabunge wa bunge la katiba. Kutakuwa na option gani?
Alianza Kikwete ,Magu akamalizia
 
Mchakato wa katiba uliharibiwa na wanasiasa wajinga waliotaka kupenyeza agenda zao ili waingie ikulu kirahisi matokeo yake yakaibuka malumbano na mwisho wa siku wenye mamlaka wakaamua wauzike tu...

Hata hawa wapiga kelele za katiba mpya ukiwauliza agenda zao utaona ni zilezile za maslahi ya kisiasa ili wapate urahisi wa kuingia madarakani lakini ukiwauliza hoja za msingi zenye manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi hawana...

Ukiwauliza ni lini mmeitisha maandamo ya watu kupewa elimu bure na bora, huduma za afya bure, fao la kujitoa, kuboreshwa kwa pension za wazee wetu nk nk...
Lini mliitosha maandamano? Katika awamu ya tano...? Mungu aturehemu Watanzania aliyeturoga Mungu amlipe tu sawa na ushenzi wake wa kutuibia akili kiasi hili?
 
ulijuaje kama nchi inahitaji katiba mpya?..
Je katiba iliyopo inatekelezwa kwa asilimia ngapi?
Katiba iliyopo haitekelezwi kwa sababu katiba hii unatoa mianya ya watu kutoifuata. Kwa hiyo tunataka katiba inayotekelezeka
 
Waliharibu wapinzani UKAWA kwa vile walitaka serikali 3 badala ya 2 na hivyo kususa kikao kama njia ya kushinikiza. Hapo ndipo walipofanya kosa la kiufundi kubwa. Laiti wangekubali kwenda by peace meal wakaanza na madaraka ya Rais, Tume ya uchaguzi, upatikanaji wa wabunge, mgombea binafsi, nk wakaruka maeneo magumu halafu 5 years later wakayarudia kwa agenda mpya. Pushing by bits. Wangefanikiwa sasa hivi tungekuwa mbali sana. Hii ndiyo mbinu ya majadiliano magumu. You dont push for everything rather moving strategically in win win situation.
Wananchi wengi walitaka serikali tatu, hata leo ukipita utaona wengi wanataka serikali tatu. Kwa Nini hili ccm walilikataaa? Walikataa maoni ya Wananchi.
 
UKAWA unawasingizia. Wao waliunda UKAWA baada ya kuona yale maoni ya wananchi kwenye rasimu ya pili ya tume yametupwa yote, instead CCM wamekuja na kitu kipya kabisa ambacho kilikuwa hakibebi maoni ya wananchi. Rejea upya chanzo cha ukawa
Watanzania wengi ni wavivu, kipindi like nilikuwa kijana mdogo lakini nakumbuka kila kitu, sasa hawa watu wazima washasahau kila kitu
 
Mchakato uliharibiwa na wananchi. Kivipi? Walirudi mstari wa nyuma wakiwaachia wanasiasa wajinafasi mstari wa mbele!
Na inavyoonekana hata huu wa sasa wananchi washaanza kuuharibu!!
 
Wananchi wengi walitaka serikali tatu, hata leo ukipita utaona wengi wanataka serikali tatu. Kwa Nini hili ccm walilikataaa? Walikataa maoni ya Wananchi.
Bajeti ya kuiendesha ccm asilimia kubwa inatokana na gawio la serikali ya Tanganyika (am)
 
Kweli wewe Ni shida, hivi unafikiri hiyo KATIBA ni ya nani na ni nani anaitunga na Nani anaipigia kura na kuipitisha au kuikataa!!??
Mambo yote haya yanataka majority na uelewa sio logic.
Logic ilitumiwa na TUME tu ambao hawakuwahi kupiga kura kwenye kuandaa rasimu Bali walikuwa Wana exhaust hoja badala ya kura.
Kama wapiga kura hawaelewi basi watapiga kura kwa mkumbu wa vyama vyao, nguvu ya majority. Tukifika huko hakuna Tena fursa ya kupata KATIBA Bora.
Mimi tena nimekuwa shida? Kwa hiyo sehemu ilipokwamia rasimu ya warioba ni kwa Sababu majority waligoma kupiga kura au? Hebu nifafanulie basi nielewe ni nani anatunga? Na nani anaipitisha? Na je ni kipi kilikwamisha kati ya anayeitunga na anayeipitisha na ueleze kwanini ilikwama?
 
Katiba iliyopo haitekelezwi kwa sababu katiba hii unatoa mianya ya watu kutoifuata. Kwa hiyo tunataka katiba inayotekelezeka
Weka hapa kipengele kimoja tu ambacho kinatoa mwanya wa kutotekelezeka kwa KATIBA yenyewe
 
Wananchi wengi walitaka serikali tatu, hata leo ukipita utaona wengi wanataka serikali tatu. Kwa Nini hili ccm walilikataaa? Walikataa maoni ya Wananchi.
Kwani sheria inasemaje juu ya Mamlaka WANANCHI kwa bunge la kutunga sheria!?
Tambua kwamba ktk mchakato kila chombo kina miiko na majukumu yake na yasiingiliwe.
Majukumu ya WANANCHI yapo ktk hatua 2 muhimu.
1. Kutoa maoni mbele ya TUME. Wakitoa maoni kazi yao imekwisha mchakato utaendelea ktk hatua zingine.
2. Kupiga kura ya kukubali au kukataa Katiba iliyoandikwa na BUNGE LA KATIBA.

Mwenye mamlaka ya kuhoji kazi ya BUNGE LA KATIBA ni Wananchi kupitia REFERENDUM.
Kabla ya referendum, bunge linahaki ya kufanya chochote na Rasimu ilimuradi hawavunji sheria ya kutunga Katiba.
 
Na
Katiba mpya ianishe,mgawanyo wa madaraka,iwe kwa zamu,bara na visiwani,,vyeo vigawanwaje,,sio mtu anapata madaraka anaanza kubuni mbinu za kutawala milele.
Eti visingizio,utamaduni wa kutawala kwa zamu si lazima,,
Lazima ianishwe na iwe lazima,Rais yeyote asiweze kutengua hicho kifungu
Wewe nae unakusanya maoni mpya au!? Na Mimi nitoe ya kwangu!?
 
Mnakuja msumbua mama bure. Mchakato wa Katiba ilikuaje ukasitishwa? Ni nani alifanya uharibifu ule wa pesa?

Je Rais aliyepo Madarakani alihusikaje katika mchakato wa Katiba?

Mnataka mchakato uendelee kuanzia wapi?

Kama kuna aliyeharibu mchakato achukuliwe hatua gani?

Vipi Raisi aliyeko madarakani akisema hakuna pesa za kulipa wabunge wa bunge la katiba. Kutakuwa na option gani?
Aseme zinahitajika sh. ngapi? Ila lisiwe bunge la Ccm tafadhali.
 
Tatizo Hakuna muungano, ni uvamizi uliopewa Jina la muungano
Nani alimvamia mwenzie na kwa silaha gani!?
Shida hapa Ni Karume na Mapinduzi yake alitofanya mwaka ule.
Alijua fika kwamba waarabu aliowapindua Wana pacha wao kule Oman na kwamba wanajipanga kuja kukomboa colony lao. Na watakaporudi hatowamudu. Ndipo akaamua kuungana na Tanganyika ili wale jamaa wa Oman wasije maana itabidi wajipange kupigana jamhuri ya Muungano.
Sasa leo kitisho Cha wa Oman kimeisha wanataka kujitoa kwenye Muungano. Wanafikiri eti Muungano Ni sawa na koti, ukisikia baridi unavaa ukisikia joto unavua.
Mimi nadhan Muungano sio koti Bali Ni NGOZI ktk mwili.
USA Ni Muungano wa mataifa 52... leo Ni uhaini kufikiria kuvunja ule muunga kwa mujibu wa sheria na Katiba yao.
 
Boss unapaswa kuwa objective wakati fulani bila kujali mtazamo wako kisiasa. Aliyeharibu mchakato wa Katiba ni CCM! Hiyo ni fact. walikataa kutimiza maoni ya Tume ya Warioba kwa sababu ya baadhi ya vipengele havikuwa vizuri kwao kama vile kuwa na serikali tatu. Yote yaliyotokea ilikuwa ni kwa sababu CCM walitaka kutupa katiba isiyo na tofauti kubwa na sasa! Mama Samia ni CCM Member kwa hiyo an wajibu katika hili.
 
Back
Top Bottom