Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Zikiwa zimebakia siku tano kabla ya uchaguzi mkuu, Mkuu wa kanisa la Evengelism Assemblies of God, Tanzania, (EAGT), Askofu Moses Kulola, amerudia tena ule wito wake wa kukemea siasa za udini zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa dini nchini, kuchanganya dini na siasa na kusisitiza kufanya hivyo, ni dhambi kwa mujibu wa maandiko matakatifu ya Bibilia.

Askofu Kulola, ameyasema hayo jana, katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii yalifanyika kwa njia ya mtandao wa video mwandishi akiwa Dar es Salaam na Askofu akiwa mjini Mwanza ambako kanisa lake, linafanya maombi maalum ya kuombea amani kwenye uchaguzi mkuu yaliyofanyikia viwanja vya Misungwi mjini Mwanza

Huku akinukuu vifungu vya Bibilia, Askofu Kulola amesema Bwana wetu Yesu Kristo aliwasisitizia Wakristu kumpa Mungu yaliyo ya Kimungu na kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari, hivyo kuchanganya dini na siasa, ni sawasawa na kumpa Mungu ya Kaisari na kumpa Kaisari yaliyo ya Kimungu.

Pia Askofu huyo amekemea vikali harakati za chini chini zinazotaka kuwagawa Watanzania katika misingi ya kidini na kuwataka viongozi wa dini, wawahimize waumini wao kujitokeza kwa vingi, kwenda kupiga kura, na wawe huru kumchagua kiongozi yoyote wanayempenda bila kufuata misingi ya kidini.

Askofu Kulola, amelaani kitendo cha mmoja wa maaskofu wa kanisa lake, kuandika waraka kwa kuwataka waumini wao, wasimpigie kura mgombea fulani wa urais ambaye ni Mwislamu, na kuwataka waumini hao wampigie kura mgombea fulani ambae ni Mkristu. Amesema waraka huoni wa uchochezi na askofu huyo alistahili kuchukuliwa hatua za kisheria.


Amesisitiza Watanzania kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo, kwa kusimamia misingi ya umoja, amani na utulivu aliyotuachia ambapo dini ya mtu sio miongoni mwa sifa za uongozi, hivyo kuwasisitizia watanzania wachague viongozi kwa sifa za uongozi na sio kwa dini za wagombea.

Ametolea mfano toka kwenye Biblia Takatifu kuhusu Mfalme Nebukadreza ambaye hakumwamini Mungu, lakini bado alimfanya kuwa Mfalme wa taifa la Mungu la
Waisraeli, hivyo kiongozi yoyote wa kisiasa atakayechaguliwa bila kujali dini yake, yeye ndiye atakuwa chaguo la Mungu.

Ametolea mfano Nyerere alikuwa Mkristo lakini alikuwa akichaguliwa na kura za wote, Waislamu na Wakristo, vivyo hivyo alipokuja rais Mwinyi, alichaguliwa na Wakristo na Waislamu, vivyo hivyo Mkapa ni Mkristo na alichaguliwa kwa kura za Waislamu na Wakristu halikadhalika Rais Kikwete, awamu yake ya kwanza alipata ushindi wa kishindo kwa kuchaguliwa na Wakristo na Waislamu, sasa anajiuliza hii dhambi ya udini, inatokea wapi?.

Amesema Watanzania wewe huru kumchagua tena Kikwete kwa misingi ya mazuri yake, au kutomchagua kwa mabaya yake, lakini sio kutomchagua kwa sababu ya dini yake. Vivyo hivyo kwa Dr.Slaa, wanaompenda, wawe huru kumchagua kwa vigezo vya uwezo wake lakini sio kwa vigezo vya dini yake.

Askofu Kulola, alimalizia kwa kuiombea Tanzania na kuuombea uchaguzi mkuu uwe wa amani, huru na wa haki.
 
Kulola nae asitake kujivunjia heshima yake, najua waTanzania watampuuza, maana safari hii wanampuuza kila anaejiweka karibu na JK,
NISEME jAMBO MOJA, KUMKAPENIA kIKWETE Kwataka moyo, lazima uwe Tahahira kidogo, otherwise huwez, yamemshinda mkapa, yamewashinda kina Butiku, ataweza Kulola mzee wamiaka 90.
 
Tumeambiwa tukuupuuze kwa hiyo tunakuambia umechelewa na tunakuupuza
 
Mmh!

Asante Pasco. Hiyo video itarushwa kwenye Luninga?

Kapima upepo nini? Mbona amespin toka lile karipio lake la mwanzo?
 

Hebu nicheki MS kama anaendana na hizi tabia?
 
Anatafuta sympathy ya nini huyu Askofu?
Ameambiwa kuwa kwanza amkataze mjukuu wake Flora Mbasha kumtumikia Mungu na Kaizari, kwanini akubali binti huyo aimbe nyimbo za Mungu kwenye kampeni za JK?..Kwanini basi asizunguke kwenye vyama vyote kuimba?
Askofu gani mbaguzi namna hii?..Ina maana mgombea mwislamu ni JK tu, kwani hakuna wengine, kwanini kujipendekeza kwa JK?
Kama ana vifaa toka ng'ambo na anataka msamaha wa kodi atumie njia zingine, na si kuvuruga watu!
Nilikuwa namheshimu huyu kizee, sasa naanza kumwona tofauti...!
 
Huyu bwana badom yupo?? Nikiwa kijana mdogo huyu bwana wakati ndiyo anawaka alikuja kule Iringa kupiga mahubiri. Kitu ambacho sitasahau ulipofika wakati wa kuto sadaka, jamaa alianza kusema toka hizo noti nyekundu usilete hivyo visenti kwa bwana. Bwana anakuona mapakamfukoni mwako......!!! Wakati ule nyekundu ilikuwa Tshs 100. That time mimi nilikuwa na Tsh 5.00, ingawa sikumbuki nilitoa kiasi gani (definetly siyo zote) lakini nili-conclude kuwa jamaa yuko after money tu na wala siyo neno la Mungu kama watu wazaniavyo. Mpaka leo nimekuwa mtu mzima naamini kuwa nilikuwa right........!!!

Sasa hii ya yeye kuanza kujiingiza kwenye siasa siku za mwishomwisho, najua naamini kuuwa anafanya hivyo kwa manufaa binafsi.
 
mzee kulola anataka kufa vibaya, mi nasema .sijui ndugu zangu wanaoabudu kwenye kanisa lake.
watu hawataki kusikia la yoyote uchaguzi huu, labda usema CHAGUA SLAA, kataa waleta Mizaha Ikulu.
 
Mimi nadani kwa mzee wetu kuendelea kurudia rudia maneno hayo yeye ndiye atajikuta anachochea hisia hizo za udini.Ninamshauri mzee wetu akae pembeni haya mambo ya siasa yana mambo mengi na inawezekana hajui kinachoendelea.Isitoshe ukweli ni kwamba hayo mambo kuwa UDINI unatumika sasa hayana msingi wowote na ni ya kufikirika na yanazushwa na kusambazwa na watu ambao wanaona wameshindwa kuwashawishi watanzania kwa kuonyesha dira ya nchi (vision), sera za chama.mvuto mkubwa uliopo sasa kwa mfano kwa mgombe kama DR SLAA ni uwezo wake mkubwa wa kiakiri, uongozi, uadilifu na vision aliyonayo kuhusu kuikomboa Tanzania ambayo kwa mtu anayefuatilia uendeshaji wa nchi kisiasa atakiri kuwa mambo kwa sehemu kubwa yanaendeshwa isivyo.Ni kushamiri kwa ufisadi na mambo chungu nzima yanayofanywa na baadhi ya viongozi wetu ambayo hayana tija kwa wananchi na mustakabari wa taifa letu.Hivi sasa watu wana kiu ya kupata viongozi wa kweli na siyo wale waliozoea kuwafanya wananchi hawana akili.Mungu ibariki Tanzania na Mungu awaonyeshe watanzania kiongozi wa kweli atakayewasaidia to reach their destiny.
 
Habaru yenyewe kwa ujumla ina ujumbe wa kujenga na si kubomoa ingefaa tuipokee bila negative comments
 
Habaru yenyewe kwa ujumla ina ujumbe wa kujenga na si kubomoa ingefaa tuipokee bila negative comments

Hapana! Habari hii ina ubaguzi ndani mwake. Inalenga kumtetea Kikwete. isome vizuri. Haiko neutral kama unavyotaka tuamini. Inawasema zaidi wakristo kwamba hawamtaki kikwete kwa sababu ya dini yake; kitu ambacho si kweli. mzee kaangukia kwenye mtego wa ccm.
 

Mtu anayefanya udini na alaaniwe. Magazeti yakigawiwa bure ya kuchafua watu; yapokelewe na kuchomwa moto palepale, si ya bure? Hapa Dar kusanya na kuchoma, popote pale, kusanya na kuchoma; hatutaki udini. Iwe Kikwete au Slaa, ni waTanzania, wote wana dini zao.
 
Kama yalioandikwa hapo ni kweli basi jamaa hafai kabisa kabisa kuwa Raisi ,na kama gazeti limechapisha habari hii basi ndio imetoka ,hapati kura kabisa sio za waislamu tu hata madhehebu mengine yatakuwa hayampi sapoti.
Slaa ameshindwa kuona katika serikali ya Kikwete mna wakiristo wangapi ,Slaa ameshindwa kuona katika serikali ya CCM kuna wabunge wangapi ambao ni Wakiristu ,naogopa alichotaka kusema pengine watu wa dhehebu lake ni wachache ,siujui yeye ni mkatoliki dhehebu ambalo linajiona ndilo lipaswalo kuwa na ukiristu na madhehebu mengine yote yamepotea na yanafaa kuondolewa na kutokomezwa.

Hapa waTanzania kama jamaa huyu akiukwaa uraisi basi tujue tumepanda mkenge.
 
Siku zote malezi mazuri huanza nyumbani, baba humkanya mwanaye!
Kama mnashindwa kumuelewa Askofu basi itawapa shida sana kutambua Udini na athari zake.
 
Leo hii kwa mara ya kwanza nasema hivi...
Kama kweli Dr.Slaa amefikia kusema haya basi tumekwisha... Yaani hata sijui tena nani mbora baina yao!
 

Bora umeweka hii hapa, sumu ya udini imeshawaingia wengi JF, trying to mislead people. Maendeleo hayaletwi na dini yako,kwa sababu huu sio msingi wa maendeleo yetu...Awe mkristo au mwislamu au pagani inahusu nini??
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…