Kuna wakati ulitolewa waraka fulani hapa ambao unazungumzia uchaguzi na dini tukakubaliana tupuuze maana dini haina nafasi kwenye siasa zetu. Viongozi wa siasa na kidini nao wanahubiri sana tuachane na udini. Swali langu, je tunamaanisha hivyo?
Nilishangaa wiki iliyopita gazeti la mwananchi kuambiwa na serikali wanafanya uchochezi. kwa kuwa mimi ni msomaji wa magazeti kila siku nikahisi tu ni kwa vile gazeti hilo linabeba picha ya Dr Slaa akihutubia maelfu ya watu ukurasa wa kwanza hiyo inaonekana ni uchochezi.
Leo nimesoma gazeti linaitwa Al-Huda na jana nimesoma Umma. Sikuamini kama serikali hii hii iliyolitishia mwananchi ndio inayosimamia magazeti mengine pia. Gazeti hilo ambalo ni toleo la october 26-27 limebeba vichwa vya habari kama ifuatavyo:
Padri Slaa alichochea mauaji mwembechai- Alifarakanisha Waislamu, wakristo kutoombana chumvi--Alipinga mihadhara, akifanikiwa atapiga marufuku Hijja---Atapiga marufuku adhana, hataki kusikia mahakama ya kadhi Tz----Asababisha majeruhi Tarime, mauaji Maswa Shinyanga
Vichwa vingine vinasema:
Chadema ipo nyuma ya genge hatari?
Linatawala ikulu nne Africa mashariki.......Linahusuka na utekaji, mapinduzi
Padre Slaa kuja na visingizio vya kuibiwa kura-------Mbinu za Adolf Hitler na chama cha NAZI kutumika
Karatu wamgeuka Slaa............Kura zote kwa Kikwete
Waislamu kuunganisha kura kuchagua kiongozi bora......hawatachagua kiongozi anayehamasisha vurugu na umwagaji wa damu......wamesema kwa kuwa makanisa yanahamasisha waumini wao wamchague padri Slaa, wao waislamu wameamua kuondoa tofauti zao na kumchagua kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza.......wanamnukuu Bi. Mayassa ambaye ni kiongozi wa baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu Tanzania akisema.....Upepo wa kisiasa katika uchaguzi wa mwaka huu mnauona hivyo tujitokeze kwa wingi na kuhakikisha kuwa kura zetu tunampa mwislamu mwenzetu ambaye tunaona anafaa na ana sifa ya kuongoza.
Katika ukurasa wa kwanza pia wameweka picha ya mafuvu ya mauaji ya halaiki ya rwanda na kuonyesha kuwa Tz itakuwa hivyo kama atachaguliwa Dr Slaa
Hadi ninavyoandika hapa siamini kuwa serikali inaweza kuruhuru gazeti kama hili liuzwe kwa wananchi. Au serikali ina kengeza? Je, gazeti lingesema hayo dhidi ya 'Dr' Kikwete lingeruhusiwa kuuzwa? Tunahubiri amani bure kama hatuko tayari kukabili wale wanaotaka kuvunja amani eti tu kwa kuwa wanamshambulia mpinzani wetu. Rwanda walianzia hapa wakatumia magazeti uchwara kama haya kuleta chuki, mwisho watu wakachukua mapanga. Wasomi wa Tz tutalaumiwa kama tutawaachia wanasiasa wenye wepesi wa mawazo watugawe kwa kuwa tu wanaitaka sana ikulu. Tuamke tupinge mambo haya kabla hatujachelewa
posted by:
Mkerio
Junior Member
Join DateSun Mar 2006LocationDSMPosts2Thanks0Thanked 4 Times in 2 Posts Rep Power0