Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
sitaki kuamini kwamba gazeti hili lilisajiliwa kwa ajili ya kueneza chuki na udini wa hali ya juu kiasi hiki!
Mimi sio mdini,ila kwa kiwango ambacho gazeti hili limefikia linaanza kunifanya niangalie mambo kwa jicho la udini sasa!

  • Mbona linafanya uchochezi na halikemewi?
  • Mbona magazeti mengine ya wakristo hayaenezi upuuzi kiasi hiki?
  • Mbona magazeti kama mwananchi na mwanahalisi wanatishiwa kufungiwa kwa sababu zisizo eleweka na wachochezi kama hawa wanaachiwa wazi wazi?
  • kikwete anaongelea uchochezi gani wa kidini kila siku au halioni gazeti hili?
  • Au kwa serikali ya kikwete uchochezi wa kidini ni pale tu wakristo watakapo ongea chochote hata kama ni cha maana ila waislamu wakitoa tuhuma nzito za mauaji kama hizi hawakemewi?
  • Chuki hizi zimebalikiwa na nani?
  • sina udini,kama gazeti hili lime fanikiwa kinifanya nianze kufikiria masuala ya udini ni watanzania wangapi wamepata sumu hii?
  • Ili tufanye nini baada ya kutupatia sumu hii ya chuki?

Yepi hayo tena. Hebu yaweke jamvini tukusaidie!
 
Hili gazeti mimi huwa naogopa hata kulisemea. maana liyaandikayo Mhhh,
Lingekuwa gazeti lenye umaarufu na likaenda kinyume na JK basi ni jalalani mapeemaaaaaaa
 
sio hilo tu mkuu, mie nimekuwa nikifuatilia sana magazeti yanayosemwa ya kidini, ni yote ya waislamu na wakristo, endelea kufuatilia utashangaa, ni hatari.
 
sio hilo tu mkuu, mie nimekuwa nikifuatilia sana magazeti yanayosemwa ya kidini, ni yote ya waislamu na wakristo, endelea kufuatilia utashangaa, ni hatari.

magazeti ya mtindo huu hayatufai hata kidogo kwa upande wote, maana imani haina maana kwa nchi kama TZ. Sisi tumekuwa na usawa na tunakuwa ndugu pande zote.
Kwa nini waseme namna ile??
Sijalipenda hata kidogo maana wanavyoandika kwa kweli basi tu!
 
Yapo mawili aluda na sijui linaitwaje lile, pamoja na radio Kheri....mmmhh, ukisikilza utajiuliza mara mbilimbili kama kweli hawa watu wameenda shule au waliokotwa kwenye shule zao zile....
 
Nimeona heading ya uchochezi wa gazeti hili leo asubuhi kuhusu mauaji ya mwembechai, lakini wasikutishe kwani watu wanaohamasishwa kupitia gazeti hili ni handful....... Kuhusu kufungiwa ni kwamba hilo haliwezekani na sababu ni kwamba limeandika habari zinazowafurahisha wakuu wa nchi.

sitaki kuamini kwamba gazeti hili lilisajiliwa kwa ajili ya kueneza chuki na udini wa hali ya juu kiasi hiki!
Mimi sio mdini,ila kwa kiwango ambacho gazeti hili limefikia linaanza kunifanya niangalie mambo kwa jicho la udini sasa!

  • Mbona linafanya uchochezi na halikemewi?
  • Mbona magazeti mengine ya wakristo hayaenezi upuuzi kiasi hiki?
  • Mbona magazeti kama mwananchi na mwanahalisi wanatishiwa kufungiwa kwa sababu zisizo eleweka na wachochezi kama hawa wanaachiwa wazi wazi?
  • kikwete anaongelea uchochezi gani wa kidini kila siku au halioni gazeti hili?
  • Au kwa serikali ya kikwete uchochezi wa kidini ni pale tu wakristo watakapo ongea chochote hata kama ni cha maana ila waislamu wakitoa tuhuma nzito za mauaji kama hizi hawakemewi?
  • Chuki hizi zimebalikiwa na nani?
  • sina udini,kama gazeti hili lime fanikiwa kinifanya nianze kufikiria masuala ya udini ni watanzania wangapi wamepata sumu hii?
  • Ili tufanye nini baada ya kutupatia sumu hii ya chuki?
 
Leta link yake hapa!

kwa kifupi linatoa sana negative juu ya mgombea anayetarajiwa sana kwa Urais, likiegemea sana katika dini,
na limejikita zaidi katika uchaguzi, likimwonesha mapungufu ya kiroho zaidi kuliko yale ya kuliongoza taifa
 
Yepi hayo tena. Hebu yaweke jamvini tukusaidie!
Yeah tuwekee hapa tuyajadili, maana hizi allegations ambazo hazina vidhibiti sio nzuri kwakweli au unadhani kila mtu anasoma hilo gazeti??!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
:nono::nono:Tupe mistari yote tuwekane wazi then tuwe na wayfoward...athante
 
Kuna wakati ulitolewa waraka fulani hapa ambao unazungumzia uchaguzi na dini tukakubaliana tupuuze maana dini haina nafasi kwenye siasa zetu. Viongozi wa siasa na kidini nao wanahubiri sana tuachane na udini. Swali langu, je tunamaanisha hivyo?

Nilishangaa wiki iliyopita gazeti la mwananchi kuambiwa na serikali wanafanya uchochezi. kwa kuwa mimi ni msomaji wa magazeti kila siku nikahisi tu ni kwa vile gazeti hilo linabeba picha ya Dr Slaa akihutubia maelfu ya watu ukurasa wa kwanza hiyo inaonekana ni uchochezi.

Leo nimesoma gazeti linaitwa Al-Huda na jana nimesoma Umma. Sikuamini kama serikali hii hii iliyolitishia mwananchi ndio inayosimamia magazeti mengine pia. Gazeti hilo ambalo ni toleo la october 26-27 limebeba vichwa vya habari kama ifuatavyo:

Padri Slaa alichochea mauaji mwembechai- Alifarakanisha Waislamu, wakristo kutoombana chumvi--Alipinga mihadhara, akifanikiwa atapiga marufuku Hijja---Atapiga marufuku adhana, hataki kusikia mahakama ya kadhi Tz----Asababisha majeruhi Tarime, mauaji Maswa Shinyanga

Vichwa vingine vinasema:
Chadema ipo nyuma ya genge hatari?
Linatawala ikulu nne Africa mashariki.......Linahusuka na utekaji, mapinduzi
Padre Slaa kuja na visingizio vya kuibiwa kura-------Mbinu za Adolf Hitler na chama cha NAZI kutumika
Karatu wamgeuka Slaa............Kura zote kwa Kikwete

Waislamu kuunganisha kura kuchagua kiongozi bora......hawatachagua kiongozi anayehamasisha vurugu na umwagaji wa damu......wamesema kwa kuwa makanisa yanahamasisha waumini wao wamchague padri Slaa, wao waislamu wameamua kuondoa tofauti zao na kumchagua kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza.......wanamnukuu Bi. Mayassa ambaye ni kiongozi wa baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu Tanzania akisema.....Upepo wa kisiasa katika uchaguzi wa mwaka huu mnauona hivyo tujitokeze kwa wingi na kuhakikisha kuwa kura zetu tunampa mwislamu mwenzetu ambaye tunaona anafaa na ana sifa ya kuongoza.

Katika ukurasa wa kwanza pia wameweka picha ya mafuvu ya mauaji ya halaiki ya rwanda na kuonyesha kuwa Tz itakuwa hivyo kama atachaguliwa Dr Slaa

Hadi ninavyoandika hapa siamini kuwa serikali inaweza kuruhuru gazeti kama hili liuzwe kwa wananchi. Au serikali ina kengeza? Je, gazeti lingesema hayo dhidi ya 'Dr' Kikwete lingeruhusiwa kuuzwa? Tunahubiri amani bure kama hatuko tayari kukabili wale wanaotaka kuvunja amani eti tu kwa kuwa wanamshambulia mpinzani wetu. Rwanda walianzia hapa wakatumia magazeti uchwara kama haya kuleta chuki, mwisho watu wakachukua mapanga. Wasomi wa Tz tutalaumiwa kama tutawaachia wanasiasa wenye wepesi wa mawazo watugawe kwa kuwa tu wanaitaka sana ikulu. Tuamke tupinge mambo haya kabla hatujachelewa

posted by:Mkerio
user-offline.png
Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join DateSun Mar 2006LocationDSMPosts2Thanks0Thanked 4 Times in 2 Posts Rep Power0
Nimeona niiweke na huku hii labda itasaidia!! ipo kwenye forums za ucgaguzi mkuu 2010.
 
Kama gazeti linaandika uchochezi ni haki ya yule anaetuhumiwa kulishitaki gazeti mahakamani!! Anaetuhumiwa hapa ni chadema na slaa, sasa kama wanaona wamechafuliwa si waende mahakamani? Kama hawatalishitaki hili gazeti na kudai fidia ya bilioni 1 basi hatuna budi kuamini kuwa chadema na slaa ni genge la mafia na wasiostahiki kupewa madaraka!!!

Sasa nyie humu jf munalia nini? Mbona slaa anamkashifu na kumtusi jk katika mikutano yake na kudai kama jk anaona anachafuliwa aende mahakamani!! Sasa mkuki kwa nguruwe........
 
Yapo mawili aluda na sijui linaitwaje lile, pamoja na radio Kheri....mmmhh, ukisikilza utajiuliza mara mbilimbili kama kweli hawa watu wameenda shule au waliokotwa kwenye shule zao zile....

unamaanisha el madrassa?
 
Nimeona title yake: Padri Slaa alichochea mauaji Mwembechai, Hataki kusikia adhana. Bahati mbaya watu kama mimi hatupati nafasi ya Urais, ningeipata, kesho tu ningelifungia bila kujali ntaongoza nchi kwa wiki mbili au la. Magazeti kama haya yanaendekeza upumbavu. Wanaoyaacha wanaendekeza upumbavu. Upumbavu Upumbavu Upumbavu. Mara nyingi najiuliza hivi Karl Marx hakuwa sahihi kusema "Dini ni mvinyo unaomfanya mtu asahau alikotoka na asijue anakokwenda"?
 
Mara nyingi najiuliza hivi Karl Marx hakuwa sahihi kusema "Dini ni mvinyo unaomfanya mtu asahau alikotoka na asijue anakokwenda"?
inategemea aina ya Imani. mfano imani ya kikristo inakutaka uwapende ,aadui zako na uwaombee wanaokuudhi. Uombee wakuu wa nchi na uwe mptanishi na si mchonganishi. Kwa kifupi inakutaka uwe mzalendo mwenye upendo kwa wote. Magazine za aina hii zinafaa kwa kufungia maandazi tu.
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zachary Kakobe, amesema madai ya udini kwenye Uchaguzi Mkuu ujao ni dhana ya kufikirika isiyo na mantiki na inapaswa kupuuzwa na Watanzania wote.

Askofu Kakobe alisema kuzua jambo hilo wakati halipo, ni kosa kubwa linaloweza kutoa mwanya wa kuliumba na
kuliingiza vichwani mwa watu bila sababu za msingi.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Askofu Kakobe alieleza kusikitishwa kwake na tetesi za madai kuhusu kuwepo mkakati wa wananchi kupiga kura kwa misingi ya udini Oktoba 31 mwaka huu na kufafanua kuwa
jambo hilo ni uzushi na 'linapikwa' kwa makusudi.

"Hili wimbi la maneno ya udini ni dhana ya kufikirika tu, haipo. Inasikitisha tunapoona jambo hili linavaliwa njuga na kusemwa sana wakati huu. Udini usiokuwepo unapotajwatajwa sana, huko ndiko kuupalilia, tunatengeneza kitu
kisichokuwepo na kukiingiza vichwani mwa Watanzania, hii ni hatari!" alionya Askofu Kakobe.

Alipuuza propaganda hizo na kueleza kuwa kama kuna udini, mbona mwaka 2000, alipanda jukwaani kumpinga
mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Benjamini Mkapa (ambaye ni Mkristo mwenzake)?

Alisema kadhalika mwaka 2005, baadhi ya maaskofu walipoibuka na kudai mmoja wa wagombea ni chaguo la
Mungu hakuna aliyedai kuwepo tishio la udini kwenye uchaguzi huo.

"Mwaka 2005 napo wakaibuka baadhi ya maaskofu wakasema mmoja wa wagombea ni chaguo la Mungu, udini haukusemwa, leo hii haya yanatoka wapi? Au wameona kuna mtu fulani hatajwi ndio maana", alisema Askofu
Kakobe.

Alitoa mfano wa Kanisa lake kubadili ratiba ya ibada siku ya uchaguzi mwaka huu ambapo badala ya kufanyika Jumapili, itafanyika Jumamosi ili kutoa nafasi kwa waumini kupiga kura. alisema jambo ambalo hilo si udini bali ni
kuwapa nafasi waumini hao kutekeleza haki yao ya msingi kwa taifa.

Alisisitiza kwamba jambo hilo si udini hata kidogo na mamlaka husika zilipaswa kumpongeza kwa hatua hiyo ya
kuchangia kufanikisha shughuli ya upigaji kura ambayo ni haki ya msingi kikatiba kwa kila raia mwenye sifa.

"Kwa mfano hapa kwangu mimi nimesema ibada zitakuwa Jumamosi badala ya Jumapili ili kuwapa waumini nafasi kushiriki vyema kupiga kura. Mimi nilidhani wangefurahi na kutupongeza kwa kusaidia kufanikisha zoezi hilo. Hapa kwangu wote ni mashahidi, sijamwambia yeyote amchague nani. Kila mtu ana utashi wake. Kumbe basi kila chama kina kura hapa. Wanaopinga mkakati huu wanajua waumini hawa watampigia kura nani? Bila shaka wako
watakaowapigia kura Chama tawala, na wako watakaowapigia kura vyama vya Upinzani.", alisema Askofu Kakobe.

Askofu Kakobe alilinganisha sera zinazoendelea kunadiwa majukwaani na bidhaa zinazouzwa madukani na
kufafanua kwamba wateja daima huvutwa na kununua bidhaa bora.

"Sera ndizo zinazomuuza mgombea, sera ni sawa na bidhaa sokoni au madukani kama vile shati na gauni. Mtu yeyote wa dini yeyote atavutwa na nguo kutokana na kuridhishwa na ubora wake. Shati bora litanunuliwa na yeyote
awe muislamu, mkristo hata mpagani, kudai mtu ananunua kwa misingi ya dini ni dhana potofu ya kufikirika.

"Bidhaa ikiwa nzuri mtu yeyote ataihitaji, hata awe mpagani atainunua tu", alisema Askofu Kakobe na kuzidi
kufafanua:

"Kama sera ni nzuri zitanunuliwa na mtu yeyote mwenye dini na asiye na dini. Sera nzuri ni bidhaa inayouzika kwa
kila mtu. Ni jukumu la wanasiasa kufafanua sera zao zieleweke kwa wananchi. Hapa hakuna suala la udini.

"Wagombea wajue sera ndizo zinazowauza, unaweza kuuza sera zikakataliwa usitafute visingizio, zitengeneze zikubalike. Kelele zinazopigwa sasa kuhusu udini ni vitu vya kufikirika. Ukizungumza sana kitu hata kama cha uwongo baadaye vitakuwepo, ukitaja sana ukabila, udini ndio unaviumba", alionya.

CHANZO: Majira 25.10.2010
 
Sijui kwanini serikali inanyamaza. Soma gazeti la Taifa Tanzania na Habari leo wanavyozungumza udini. Kwa ufupi wananukuu baadhi ya barua zinazodaiwa kuandikwa na maaskafu kuwa wakristo wapigie kura Dr Slaa. JK anapenda sana kutumia magazeti vibaya. Kama asingeyatuma wangeshayafungia. Lakini nina furaha maana udini unawatafuna. Kuna watu wengi nawafahamu ilikuwa wampigie kura JK ila sasa wamegeuka kwa vile wameambiwa na magazeti kuwa msimamo wa wakrtisto ni kumchagua Dr Slaa. Ila pia ninavyomjua JK ni mtu mwenye visasi sana. Akichaguliwa tena wakristo watapata shida sana. Kwa kuwa anahisi wanampinga basi atalipiza kwa mfano kurudisha kodi ya vifaa vya madhehebu ya dini na kuteua watu wa upande wake. Udini wanaleta wenyewe. Ili ujue kuna udini mkubwa, angalia kampeni za CUF. Umewasikia CUF wanakwaruzana na CCM? Wako pamoja kwa vile wote ni dini moja au? Tafakari
 
Jumapili nahudhuria Ibada ya Misa Takatifu Kumuombea Dr. Slaa awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Anayetegemea kuwa dini itamsaidia anacheza mchezo wa mauti.Kitacahosaidia ni sera zenye tija na siyo dini ya mtu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom