Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Zikiwa zimebakia siku tano kabla ya uchaguzi mkuu, Mkuu wa kanisa la Evengelism Assemblies of God, Tanzania, (EAGT), Askofu Moses Kulola, amerudia tena ule wito wake wa kukemea siasa za udini zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa dini nchini, kuchanganya dini na siasa na kusisitiza kufanya hivyo, ni dhambi kwa mujibu wa maandiko matakatifu ya Bibilia.
Askofu Kulola, ameyasema hayo jana, katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii yalifanyika kwa njia ya mtandao wa video mwandishi akiwa Dar es Salaam na Askofu akiwa mjini Mwanza ambako kanisa lake, linafanya maombi maalum ya kuombea amani kwenye uchaguzi mkuu yaliyofanyikia viwanja vya Misungwi mjini Mwanza
Huku akinukuu vifungu vya Bibilia, Askofu Kulola amesema Bwana wetu Yesu Kristo aliwasisitizia Wakristu kumpa Mungu yaliyo ya Kimungu na kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari, hivyo kuchanganya dini na siasa, ni sawasawa na kumpa Mungu ya Kaisari na kumpa Kaisari yaliyo ya Kimungu.
Pia Askofu huyo amekemea vikali harakati za chini chini zinazotaka kuwagawa Watanzania katika misingi ya kidini na kuwataka viongozi wa dini, wawahimize waumini wao kujitokeza kwa vingi, kwenda kupiga kura, na wawe huru kumchagua kiongozi yoyote wanayempenda bila kufuata misingi ya kidini.
Askofu Kulola, amelaani kitendo cha mmoja wa maaskofu wa kanisa lake, kuandika waraka kwa kuwataka waumini wao, wasimpigie kura mgombea fulani wa urais ambaye ni Mwislamu, na kuwataka waumini hao wampigie kura mgombea fulani ambae ni Mkristu. Amesema waraka huoni wa uchochezi na askofu huyo alistahili kuchukuliwa hatua za kisheria.
Amesisitiza Watanzania kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo, kwa kusimamia misingi ya umoja, amani na utulivu aliyotuachia ambapo dini ya mtu sio miongoni mwa sifa za uongozi, hivyo kuwasisitizia watanzania wachague viongozi kwa sifa za uongozi na sio kwa dini za wagombea.
Ametolea mfano toka kwenye Biblia Takatifu kuhusu Mfalme Nebukadreza ambaye hakumwamini Mungu, lakini bado alimfanya kuwa Mfalme wa taifa la Mungu la
Waisraeli, hivyo kiongozi yoyote wa kisiasa atakayechaguliwa bila kujali dini yake, yeye ndiye atakuwa chaguo la Mungu.
Ametolea mfano Nyerere alikuwa Mkristo lakini alikuwa akichaguliwa na kura za wote, Waislamu na Wakristo, vivyo hivyo alipokuja rais Mwinyi, alichaguliwa na Wakristo na Waislamu, vivyo hivyo Mkapa ni Mkristo na alichaguliwa kwa kura za Waislamu na Wakristu halikadhalika Rais Kikwete, awamu yake ya kwanza alipata ushindi wa kishindo kwa kuchaguliwa na Wakristo na Waislamu, sasa anajiuliza hii dhambi ya udini, inatokea wapi?.
Amesema Watanzania wewe huru kumchagua tena Kikwete kwa misingi ya mazuri yake, au kutomchagua kwa mabaya yake, lakini sio kutomchagua kwa sababu ya dini yake. Vivyo hivyo kwa Dr.Slaa, wanaompenda, wawe huru kumchagua kwa vigezo vya uwezo wake lakini sio kwa vigezo vya dini yake.
Askofu Kulola, alimalizia kwa kuiombea Tanzania na kuuombea uchaguzi mkuu uwe wa amani, huru na wa haki.