Ndugu zangu Watanzania, pamoja na ndugu zangu wote waliokuwa wanafuatilia matukio ya bungeni leo. Aaah... ni kweli nimepata watu wengi wakiulizia, aah.. ni kwanini wabunge wa CHADEMA walitoka ndani ya ukumbi wa bunge, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano alipoanza kutoa hotuba yake. Eeenh... moja ni kwamba CHADEMA ni chama chenye msingi, kinachofuatilia, eenh na kuhakikisha kwamba daima kiko consinstent yaani kinatekeleza kile ambacho kinasimamia, aah kwa kuwa tulikwisha kukataa kutambua matokeo ya uchaguzi, na vilevile baada ya kukataa kutambua matokeo tulikataa vilevile kumtambua rais aliyepatikana kwa mchaka.. eenh kutokana na mchakato huo ambao hatuutambui, basi ni dhahiri kabisa aah matendo yetu yaendane na kile tunachoamini.
Wabunge wetu wapo kwenye forum ambayo inasimamia kile ambacho CHADEMA inakiamini. Bunge ni mahali ambapo wabunge wana nafasi ya kubeba bendera ya CHADEMA, na mahali pa kwanza pa kuonyesha kwamba hatumtambui rais ni dhahiri basi ni kwamba ni ndani ya bunge. Kitendo cha leo kilianzia asubuhi, kwa wabunge wetu kutohudhuria hafla ya kumuapisha Waziri Mkuu, kwa sababu isingekuwa na maana kwenda kuhudhuria hafla ambayo inasimamiwa na rais ambaye kimsingi hatumtambui, lakini vilevile ni ishara kwa watanzania kwamba bado eenh tunataka maelezo ya kina kutoka serikali kuhusu kauli tulizokwishakuzitoa.
Baada ya kususia hafla ya leo asubuhi , hatua ya pili ilikuwa kususia hotuba ya rais, na jambo hilo lilifanyika, na hatua ya tatu ni kususia hafla ambayo inatokea leo usiku, ambayo tulikubaliana pia wabunge wetu wasihudhurie. Hizi ni ishara muhimu katika siasa, kupelekea kuipeleka kwa serikali kwamba kuna malalamiko ya msingi ambayo tunayo kuhusu mchakato wa uchaguzi, na ni dhahiri kwamba kama serikali ni makini, kama serikali ni sikivu basi itasikiliza kauli hiyo ya wenzetu ambao huko bungeni. Lakini kauli hizo hazitaishia pale, kama tulivyokwishakutoa katika press conference yetu, tulisema tutatumia forum ndani ya bunge, na forum inje ya bunge kupiga kelele mpaka serikali itusikilize.
Ni nini tunachokihitaji ? Tunahitaji, aah, demokrasia ya kweli katika nchi yetu, tunahitaji uchaguzi ambao utaendeshwa kwa misingi ya misingi ya demokrasia ya kweli. Tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Eenh.. tunahitaji sheria mbovu ziweze kurekebishwa, ili chaguzi zisiendelee kuchakachuliwa kama ilivyotokea safari hii. Kwa hiyo haya ni mambo ya msingi ambayo hakuna mtu yeyote atatuambia tusiyadai, kwa sababu tumelalamika mara nyingi juu ya kat.. ya marekebisho ya katiba, serikali imekuwa si sikivu haitaki kusikiliza, tumedai kuhusu tume huru, serikali imekataa kutusikiliza, tumedai marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo ni kandamizi serikali haitusikilizi, tumedai serikali iache kutumia vyombo vya dola hasa polisi na FFU katika uchaguzi serikali haitusikilizi. Kwa hiyo namna pekee ya kudai haki, ukiona mazungumzo ya kistaarabu hayafanyiki basi unapiga kelele. Na hii ni namna mojawapo ya kupiga kelele.Tukumbuke kwamba CHADEMA tumesema hatuhitaji vurugu, hatuhitaji kuwaambia wananchi waende mitaani kwa maandamano - hata kama ni ya amani kwa hatua ya awali - tukitegemea kwamba serikali itatusikiliza, tukae pamoja au ituahidi kwamba itafanya haya marekebisho kabla ya uchaguzi wa 2015. Bila ya kuchukua hatua kama hizi, 2015 tutarejea kwenye mchezo huo huo mchafu, kura zitaendelea kuchakachuliwa, vyombo vya dola vitaendelea kutumika, watanzania wataendelea kunyanyasika, na ukombozi ambao tumewaahidi watanzania hautaweza kupatikana.
Kwa hiyo kimsingi yaliyotokea ni tafsiri ya press conference ambayo tulifanya siku chache zilizopita pale Dodoma, inawezekana Watanzania wengi hawakuelewa ile press conference. Sasa hii ni tafsiri ya ile press conference, na tunawaomba Watanzania watuelewe kwamba tuliposema tutatumia ukumbi wa bunge, na tutatumia eenh.. fora nyingine nje ya bunge, hii ndiyo maana yake. Inje ya bunge tumesusia hafla mbalimbali, ikiwemo hii ya waziri mkuu kuapishwa, kikiwemo ya chakula cha rais, lakini nahafla zingine zitakazoendelea ambapo rais ataendelea kuwa ndiye mwenye hafla hiyo. Eenh, lakini vilevile tumesema kwamba tutakwenda kwa wananchi kuwaeleza sasa ni nini kimetokea.
Kwa hiyo watu wasishangae kwamba tunafanya mikutano yenye sura ya kufafanua zaidi hatua zetu maana yake ni nini, nadhani hii ni kitu ambacho kila mtanzania anaielewa, na kwa simu tulizopokea mpaka sasa hivi, sms ambazo nimekuwa nikizipokea mpaka sasa hivi, watanzania wengi sana wametusifu , wamepongeza wabunge wetu. Ninaomba Watanzania wote wenye nia njema watuunge mkono katika kilio hiki, lakini tukizingatia kwamba yote tunayofanya yawe kwa msingi ya amani, tusitoke mitaani kama tulivyokwishakuwaomba. Watanzania kama wa Shinyanga ambao wamechakachuliwa kura za mbunge wao waziwazi, Watanzania kama wa Mbozi ambao wamechakachuliwa kura zao waziwazi, Watanzania kama Segerea ambao wamechakachuliwa kura zao waziwazi, tunaendelea kusisitiza kwamba, mazungumzo daima ni njia bora ya kuondoa migogoro. Kwa hiyo tusingependa katika hatua hii eeenh yale yaliyotokea yaendelee kutokea.
Ninawaomba amani, ninawaomba utulivu lakini tuendelee kudai haki zetu kwa njia ambazo zinaweza kuzaa matunda.