outstanding mkuu!.....'Kutomtambua rais' is not in a strict way, kama nilivyosema.
Kitu ninachokiona cha msingi hapa, ni mechanism ya kueka madai yao kwenda kwene ufanikishaji na matokeo yake kwa mustakabali wa taifa.
Bahati mbaya Chadema wanaona kunahitajika marekebisho, mathalan ya muundo wa NEC, wakati vyama vingine vinaona pouwa tu, pengine kwa sababu havikuwa na wagombea wenye ushawishi kama Chadema, sasa huu ni udhaifu wa vyama mbadala, maana it is about the principal not the event or the individuals.
Nakubali kwamba vyama mbadala vina maono na methods tofauti kuhusu uendeshaji wa nchi, lakini kama chama cha siasa hakioni umuhimu wa tume huru ya uchaguzi, na kuipa kipaumbele hii hoja, nadhani huko tuendako ni kiza kinene.
Nadhani bado sheria ya uchaguzi haijaeleweka sana, hasa urais. Dr Slaa akiongelea kujipanga kwa 2015 yuko sawa maana hamna kinachoweza kubatilishwa na sheria nyingine. Sana sana zitakuwa porojo zisizo na tija. Tiyari JK ni rais, kama urais wake ni batili katika sanduku la kura na bado kaapishwa hiyo imetoka. Sasa ni kufanya kazi ya kubadili sheria na kanuni kandamizi zenye kulinda maslahi ya wachache. Tujitahidi kuuona ukweli na hali halisi ya sheria zetu, lakini bado tusiwe mamuma wa kukubali kila jambo hata kama si sahihi-ndiyo mzee!
Ndugu wanajamii ,
Jana nilikuwa naangalia taarifa ya habari TBC 1 , nikakuta mama Akilimali anaongelea kuwa rais kasema uchaguzi umeacha nyufa kubwa ya udini , na huyo mama akawa anachambua kuwa hakukuwa na dalili za udini au udini haukujionyesha kama issue kubwa katika uchaguzi uliopita kama alivyoongea rais !
Je mambo ya Kujiuliza !
1: Haya mawazo ya nyufa za udini yametoka wapi ? na watu gani wameundalia rais hotuba ile ?
2:Lengo ni kupotezea maswala mazima ya uchakachuaji wa kura na wizi uliofanyika ?
3:Kutisha watanzania ili waogope kudai haki zao zilizoibwa ?
Mkandara,
Logic yako ina mawaa yafuatayo.
Dr. Slaa alikuwa mgombea katika uchaguzi, alikuwa mmoja wa wagombea wengi. Kwa hiyo iliwezekana kabisa kwa watu ambao hawamtambui Dr. Slaa kama rais leo, hawakumtambua huko nyuma pia na wala hawakumuona kama ana uwezo wa kuwa rais, wakampigia Lipumba. Kwa hiyo mfano wako, kwa sababu unahusisha uchaguzi ambao unachagua rais kutoka wawakilishi wa vyama mbalimbali, kwa kupitia watu mbalimbali, hauwezi kufanana na uhakiki wa bunge ambao umeletwa bungeni na mtu mmoja, rais Kikwete.
Narudia
Pendekezo la Pinda lililetwa na mtu mmoja, Kikwete. Alilileta kwa kutumia kofia yake ya urais, kama ilivyosemwa katibani. Kitendo cha wabunge wa CHADEMA kushiriki kupiga kura katika uhakiki huu kilikuwa tayari ni kumtambua Kikwete kama rais.
CHADEMA wangeletewa jina limependekezwa na Matonya, wakaambiwa Matonya hajachaguliwa kuwa rais, lakini kampendekeza Chonya wa Chilonwa kuwa Waziri Mkuu, wangeshiriki kupiga kura kuhakiki pendekezo hili ?
Kama wangeshiriki ni kwa sababu gani ? Kama wasingeshiriki ni kwa sababu gani?
Kiranga
Kwenye kupiga kura kuna option mbili kwamba una kubali au unakataa - CHADEMA Walipiga kura ya Kumkataa Pinda ndio wameonyesha kutokubaliana na JK na pendekezo lake .
Nashindwa kuelewa kwanini unag'ang'ania hii kwamba ndio kikubwa, we all know kwamba JK amekwiba kura na sasa ndio amekalia kiti hicho.
Amekuja kuhutubia , niambie option ambayo wewe unaona CHADEMA wangeifanya kwa kufuata logic yako, ninachoona mimi hapa option waliyokuwa nayo na ili ujumbe ufike mbali kwenye media zote, na balozi zote ni kutoka nje , maana kukataa kumsikiliza!!
Usiyeelewa zaidi ni wewe ambaye umeshindwa hata kusema nisipoelewa ni wapi.huyu kiranga haelewi kabisa na hojza zako hazina mashiko mkuu
Kweli nimeamini ...ukimchagua Rais asiye na uwezo wa kuongoza nchi kuna uwezekano mkubwa wa Taifa Kusambaratika. Maana kuna baadhi ya hoja yeye ndo anaeziunda na kuendelea kuzijenga huku akitaka aungwe mkono wa watu mbalimbali.