Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Ndugu wanajamii ,

Jana nilikuwa naangalia taarifa ya habari TBC 1 , nikakuta mama Akilimali anaongelea kuwa rais kasema uchaguzi umeacha nyufa kubwa ya udini , na huyo mama akawa anachambua kuwa hakukuwa na dalili za udini au udini haukujionyesha kama issue kubwa katika uchaguzi uliopita kama alivyoongea rais !

Je mambo ya Kujiuliza !
1: Haya mawazo ya nyufa za udini yametoka wapi ? na watu gani wameundalia rais hotuba ile ?
2:Lengo ni kupotezea maswala mazima ya uchakachuaji wa kura na wizi uliofanyika ?
3:Kutisha watanzania ili waogope kudai haki zao zilizoibwa ?
 
'Kutomtambua rais' is not in a strict way, kama nilivyosema.

Kitu ninachokiona cha msingi hapa, ni mechanism ya kueka madai yao kwenda kwene ufanikishaji na matokeo yake kwa mustakabali wa taifa.
Bahati mbaya Chadema wanaona kunahitajika marekebisho, mathalan ya muundo wa NEC, wakati vyama vingine vinaona pouwa tu, pengine kwa sababu havikuwa na wagombea wenye ushawishi kama Chadema, sasa huu ni udhaifu wa vyama mbadala, maana it is about the principal not the event or the individuals.

Nakubali kwamba vyama mbadala vina maono na methods tofauti kuhusu uendeshaji wa nchi, lakini kama chama cha siasa hakioni umuhimu wa tume huru ya uchaguzi, na kuipa kipaumbele hii hoja, nadhani huko tuendako ni kiza kinene.
outstanding mkuu!.....
copy that......
 
Nadhani bado sheria ya uchaguzi haijaeleweka sana, hasa urais. Dr Slaa akiongelea kujipanga kwa 2015 yuko sawa maana hamna kinachoweza kubatilishwa na sheria nyingine. Sana sana zitakuwa porojo zisizo na tija. Tiyari JK ni rais, kama urais wake ni batili katika sanduku la kura na bado kaapishwa hiyo imetoka. Sasa ni kufanya kazi ya kubadili sheria na kanuni kandamizi zenye kulinda maslahi ya wachache. Tujitahidi kuuona ukweli na hali halisi ya sheria zetu, lakini bado tusiwe mamuma wa kukubali kila jambo hata kama si sahihi-ndiyo mzee!

Unadhani utawezeje kubadili sheria na kanuni kandamizi? ndiyo maaana Dk. Slaa na wabunge wake wameanza move ya kuelekea huku sasa unaposema tusiwe mamuma wa kukubali kila kitu huku wewe mwenyewe ukiona haja ya kubadili kwa sheria hii unajikanganya mwenyewe. Kuwa na Msimamo usiwe POPO CUF ambaye katika Upinzani yupo na serikalini yupo kupitia muafaka huku akilalamika ameachwa katika kambi ya upinzani.
 
Kingo umeiweka hii inshu kawaida sana ndugu, hapa hakuna kujipanga ni haki kupatikana tu. Hata kama kaapishwa ni kutokana na katiba yetu finyu, mfano mzuri kenya hapakuwa na mda wa kujipanga kwa chaguzi zijazo ila haki ilipatikana kipindi kile kile, bongo hatuwezi maana twaogopa mengi, amani yetu haiwezi potea kwa kudai haki.
 
mimi si mwanasiasa mzuri LAKINI namshukuru mungu kwa kunipa uwezo wa kuelewa kuwa KIRANGA is an empty can
 
Ndugu wanajamii ,

Jana nilikuwa naangalia taarifa ya habari TBC 1 , nikakuta mama Akilimali anaongelea kuwa rais kasema uchaguzi umeacha nyufa kubwa ya udini , na huyo mama akawa anachambua kuwa hakukuwa na dalili za udini au udini haukujionyesha kama issue kubwa katika uchaguzi uliopita kama alivyoongea rais !

Je mambo ya Kujiuliza !
1: Haya mawazo ya nyufa za udini yametoka wapi ? na watu gani wameundalia rais hotuba ile ?
2:Lengo ni kupotezea maswala mazima ya uchakachuaji wa kura na wizi uliofanyika ?
3:Kutisha watanzania ili waogope kudai haki zao zilizoibwa ?

nadhani siku zote mtu akifumaniwa anaweweseka na kutafuta kila sababu ili aonekane kuwa alikuwa hana kosa. Udini ni agenda ya JK na wala si vinginevyo. Watanzania hatukuona udini zaidi ya ule wa CUF ambao tumeuzoea. huyu jamaa anataka kpoteza watu mawazo ili wasahau aliyoyafanya ya kuchakachua.

Nawapongeza sana Chadema kwa tukio la kususia hotuba ya mwizi wa kura. Japo wapo wanafiki wanaosema kuwa ni jambo la aibu, lakini walipaswa kuiona aibu kubwa kuliko zote ya JK kuiba kura na kuingia madarakani kwa mlango wa uani. HII NDIYO AIBU KWA TAIFA NA SIYO CHADEMA KUKATAA KUMKUBALI MWIZI. WATANZANIA WENYE ELIMU ZAO NA WANAOJUA HAKI WAKO NYUMA YA CHADEMA.
 
Mkandara,

Logic yako ina mawaa yafuatayo.

Dr. Slaa alikuwa mgombea katika uchaguzi, alikuwa mmoja wa wagombea wengi. Kwa hiyo iliwezekana kabisa kwa watu ambao hawamtambui Dr. Slaa kama rais leo, hawakumtambua huko nyuma pia na wala hawakumuona kama ana uwezo wa kuwa rais, wakampigia Lipumba. Kwa hiyo mfano wako, kwa sababu unahusisha uchaguzi ambao unachagua rais kutoka wawakilishi wa vyama mbalimbali, kwa kupitia watu mbalimbali, hauwezi kufanana na uhakiki wa bunge ambao umeletwa bungeni na mtu mmoja, rais Kikwete.


Narudia
Pendekezo la Pinda lililetwa na mtu mmoja, Kikwete. Alilileta kwa kutumia kofia yake ya urais, kama ilivyosemwa katibani. Kitendo cha wabunge wa CHADEMA kushiriki kupiga kura katika uhakiki huu kilikuwa tayari ni kumtambua Kikwete kama rais.

CHADEMA wangeletewa jina limependekezwa na Matonya, wakaambiwa Matonya hajachaguliwa kuwa rais, lakini kampendekeza Chonya wa Chilonwa kuwa Waziri Mkuu, wangeshiriki kupiga kura kuhakiki pendekezo hili ?

Kama wangeshiriki ni kwa sababu gani ? Kama wasingeshiriki ni kwa sababu gani
?

Kiranga
Kwenye kupiga kura kuna option mbili kwamba una kubali au unakataa - CHADEMA Walipiga kura ya Kumkataa Pinda ndio wameonyesha kutokubaliana na JK na pendekezo lake .
Nashindwa kuelewa kwanini unag'ang'ania hii kwamba ndio kikubwa, we all know kwamba JK amekwiba kura na sasa ndio amekalia kiti hicho.

Amekuja kuhutubia , niambie option ambayo wewe unaona CHADEMA wangeifanya kwa kufuata logic yako, ninachoona mimi hapa option waliyokuwa nayo na ili ujumbe ufike mbali kwenye media zote, na balozi zote ni kutoka nje , maana kukataa kumsikiliza!!
 
Mie nilifikiri hata wapinzani wa CHADEMA walipaswa kusifia njia waliyotumia kufikisha ujumbe kuwa hawakubaliani na mchakato mzima wa kura za Urais. Kuna njia nyingi sana za kutokubaliana na wizi wa kura ikiwemo iliyotumika Kenya. Jee hatuoni kuwa CHADEMA wametuepusha na yale maafa kwa kutumia njia ya kistaarabu kabisa kufikisha ujumbe? Viongozi wa CHADEMA wanajua fika kuwa wakitoa kauli tata ya KIHASIRA yale yaliyotokea Nyamagana na Shinyanga yanaweza kutokea nchi nzima na mkashangaa kuwa yale ya CUF Zanzibar 2001 ulikuwa ni mchezo wa kitoto kwani hii ingekuwa dhahma isiyo mfano. Wananchi wakiwa katika maisha magumu kama ya hapa TZ kwa sasa huwa wanasubiri kauli tuu ili waingie mtaani, kwani huwa wengine wanaponea humohumo kwa uporaji na visasi.
CHADEMA kweli ni wazalendo kwani wameyakwepa hayo kwa kutumia njia ya amani ila kwa upofu wetu tuna walaumu na kuwabeza.
 
icon1.gif



quote_icon.png
Originally Posted by Atigi
Rais na serikali siyo halali usichoelewa ni nini? Hao wamechaguliwa na NEC siyo wapiga kura.



Kwenye uchaguzi huu hata CHADEMA wamepata wabunge wengi kumbe nao wamechaguliwa na NEC?


Ni kweli CHADEMA wamepata wabunge wengi, waliochaguliwa na WANANCHI na sio NEC, hilo ukae ukijua. PILI, hakuna wananchi waliokesha kwenye vituo vya wasimamizi wa kupiga wakidai matokeo kwa ajili ya wabunge wa CCM hii pekee inaonesha kwa kiwango gani wamechoka na udhalimu uliofanywa na CCM. WABUNGE wa kweli ni wale ambao wananchi wamewapa dhamana wa waongoze na si kuawatawala, hawa ni CHADEMA, na WABUNGE walio chaguliwa na NEC wamepewa dhamana ya kutawala na sio kuongoza, hawa ni CCM . Vivyo hivyo kwenye URAIS aliyepewa dhamana ya kutawala na NEC ndie anaetawala kwa sasa, tambua huyu siye aliyepewa dhamana na wanachi ya kuongoza na kuwaongoza. HII NDIO HOJA KUU NA NDIO Dr W SLAA amefafanua.
 
jana chadema wanetumia njia ya haki na amani sana wala hakuna utata. ujumbe umefika vizuri
 
Kiranga
Kwenye kupiga kura kuna option mbili kwamba una kubali au unakataa - CHADEMA Walipiga kura ya Kumkataa Pinda ndio wameonyesha kutokubaliana na JK na pendekezo lake .
Nashindwa kuelewa kwanini unag'ang'ania hii kwamba ndio kikubwa, we all know kwamba JK amekwiba kura na sasa ndio amekalia kiti hicho.

Amekuja kuhutubia , niambie option ambayo wewe unaona CHADEMA wangeifanya kwa kufuata logic yako, ninachoona mimi hapa option waliyokuwa nayo na ili ujumbe ufike mbali kwenye media zote, na balozi zote ni kutoka nje , maana kukataa kumsikiliza!!

1. Kura ilikuwa ya siri, habari ya nani alipiga vipi kura ni propaganda, Hata wabunge wenyewe hawajui wenzao walivyopiga kura. Kila mtu anajijua yeye tu alivyopiga kura.


2. Hata ukipiga kura ya Hapana, maana yake unakubali Pinda alistahili kupigiwa kura, maana yake unakubali aliyependekeza jina la Pinda ana mamlaka ya kupendekeza hilo jina, maana yake Kikwete unamtambua kama rais.

Sasa CHADEMA washamtambua Kikwete kama rais, halafu wanataka kusema hawamtambui, wanatuchanganya.

Kina Tundu Lissu na Mnyika si walitoa madukuduku yao kuhusu uchaguzi wa PM? Si walisema habari za serial numbers and all? Mbona hawakusema aliyeleta jina si rais tunayemtambua kwa sababu hii na ile ?
 
yeye ndo mwenye kuleta udini kwani tumeshuhudia dini yake ikiwaambia waumini wake kuwa kuliko kuchagua kafiri bora kula ya zao apigiwe lipumba, sasa huo udini nani anauleta? Hapohapo anamtumia membe kuwaletea watanzani mahakama ya kadhi wakati hilo si swala la kitaifa bali ni swala la dini ya kislamu,huyu mkwere hana jipya aende zake msonga akauze machungwa
 
Huyu mkuu wa nchi amekemea udini baada ya uchaguzi lakini ukiangalia uteuzi wa wabunge watatu wa mwanzo tu umejaa udini mtupu. sasa sijui anafikiri watz ni vipofu au.
ukiangalia serikali yote ya Muungano kuanzia rais, makamu, rais wa zanzibar, makamu wake wote wawili. Sasa hapo hakuna udini kweli??
 
huyu kiranga haelewi kabisa na hojza zako hazina mashiko mkuu
 
Kweli nimeamini ...ukimchagua Rais asiye na uwezo wa kuongoza nchi kuna uwezekano mkubwa wa Taifa Kusambaratika. Maana kuna baadhi ya hoja yeye ndo anaeziunda na kuendelea kuzijenga huku akitaka aungwe mkono wa watu mbalimbali.
 
Kweli nimeamini ...ukimchagua Rais asiye na uwezo wa kuongoza nchi kuna uwezekano mkubwa wa Taifa Kusambaratika. Maana kuna baadhi ya hoja yeye ndo anaeziunda na kuendelea kuzijenga huku akitaka aungwe mkono wa watu mbalimbali.

Wakati wa uchaguzi JK na CCM walituingiza kwenye udini, angetumia akili na busara kidogo kuteua wabunge wa dini mchanganyiko. ana nafasi kumi, kama hao watatu anawapenda sana, basi angeteua angalau sita achanganye na kuonyesha wananchi kwamba yuko na dini zote
 
Mimi naona huyu JK anataka kutugawa kidini, maana hata huo udini kila siku anaoongelea hata siuoni, atupe mifano ya huo udini ulikuwakuje na ni akina nani ambao walikuwa wanahubiri huo udini, kiongozi wa nchi kuendelea kuhutubia majukwaani mambo ya udini ni hatari kwa taifa hili, maanake nini, sasa watu wanaanza kufuatilia kwa undani kauli yake, na matokeo yake, kwa huu mfano mdogo tu, Rais Muslim,makamu Musilim,ZNZ kuanzia raisi na makamu wote wa raisi muslim, sasa haoni kuendelea kuhutubia mambo ya udini, wakristo wanaweza wakaona wao ndo waathirika namba moja ya kauli ya raisi??.
Namuomba JK aache kutoa kauli hizo zenye utata wa kuligawa taifa letu lililo achwa na mwalimu likiwa salama na amani tele iliyotukuka.


Pamoja tutaijenga Tanzania pasipo kuhubiri mambo ya uchochezi yasiyo na ukweli wowote
 
Kwa utaratibu na Siasa za Tanzania ni ngumu sana KUmtenga raisi kwa kila kitu, siasa za Tanzania Ziko mikononi mwa raisi, raisi ndo kila kitu, na kila mtu analijua hilo na hata Chadema wanalijua hilo, Mtu anaposema Chadema wasusie Bunge, basi Chadema inawpasa kuwasusia Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Mawaziri wote, Wakuu wa Mikoa wote, Wakuu wa Wilaya wote, makatibu na makamishna wa wizara zote, Mlolongo wa uteuzi wa Rais ni mkubwa mno,
Kwa siasa kama za Tanzania ambazo zinampa Raisi madaraka makubwa inakupasa utumie njia yenye akili sana ili kuonyesha kutomtambua Rais, Vinginevyo ni kuipeleka nchi kwenye vita moja kwa moja,
Raisi wa Tanzania keshatangazwa na ndio imetoka hiyo, lakini je alipatikana kihalali? kama sio kihalali na uwezo wa kumtoa hakuna nini kifanyike? Chadema wanalijua hilo la kugomea kila kitu (uteuzi wake) haliwezekani, lakini kuonyesha malalamoko yao ni kumgomea Rais yeye mwenyewe (Kwamba wewe hatukukubali), Hizo teuzi zake hakuna jinsi ya kuzipinga ni nyingi kuliko maelezo (Kila kona unakutana na mtu aliyeteuliwa na Rais), lakini kwa kuanzia hapo kwa raisi taratibu (ikieleweka na Jamii) itashuka mpaka kufika kwenye hizo teuzi zake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom