Kiranga kufikiri hakufanani siku zote. Punguza munkari sheikh!Afadhali mie empty can, wewe ni "empty can't"
Hivi ni lazima kwa uongozi wa Chadema kusema wanamtambua Kikwete kama Rais ili apate uhalali wa kura Rais? Sote tunajua tume imemtangaza kuwa ni Rais na kisheria ni Rais; lakini hakuna mahali ambapo Mtanzania analazimishwa kumtambua kwani kumtambua au kutomtambua hakumfanyi asiwe Rais. Lakini dhamira safi ikisema haimtambui ni kwa ajili ya dhamira hiyo.
Mkuu MwanakijijiHata kama watu hawakubaliani na kilichotokea, ni muhimu kutambua umuhimu wake katika siasa za Tanzania. Kuna mambo ambayo Tanzania bara hayakuwahi kudhaniwa yanaweza kutokea lakini safari hii karibu yote yametokea. Kuna watu ambao wanapenda kuona Tanzania ya zamani ambapo mtu akisema "umoja na mshikamano" basi wote wanapanga foleni na kadi zao zimeandikwa "umoja na mshikamano".. wakiulizwa wana umoja na mshikamano kwenye kitu gani? ndipo songombingo inapoanza. Tanzania ya sasa ni Tanzania yenye kuhitaji majibu.
- Hivi, kwanini Tume ya Uchaguzi haikuamua kusitisha hata kwa muda kutangaza matokeo ya Urais ili kusikiliza malalamiko ya CHADEMA? Kwa sababu tume hailazimishwi na sheria kutangaza matokeo katika kipindi fulani ingeweza kuchelewesha hata kwa siku mbili ili kusikiliza na kupitia ushahidi ambao Chadema walisema wanao. Ingeupitia na kuamua na kuendelea na matangazo au kufanyia kazi. Kwanini hawakusitisha kutangaza kura za Rais?
- Kwanini, tume ilikataza vyombo vya habari visitangaze matokeo ya Urais kutoka Tanzania bara wakati matokeo yake yalikuwa tayari majimboni na badala yake ikaanza kutangaza matokeo ya Zanzibar, Mtwara na Lindi wakati yale ya sehemu za Dar, Mwanza, Tanga Mjini, Mbeya, Arusha Mjini yalikuwa tayari kabla ya kura za Zanzibar kuanza kutangazwa?
Dr., Since umeanza kwa kuongelea consinstency, swali langu mimi ni, kama hamumtambui Kikwete mlipopiga kura pendekezo lake bungeni kwa kiti cha Waziri Mkuu, mlikuwa mnapigia kura pendekezo la nani? Je pale mlimtambua halafu mkashauriana na sasa hamumtambui? Kuna consistency gani hapo ?
Utasemaje unaonyesha kutomtambua rais kwa kutohudhuria hafla ya kuapishwa Waziri Mkuu wakati umehudhuria, kushuhudia na kushiriki upigaji kura zilizompitisha huyo waziri mkuu aliyependekezwa na rais ? Kipi muhimu, kura za kumpitisha au tafrija ya kumpongeza baada ya kupitishwa ? Hivi kweli mnataka tuwachukulie seriously kwa mwendo huu ?
Muda wa ishara umekwisha, tunataka matendo yenye lengo la kuleta mabadiliko ya kisheria.
OK, kwanza unasema serikali haiwasikilizi, halafu unaendelea kusema unategemea serikali itawasikiliza, au hata inaweza kuwaahidi marekebisho. Wanasema kufanya kitu vile vile na kutegemea matokeo tofauti ni kichaa, sasa CHADEMA mnafanya nini tofauti na nyuma ? Au "mnapiga makelele" tu kama unavyosema mwenyewe mkitumaini CCM wataona haya na kuwapa mabadiliko katika kisahani cha dhahabu? Kama hawana haya na hawawapi mabadiliko je, mtafanya nini ?
Again, huwezi kushiriki kumpitisha Waziri Mkuu, halafu ukasusia hafla, halafu uniambie uko serious. This is a big joke.
Mimi ningekusifu na kukupongeza zaidi kama ungesusia kila kitu cha rais huyu, pamoja na kupigia kura uhakiki wa chaguo lake la waziri mkuu.
Njia unayotumia wewe haizai matunda, actually ni the worst of both worlds. Wataka mabadiliko wa kweli kama mimi tunakuona haufanyi vya kutosha, wapenda ushirikiano wa vyama vya kisiasa watakuona unawagawa Watanzania kwa misingi ya vyama. Utawapata wafuasi wako hao hao wanaoamini CHADEMA kama dini.
Kama kweli unataka kutomtambua rais huyu itisha migomo na maandamano nchi nzima.
La, mkubali uende kutaka mabadiliko bungeni. Zaidi ya hapo unazua maswali mengi kuliko majibu.
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.
hiyo point mkuu kuna watu inafaa wapimwe iq yao kabla hawajaingia kwenye uongozi!kuna haja ya kupima iq za hawa jamaa. Maana wanaongea vile midomo inavowatuma na ndo maana hata miili yao huwa haioneshi ushirikiano wakati wa kuongea, wanabakia wakiongea taarabu tu.!!!!!!!!!!
Mkuu Mwanakijiji
Maswali hayo majibu yake hatuwezi kuyapata wakati rais alilshatangazwa.CHADEMA wana matokeo yao ya kila sehemu wayalete basi na kuonesha ni nani alishinda..
mie huw sipendi story na speculation bila kuwapo na facts...tutaanzia hapo ila hili suala la kulia lia tu